Udini: Ukweli unaouma tanzania

Udini: Ukweli unaouma tanzania

Status
Not open for further replies.

Wa Busiya

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
326
Reaction score
67
Wahenga walisema,'Ukweli Huuma' wakiwa na maana kuwa siku zote watu huamua kudanganya ili kukwepa maumivu yatokanayo na kusema ukweli. Hali hii ndiyo iliyoikumba jamii ya watanzania miaka ya hivi karibumi. Donda la udini linazidi kukua kutokana na watanzania viongozi wa nchi na raia kuukana ukweli wanaoufahamu kwamba tumeanza kuwa wadini tukiongozwa na vyombo vya habari vya kidini. Fikiria muumini wa dini yoyote kati ya uislam na ukristo.

Mioyoni kila muumini wa dini hizi anafahamu kuwa kuna maumivu ya kimyakimya yaliyolelewa na kukuzwa na viongozi kwa kukataa kusema ukweli ili kuhifadhi dini zao. Kwa mfano; serikali inashindwa kutamka kuwa hakuna sheria ya nani anastahili kuchinja nchini Tanzania badala yake inajiingiza kwenye mgogoro wa kutetea upande mmoja wa dini bila kujua kuwa inachochea mpasuko kwa raia wake.

Nionavyo mimi, Rais au wasaidizi wake wenye dhamana walitakiwa kwanza kutamka kuwa sheria ya nani achinje haipo, kisha iwaombe raia kuendeleza uhusiano wa kuvumiliana au kwamba ziwepo bucha zenye kufuata misimamo ya kidini kwa wenye misimamo yao lakini kwetu wenye misimamo ya wastani tununue popote.

Watanzania wenzangu bila kujali dini zetu, kama kweli tunaipenda nchi yetu basi tusiendekeze udini hata kidogo. Tujifunzeni kwa wenzetu kama Nigeria, Somalia, Syria, Afghanstan n.k. Tukianza kubaguana hakuna atakayefaidi eti kwa kuwa dini yake imapata upendeleo ama vipi. Kwa bahati mbaya tunazitumia dini zetu kwa kivuli cha maagizo ya Mungu na kwamba kwa kufanya hivyo pengine tutakwenda mbinguni!

Niwaombe wtz wenzangu tuanze kufuta doa la udini ambalo wengi limeanza kutusumbua. Tusitegemee serikali
kutusaidia maana tunaona jinsi serikali inavyofanya sanaa juu ya maisha yetu wenyewe.

Tukataeni udini!
 
Kusema kweli hili la kuchinja linanipa tabu kama linaweza kutufanya kugombana.
Kuna mambo mengine ni kuvumiliana tu. Mi bana nikinunua Kuku wangu nampa Muislam kuchinja....
Sijui nani atapiga hodi kuja kupata msosi, kwa nini nimkwaze mwenzangu kwa jambo ambalo haliathiri Imani yangu?

Tena na familia zetu hizi za Kiafrika mtu anakuja kwako bila miadi!
 
Kwa nionavyo mimi, hapa lilipofikia ni Raisi tu kusimama na msimamo wa Katiba basi. Ni kusema kuwa hakuna sheria ya nani achinje - ruksa kila mtu achinje, lakini tutafakari kwamba kwa nini tumefikia hatua hii?

Awaite wazee awaulize. Awaite maaskofu na mashakhe na awaulize. Wanaweza kumsaidia kuleta suluhu. Ni hatari sana kuliacha suala hili mikononi mwa raia bila ufumbuzi. Ule mwanya unazidi kupanuka. Na huko tuendako hapatabiriki kwa hali hii ya Tunduma.

Kusema kuwa tunduma ni Diwani wa Chadema na Mchungaji wa KKKT ati ndo wamechochea naona ni kujitafutia jibu rahisi. Mamlaka ya Raisi pamoja na viongozi wa dini hizi kwa pamoja waweza kuleta suluhu. Kwa nini Raisi anasomewa Itikafu na anapiga tu kelele jukwaani bila kushtuka?

Kwa nini anaacha maaskofu mpaka wanatoa tamko zito namna ile bila kuchukua hatua? Inabidi afanye kitu, tena kabla hali haijawa mbaya zaidi!
 
Kusema kweli hili la kuchinja linanipa tabu kama linaweza kutufanya kugombana.
Kuna mambo mengine ni kuvumiliana tu. Mi bana nikinunua Kuku wangu nampa Muislam kuchinja....
Sijui nani atapiga hodi kuja kupata msosi, kwa nini nimkwaze mwenzangu kwa jambo ambalo haliathiri Imani yangu?

Tena na familia zetu hizi za Kiafrika mtu anakuja kwako bila miadi!

mkuu watu siku hizi wanapenda ligi. wakati mwengine hata hazitusaidii zaidi ya kutufifisha,
 
Kusema kweli hili la kuchinja linanipa tabu kama linaweza kutufanya kugombana.
Kuna mambo mengine ni kuvumiliana tu. Mi bana nikinunua Kuku wangu nampa Muislam kuchinja....
Sijui nani atapiga hodi kuja kupata msosi, kwa nini nimkwaze mwenzangu kwa jambo ambalo haliathiri Imani yangu?

Tena na familia zetu hizi za Kiafrika mtu anakuja kwako bila miadi!

Kwa hakika ukiliangalia suala la kuchinja kijuujuu utaona ni suala dogo sana na la kututia aibu. Lakini ni suala kubwa ukiingia kwa undani. Kitu ambacho Watanzania wengi ikiwa ni pamoja na Mkuu wetu wa Kaya ama tumeshindwa kukijua au tunajifanya hatutaki kukijua ni kwamba suala la kuchinja ni matokeo ya kuruhusu watu kukashfu na kukejeli imani za watu wengine.

Tusipokubali kutunga sheria ya kukomesha kundi la imani moja kukashfu na kukejeli imani za kundi jingine (yaani hilo kosa kuwa ni la jinai linaloambatana na adhabu kali), hivi vitu vinavyoonekana vidogo vidogo vitaendelea kuibuka tena kama mafuriko.

Ninaamini kama isingekuwa ni huu utamaduni tulioachia wa watu kukashfu na kukejeli dini za wengine tena hadharani, yale mazoea ya Waislamu kuchinja yasingeanza kuhojiwa na mtu ye yote. Kwa hivyo wanaouliza mbona mzozo wa kuchinja hakutokea enzi za Nyerere au Mwinyi au Mkapa, jibu ndio hilo kwamba hizi kashfa na kejeli za kidini hadharani zilikuwa bado hazijotokea.

Watu wa dini zote walikuwa wakiheshimiana na ndo hayo matokeo ya mazoea ya Waislamu kuchinja. Mabadiliko ya aina yo yote yale yawe ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, nk huhitaji kuwa managed na serikali. Kwa vile hali imebadilika basi serikali haina budi kutunga sheria mpya ambazo zitairejesha jamii katika mstari.

Kinachosikitisha ni kwamba badala ya Mhe JK kuchukua hatua za kutunga sheria ya kutokomeza tabia mbaya ya watu kukashfu na kukejeli dini za watu wengine, tunamwona anakuja kulialia na kutaka sisi tumwonee huruma kuwa yeye hana udini, yeye si mdini! Mhe JK anatuangusha.
 
Serikali imechelewa kuchukua hatua za kisheria mara ishara zilipoanza kabla ya tukio la Karagwe lililochochewa na pale yaliyompata mchungaji alipochinja kitoweo kwa ajili ya hafla yao -rais alikwepa kutaja tukio hili. Pamoja na kwamba wakristo karibu wote hawajali kuacha muislamu achinje kwa faida ya wageni wake wote pindi wamtembeleapo (kati yao ni ndugu, jirani, rafiki, nk.).

Kwa sababu damu imemwagika eti kwa sababu mkristo akachinja, basi hapa ni sheria tu itakayotatua suala hili baada ya kuwachukulia hatua za kisheria wote waliowaletea madhara wakristo kwa sababu ya kuchinja na kukumbusha kuwa hakuna anayekatazwa kuchinja ili mraddi taratibu za afya zimefuatwa.

Majibu na nia ya serikali ni kubariki tendo la walioua au kujeruhi wakristo waliochinja. Serikali inapata kigugumizi kutamka kuwa hakuna sheria inayozuia mkristo kuchinja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom