Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya Taasisi ya kidini ya UAMSHO Zanzibar kwa muda mrefu. Jumuiya hii imesajiliwa kama taasisi ya kidini, lakini sasa inaonekana majukumu yake yamebadiliki na inafanya majukumu yanayopaswa kufanywa na chama cha upinzani katika Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Jamhuri ya watu wa Zanzibar baada ya kuaanzishwa kwa "serikali ya Umoja wa kitaifa" kati ya CUF na CCM wananchi walikosa ule uhuru wa kukosoa serikali yao, maana serikali yote inafikiria jambo moja. Zanzibar tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi imekuwa katika hekaheka hiyo kwa takriban miaka 20, lakini ghafla wakakosa hiyo nafasi ya kufanya siasa za demokrasia.Dirisha lile la CUF lilokuwa linatumika kuwasilisha mawazo yao limefungwa ghafla na mungu kawapa mlango mpana unaoitwa UAMSHO. Hili ombwe la kukosekana kwa upinzani Zanzibar limezalisha UAMSHO na kuipa nguvu na limekuwa tumaini jipya kwa wazanzibari. Nasema hivi kwa sababu leo hii CUF haiwezi kusema jambo lolote linaloendelea kinyume na maoni ya serikali ya umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo, tuilaumu serikali ya Umoja wa kitaifa maana ndiyo wamezalisha kikundi cha UAMSHO na imechukua nafasi ambayo inapaswa kuchukuliwa na Upinzani zanzibar. Zanzibar inapaswa kurudi kwenye utamaduni wake wa upinzani ili taasisi za kidini zifanye kazi zao badala ya kujaza OMBWE la kutokuwepo upinzani.:embarrassed: