UDOM hii si haki

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,548
Chuo kikuu cha Dodoma kimetoa tangazo kwenye gazeti la Daily news la tarehe 12/11/2012, ukurasa wa 20, kuhusu usaili wa watu waliomba kazi chuoni hapo katika kada zote. Tangazo hili limeeleza kuwa tarehe ya usaili huo ni tarehe 17/11/2012. Ili kujua kama upo kwenye orodha ya watakaosailiwa tangazo hilo limeeleza kuwa unatakiwa kutembelea tovuti ya chuo hicho. Ch kushangaza mpaka naanzisha huu uzi hakuna orodha yoyote iliyowekwa katika tovuti ya chuo hicho. Je hii ni haki? au ndio tayari watu wameshapatiwa kazi hizo kwa ujanja ujanja...naombeni msaada wana JF kwa kuwa na mimi nilituma maombi.
 
Hiyo ndo UDOM bwana CHOO kibubwa east Africa.
 

Acheni kutoa lawama za Kipuuzi kila wakati, wewe uliingia lini?
Wakati website yao ipo kwenye matengezo kuna link chache tu ziliwekwa ikiwemo na majina ya watu walioitwa kwenye interview, na hata ukiingia kwenye nafasiza kazi na tenda majina yapo.
Sasa muda mwingine muwe watafutaji sio mnabip ili mkimbilie jukwaani kutoa lawama na matusi, DUMB NUT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…