Waislamu mnatakiwa muwe na umoja wa nyuki na sio umoja wa inzi.
Ukilipiga jiwe kundi la inzi kila mmoja ataenda upande wake, hali ni tofauti kwa nyuki ambapo kama ukiwapiga jiwe wote watamtafuta adui na kumtia adabu hali hii ndiyo ipo kwa wakristo amabapo wakisimamia kitu ni mpaka kieleweke tena wanakuja na hoja zenye mashiko. lakini kwa waislamu hali ni tofauti, maulamaa wakisema a dhidi ya serikali, bakwta wanakuja na b matokeo yake ndo kama hivyo tena, wamepigwa mabao na magamba hata kwenye hoja simple kama ya Mahakama ya kadhi. Amkeni, jitengeni na serikali, endesheni mambo yenu kidini zaidi kuliko kisiasa