Udiwani umekuwa chaka la mafisadi, wajinga na wanyan'anyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udiwani umekuwa chaka la mafisadi, wajinga na wanyan'anyi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Jan 29, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sina shaka kabisa kwamba udiwani ni ngazi ya muhimu katika kuwakilisha mawazo ya wananchi katika vyombo vya kiutendaaji, hasa Wilayani na taifa kwa ujumla.Lakini sina hakika kama kiungo hiki muhimu kinapewa uzito unaostahili.Mara nyingi tumesikia madiwani ambao kama wamesoma ni kidogo sana.Diwani wangu ameishia darasa la tatu,tena alikimbia shule kwa sababu wakati fulani huko nyuma mzee Ruksa alipokuwa Rais, biashara ya fegi ilitamba sana.Akawa yeye ni muuza fegi kwenye mabasi na mdokozi mkubwa wa mizigo ya abiria.Mpaka leo fani ya wizi pamoja na udiwani wake hajaiacha.Pia ni mshirika mkubwa wa vijana wanaoshusha mizigo kwa njia ya kushangaza kigogo kwenye malori, maarufu kama "shushashusha".Sijui kama ndugu yangu Masha ana taarifa ya wizi huu wa aina yake!Yeye pia ni mnunuzi mkubwa wa bidhaa hizo za wizi.Madiwani wengi nchini wanatuhumiwa na vitendo vya ajabu ajabu kama hivi,ikionyesha wazi kwamba hatuko makini sana na ngazi hii muhimu sana ya uongozi. Nimetangulia kusema kwamba ngazi hii ni muhimu sana katika kuleta maendeleo ya wananchi.Siku zote nimejiuliza,hivi kweli mwenye elimu ya darasa la tatu anaweza kuchambua matatizo ya wanachi na kuyawakilisha kwenye vikao vya halimashauri kwa utekelezaji?Jamani hivi tuna kwenda wapi?Sidhani hata kama mtu kama huyu anajua kwa nini ni diwani.Karibu tunaingia katika uchaguzi wa 2010.Inabidi tuwe na mtizamo tofauti.Kazi ya udiwani sio ndogo,ina hitaji mtu mwenye ufahamu na anayeweza kuchambua mambo(diagnostic).Ni vema basi akawa mtu ambaye ana ufahamu mzuri,mwenye "proven intergrity",na ambae angalau ana Diploma,tena "inayofahamika" sio ya mtaani.
   
 2. A

  AndrewMwanga Member

  #2
  Jan 29, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa jinsi dunia inavyoendelea kwa kasi hasa nchi za magharibi nakubaliana nawe tunahitaji viongozi awakilishi wa wanachi kuwa na elimu ya kutosha na upeo wa kujua dunia inaelekea wapi nanini mahitaji ya wanachi kwa kwasasa na kwa baadae.
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tikkera, mtu anaweza kuwa darasa la 3, na akafanya mazuri kama ana wito tu wa kuwa kiongozi. Kama umeingia katika uongozi kutegemea kupata jambo fulani na si kusaidia raia hata uwe na PhD utavurunda. Kwani walioingia mikataba ya kununua RADA, kujenga maghorofa ya BOT, EPA nk ni watu wa darasa la 3?.

  Kuhusu wizi wa diwani wewe/nyinyi kama wananchi mmechukua jukumu gani?. Kama mna ushahidi siku hizi sio lazima kwenda polisi, simu za makamanda wa polisi ziko wazi, ni kupiga na kutoa huo ushahidi kuwa jamaa mwizi. Kama si hivyo yaweza kuwa majungu...
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Diwani ni daraja muhimu kati ya halmashauri za miji na wadi zake, Diwani ndie ambae uidhinisha bajeti ya matumizi ya halmashauri yake na ndie usimamia shughuli za maendeleo katika wadi yake. Zaidi diwani anaweza kuwa Meya wa Jiji/Halmashauri na ni baada ya kuchaguliwa na madiwani wenzake.

  Kuwa diwani hakuitaji sifa nyingi kama zile za ubunge ama uprezi, aidha kikubwa kinachoangaliwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujikimu bila ya kutegemea malipo ya vikao vya madiwani, sifa hii kwa muda mrefu imekuwa ikipuuzwa na hatimaye Halmashauri nyingi zimekuwa zikijikuta zina Wadiwani watendaji badala ya watunga sheria ndogo ndogo na waandaji wa sera.

  Tatizo hili nahisi ni mojawapo ya tatizo ambalo Mhe. Diwani wa Tikerra analo, hivyo kumfanya ashindwe kuacha tabia yake ya awali ya udokozi. Hapana shaka sasa anautumia Uheshimiwa wake kwa kupora zaidi.

  Wasomi wengi hawapendi kuwa madiwani,anaweza kuwa Diwani kwa lengo la kutaka kuwa meya au kwa kutaka kujenga umaarufu kabla ya kuwania nafasi ya juu zaidi ya Ubunge. Kundi lingine ni lile ambalo linataka kunufaika binafsi na kinga ya Udiwani katika shughuli zao. Hili ndio kundi ambalo limegeuza Udiwani kama ajila na kutwa utawakuta katika ofisi za Halmashauri zao kama vile ni watendaji.
   
 5. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani jamaa hasemi madiwani wawe na PhD afterall PhD pekee siyo kipimo cha usomi.Lazima tukubali sasa kuwa uongozi siyo kipaji pekee.Haya mambo ya kuwa na kiongozi wa darasa la tatu eti kwa vile ana wito ni ya wakati wa kina nyerere na kawawa siyo wakati wetu huu.
  Kama walivyosema wengine,udiwani ni nafasi nyeti.Sasa anatokea mtu kibaka tu,aliyekimbia shule mnamchagua awe diwani.Sasa kwa mfano huyu mtu atawezaje kusimamia maendeleo ya elimu kwenye kata yake wakati mwenyewe alikimbia shule kwavile hakuona umuhimu wa elimu?
   
 6. l

  lageneral Member

  #6
  Jan 30, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli elimu za madiwani wengi zinasikitisha.Tuko katika dunia ya sayansi na teknolojia,ambapo kitu muhimu ni elimu.Wakati umefika sasa kuweka kiwango cha elimu katika ngazi za uongozi wa wananchi.Tunaweza kuanza na kusema kila diwani lazi awe na elimu ya kidato cha sita.
  Haishangazi kuona kazi za halmashauri zikifanywa na serikali kuu kwa sababu madiwani hawajui wajibu wao.
   
Loading...