Udini wamtisha JK; Amtuma Wassira kusuluhisha Waislamu, Wakristo...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]ALHAMISI, JANUARI 24, 2013 05:05 NA WAANDISHI WETU



*Amtuma Wasira kusuluhisha Waislamu, Wakristo
*Mzozo wa kiimani wazusha mtafaruku shuleni

MGOGORO wa udini unaoendelea kulitikisa taifa, umeonekana wazi kumshtua Rais Jakaya Kikwete, ambaye amelazimika kumtuma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira, kwenda mkoani Mwanza kukutana na viongozi wa madhehebu yote ya dini.

Hatua ya Rais Kikwete kumtuma Waziri Wasira, imekuja siku chache baada ya kuibuka mvutano mkali kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu kuchinja wanyama. Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete amemtuma Waziri Wasira ambaye ameondoka leo asubuhi kwenda mkoani Mwanza kukutana na viongozi wa madhehebu yote.

Habari za kuaminika zilizopatikana kutoka Ikulu mjini Dar es Salaam, zinasema Waziri Wasira anatarajia kuwasili kwa ndege leo na moja kwa moja kukutana na viongozi hao, ili kuondoa tofauti zilizopo.

“Waziri Wasira anaondoka kwenda Mwanza kesho (leo), kwa ajili ya kukutana na viongozi wa madhehebu yote ya kidini mkoani Mwanza, tunatarajia atatumia uwezo wake wote ili kuona wananchi wanaishi kwa amani.

“Taarifa tulizo nazo ni kwamba, kikao hicho kimeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo… kama utakumbuka hivi sasa kuna mvutano mkubwa kati ya Waislamu na Wakristo,” kilisema chanzo chetu.

Hatua ya Waziri Wasira kwenda huko, inatokana na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Ndikilo, kutoa kauli ya utata mwishoni mwa mwezi uliopita, ambapo aliwataka Waislamu ndio waendelee kuchinja na Wakristo wasifanye hivyo.

“Unajua mwishoni mwa mwezi uliopita, RC Ndikilo alikwenda katika eneo la Nyehunge na kukuta kuna bucha za Waislamu na Wakristo, lakini kubwa zaidi ni pale alipokuta mchungaji mmoja amechinja ng’ombe, kutokana na ugeni wake aliokuwa nao, jambo hilo lilizua mambo mengi.

“Baada ya kuona hivyo, Ndikilo alitamka bila wasiwasi kwamba Waislamu ndio wenye haki ya kuchinja, kauli hii ilisababisha azomewe na watu waliokuwa wamekusanyika pale na kuamua kuondoka,” kilisema chanzo chetu.

MTANZANIA ilipomtafuta Waziri Wasira ili kupata ukweli wa safari yake, alikiri na kusema lengo ni kutaka kuona Watanzania wanaishi kama ndugu.

“Naondoka kwenda Mwanza kesho (leo), kwa ajili ya kukutana na viongozi wote wa dini ili kuzungumza nao masuala mbalimbali, tunataka kuona Watanzania tunaishi kama ndugu, maana ndivyo tulivyolelewa na kukua katika mazingira haya,” alisema Waziri Wasira.

Alipoulizwa ni sababu gani kubwa iliyomsukuma, Waziri Wasira hakuwa tayari kusema zaidi ya kudai “naomba utume waandishi wako najua pale Mwanza wapo, waje wasikilize nini nasema na kisha wawajulishe Watanzania,” alisema.

Habari zaidi kutoka Mwanza, zinasema baada ya mazungumzo hayo, Waziri Wasira anatarajia kuelekea mkoani Geita, ambako nako inaelezwa hali hiyo, imeanza kujitokeza.

Mwishoni mwa mwaka jana, Padri wa Kanisa Katoliki Mpendae, visiwani Zanzibar, Ambrose Mkenda, alijeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake wakati akitoka kanisani.

Padri huyo, alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake na kujeruhiwa katika sehemu ya kichwa.

Alitibiwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Katika tukio jingine, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga, alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Kufuatia matukio hayo, viongozi mbalimbali wa Serikali walisema Serikali itawasaka kwa udi na uvumba wahusika ili wafikishwe mbele ya vyombo vya dola kujibu tuhuma zinazowakabili.

DODOMA

Katika hali ya kushangaza, mkoani Dodoma, juzi waumini wa dini ya Kiislamu wenye itikadi kali walivamia Shule ya Msingi Kigwe, iliyopo wilayani Bahi na kutoboa masufuria yanayotumika kuwapikia uji wanafunzi.

Waumini hao, waliokuwa na silaha za jadi, walifikia hatua hiyo, wakidai masufuria hayo yalitumika kuchemshia maji ya kunyonyolea nguruwe.

Kabla ya kuanza kushambulia masufuria hayo, walidai Mkuu wa Shule hiyo, Mathias Mbowe, huwa anatumia moja ya masufuria kuchemshia maji ya kunyonyolea nguruwe kisha kwenda kuuza nyama mnadani.

Akizungumzia tukio hilo, Shekhe wa Wilaya ya Bahi, Hassan Khamisi, alisema waumini hao waliharibu masufuria ya shule, baada kupata taarifa kuwa moja ya masufuria hutumika kuchemsha maji ya nguruwe.

“Hali hii iliwafanya waumini wa eneo hilo ambao watoto wao wanasoma katika Shule ya Msingi Kigwe na kupatiwa uji wakiwa shuleni kupatwa na hasira kwa kuwa watoto wao wanalishwa haramu,” alisema Shekhe Khamis.

Ofisa Elimu wa Wilaya hiyo, Mary Methew, alilaani kitendo hicho akisema hakikuwa cha kiungwana kwa kuwa waumini hao walijichukulia sheria mikononi.

“Siyo kweli kwamba masufuria hayo yanatumika kwa jili ya kuchemshia maji kama walivyodai waumini hawa… kitendo cha kutoboa masufuria kitasababisha wanafunzi wa shule hiyo kukosa huduma ya kunywa uji shuleni,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alikiri kutokea kwa tukio hilo.

Alisema baada ya kutokea kwa vurugu hizo, polisi walikwenda eneo la tukio, lakini walikuta waumini hao wakiwa wameshatawanyika.


Alisema polisi, wanaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo.
 
Ni kwanini Rais KIKWETE anakimbia MASUALA NYETI ya UDINI na UKABILA?? Wakati alikuwa huru kuvitangaza 2010 akiwa anagombea URAIS???

AU HANA HEKIMA ya KUZUNGUMZIA>>>
 
Wakati wa kapeni za uchaguzi wa 2010...misikiti mingi kariakoo ilikuwa ina hubiri kura ya muislamu kwa muislamu mwenzie na ccm/serikali ilikaa kimya kwa kuwa wao ndo wangenufaika na mahubiri hayo. Nevertheless wakaendeleza kampeni chafu ya kuwa CDM ni chama cha wakristu na Padri Slaa arudi kanisani.

Sasa ile mimba ya uislam na ukristu badala ya watanzania inetoa majibu kwa hiyo wasistaajabu... Sasa wamehamia kwenye ukanda katika kukichafua chama cha CDM..wasubiri hiyo mimba itaanza kukuwa nayo itafikia mahali nayo itajibu. Mathalani watu Mtwara wanadai maisha mazuri na matumizi ya gesi yanayo jali maslahi ya kule inapotoka nao mmeshawaita wahaini...Hakuna anayetaka kuwasikiliza hiyo nayo ni kansa kesho na kesho-kutwa watu wamtwara watasema tulipokuwa tuna pambana na mafisadi hamkutusaidia hivyo kila kitu ni mtwara

Siasa za divide and rule ni sumu ambayo bado inaziumiza nchi nyingi za kiafrika, sasa unapoona watu wanashabikia hilo ( Nape Nnauye, Wasira na Mwigulu) juwa hawatutakii mazuri kabisa watanzania
 
what goes around comes around, amelikoroga na atalinywa! udini aliouumba mwenyewe ili aingie madarakani utamtokea puani.
 
Kuna tangazo la bidhaa moja inasema hivi"Maumivu ya kichwa huanza polepole......"
 
Style hii ya menejimiment inaliingizia Taifa hasara kubwa.

Matatizo yanafugwa, yanaachwa yakomae na kuwa sugu, then ndio watu wanajikongoja kuchukua hatua.

Kwa kiongozi, kauli ni silaha kubwa, kauli thabiti inatosha kutoa msimamo na kurekebisha mambo!

Inasikitisha, kauli sahihi hazitoki katika muda muafaka.

Zinapotoka zinakuwa ni dhaifu, then kupelekea matumizi ya ovyo ya muda na rasilimali za Taifa.

Hakika kuongoza ni kazi, kazi hii ya kujifunza kunyoa daily inasikitisha.
 
Yeye kwa nini anakwepa? Anatuma wasaidizi wakati 2010 walikuwamstari wa mbele kutangaza udini, 2010 alimtuma Membe Mwanza leo wasira kwa nini? Na wassira ni bora angeondoka na Ndikilo kwani ameshindwa kuongoza kwa kushindwa kujua katiba.
 
Wassira huyu mbomoaji wa demokrasia katika siasa ndio anaenda kutumika kupatanisha mambo ya imani? Tusidanganyane. Na hili suala la udini lipo kwa waislam tu. Nashindwa kuelewa waislam wanasumbuliwa na kitu gani hadi wawe hivi. Najua tu labda ni uelewa mdogo wa mambo unaopelekea kutojiamini. Tunawaombea kwa Mungu ili waweze kubadilika na kuujua ukweli. Adui wa mwislam sio mkristo. Ingekuwa hivi basi washia na wasunni wasingeuana. Wote si waislam? Adui wa mwislam ni viongozi wa kisiasa, tena wengi wao wenye imani ya kiislam. Waislam angalieni msije mkachelewa katika kulijua hili.
 
Watu kama Ndikilo ndio wanasababisha sintofahamu katika jamii, ni nani aliyeagiza kuwa waislamu ndio wenye haki ya kuchinja wanyama; au ndivyo inavyosema katiba ya CCM?!

Hivi kweli inaingia akilini kwamba mkristo nina mifugo yangu nyumbani nikitaka kuchinja nikamtafute muislamu anichinjie! ili baadae adai ushuru wa kuchinja au kipande cha nyama kwa sababu gani? au ndio ilani ya uchaguzi ya CCM ya kuongeza ajira!!

Hivi waislamu wakichinja ndio nyama inaiva vizurii au mlaji anakwenda peponi ghafla!?

Ndikilo awambie waislamu waende skuli ili wapate ajira zilizosoma sio kulazimisha deal za kipuuzi.
 
CCM wakati wa kuondoka madarakani watatuachia nchi yetu ikiwa vipande.
Wanachowaza wao ni kutawala tu, bika kujali athari ya njia zinazowaingia madaraka.
WaTanzani wa vizazi vijavyo watakuja kufukua makaburi ya viongozi wa CCM wa awamu hii na kuteketeza kwa moto masalia ya maiti zao.
 
Kama JK au mtu wake wakaribu anafuatilia JF basi ninamuomba na Ustaadhi Ilunga na wawakilishi wa redio Imani nao wawepo kwenye hicho kikao amasivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye mtungi!
 
Kama JK au mtu wake wakaribu anafuatilia JF basi ninamuomba na Ustaadhi Ilunga na wawakilishi wa redio Imani nao wawepo kwenye hicho kikao amasivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye mtungi!

kwanza awali ya yote, waumini wa dini zote watoe sharti la kumkataa mkuu wa mkoa ili ajue kweli tumechukia na umbumbu wake. mkataeni huyoooooooo!!!!
 
Watu kama Ndikilo ndio wanasababisha sintofahamu katika jamii, ni nani aliyeagiza kuwa waislamu ndio wenye haki ya kuchinja wanyama; au ndivyo inavyosema katiba ya CCM?!

Hivi kweli inaingia akilini kwamba mkristo nina mifugo yangu nyumbani nikitaka kuchinja nikamtafute muislamu anichinjie! ili baadae adai ushuru wa kuchinja au kipande cha nyama kwa sababu gani? au ndio ilani ya uchaguzi ya CCM ya kuongeza ajira!!

Hivi waislamu wakichinja ndio nyama inaiva vizurii au mlaji anakwenda peponi ghafla!?

Ndikilo awambie waislamu waende skuli ili wapate ajira zilizosoma sio kulazimisha deal za kipuuzi.

Rais makini asingetuma "msuluhishi" huko Mwanza, ambacho angefanya ni...kumfukuza kazi RC huyo kupitia MEDIA...na hilo lingekuwa suluhisho la kudumu...
 
Kila mchuma janga hula na wakwao! Sasa JK na serikali yake ndio wanavuna walichopanda!
 
Back
Top Bottom