UDINI: Uchafu Chini ya Kapeti tunajidanganya wasafi - Zitto

Status
Not open for further replies.
Tunahitaji watu wenye mawazo yanayojenga kama Zitto,lkn lazima tukubaliane haya yote yameletwa na Mr Dhaifu pale alipotumia udini kama Mtaji wake wa Kura sasa unatutafuna wote na kinachotakiwa akielewe kuwa vita vya udini haitamweka kando kamwe na ni moja ya historia mbaya anayotuachia na hili atakumbukwa nalo milele na milele.sielewe nini kinachomshinda kukemea,mfano leo hii neno HALAL linatawala bidhaa nyingi zinazouzwa hapa nchini kuliko hata nembo ya TBS! inamaana bidhaa zisizokuwa na neno Halal ni Haramu? majibu tunayaona tumeanza na kuchinja tutaelekea kwenye Juice unga n.k
 
thatha

Unafiki ndio umetufikisha hapa tulipo. Wana siasa ndio wanabeba mzigo wote wa mambo ya udini maana wameutumia udini katika kupambana kwa maslahi yao na ya vyama vyao. Badala ya kuhimiza watu kushirikiana na kujenga nchi wanahimiza watu wa chama hiki wawachukie wa chama kile kwa vigezo vya udini...inahitajika busara kututoa hapa tulipofika...tukimpa man of mediocrity again imekula kwetu
 
Last edited by a moderator:
Tunahitaji watu wenye mawazo yanayojenga kama Zitto,lkn lazima tukubaliane haya yote yameletwa na Mr Dhaifu pale alipotumia udini kama Mtaji wake wa Kura sasa unatutafuna wote na kinachotakiwa akielewe kuwa vita vya udini haitamweka kando kamwe na ni moja ya historia mbaya anayotuachia na hili atakumbukwa nalo milele na milele.sielewe nini kinachomshinda kukemea,mfano leo hii neno HALAL linatawala bidhaa nyingi zinazouzwa hapa nchini kuliko hata nembo ya TBS! inamaana bidhaa zisizokuwa na neno Halal ni Haramu? majibu tunayaona tumeanza na kuchinja tutaelekea kwenye Juice unga n.k

Ndugu yangu, issue ya Halaal foods ipo nchi nyingi sana, especially ambazo wakazi wake wengi ni wakristu, huwa wanaweka hivyo ili kutokuwakwaza wengine, na sio tu kwa waislamu bali hata Non-vegetarians nao wana portion yao, issue ya Udini, Mh. Kikwete alitahadharisha juu ya hilo, cha ajabu mwisho wa siku ikawa ye ndo mchochezi, maana alisema maneno kama haya ya mh. Zitto rejea hotuba yako ya kukubali ushindi wa uraisi 2010 mara tu alipotangazwa pale Karimjee. issue nyingine ni suala la Ilani na Waraka wa kanisa katoliki, though Maneno yake yalikuwa mazuri, na ya kuvutia kwa kila mtanzania, Lakini nayo yalipewa tafsiri nyingine, ambayo ilizaa udini. Na hata pale mzee kingunge ngombale mwiru alipotahadharisha, watu waliamua kumnyamazisha kwa kumwita Fisadi na kuanza kumsakama, I tell u hiyo ilileta shida sana.

Kwa mimi ambaye nilishiriki kampeni katika jimbo langu especially zile za maoni za CCM, tulikuwa na wakati mgumu kuwashawishi waislam kuwa mgombea wetu ambaye alikuwa mkristu alitaka kutetea maslahi ya watu wake na si ya dini yake kama ilivyotangazwa, lakini haikusaidia. ndo maana nasema mheshimiwa zitto, kaamua kusema ukweli, kaamua kuutupa unafiki kule, hata kama kwa kufanya hivyo kutamgharimu (especially kwa wale wanaodhani kuwa ni CCM pekee au waislamu pekee walioutumia udini 2010
 
Safi sana zitto

Kama kweli Mh. ZZK hii imetoka moyoni ndani kabisa, ni meseji kali sana inayohitaji kusomwa na kufanyiwa kazi haraka ili kuliponya Taifa letu hili!!! Udini utatumaliza! tunahitaji Rais Dikteta katika kuumaliza kabisa katika ramani ya TZ. Mungu ibariki Tanzania.
 
Tukio la mauaji ya Padre limetokea juzi tu, na hakujakaliwa kikao chochote cha Bunge tangu mauaji, sasa hiyo 'Mheshimiwa Spika' ni ya lini?

usiwe unasoma ka unachongo hebu rudi kasome tena basi.
 
udini unatumiwa na chama fulani kuangamiza chama fulani, ushahidi upo tusimungunye maneno, ndugu Zitto hilo analijua anazunguka tu.

wanataka kulinda madaraka kuwa njia yoyote ile , kwani mkichinjana wao wana hasara gani wamewekeza mipesa ya kutosha huko uswiss mpaka wafe, wakiona vipi watasepa si tayari wana uhakika.

wana dola wanashindwa nini kudhibiti upuuzi unaoendelea

ukweli ni kwamba wameshindwa kuongoza nchi hata kama ndugu Zito hataki kukiri udhaifu wao

si ni hao wanawalipa vijana fulani, hata jana walisika kwenye radio maarufu, wakichochea udini, eti chama fulani ni cha kidini??

kuna magazeti, radio huko morogoro na baadhi ya viongozi wa dini wanachochea maasi wanajulikana nani ana jukumu la kudhibiti??

nini kifanyike?? nashauri
ili suala hili lisiendelee kutuathiri,

1.kwanza serikali itekeleze wajibu wake wa kuchukua hatua kwa wachochezi

2.upelekwe mswada bungeni ili yaanzishwe mabaraza ya maridhiano kuanzia serikali za mitaa, kata wilaya mkoa hadi taifa yawe na wajumbe wa dini zote na viongozi wa kiserikali, itawafanya viongozi wa dini kuwa karibu zaidi na kuweza kubaini tatizo mapema kabla maafa kama ya Geita hayajatokea

2.kuanzia sasa kuwepo kampeni mahususi ya kupinga udini matangazo,mihadhara,mikutano semina matamasha nakadhalika,kampeni hii iongozwe na baraza la vijana la taifa kw kuwa ndio waathirika wakuu wa udini, isiwe na itikadi za vyama. iwe ni kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwa weka pamoja vijana wakatae udini. huu uwe mkakati endelevu kuelekea 2015 il tuvuke salama

3.tukubali tumeishaharibu mfumo kwa tamaa za madaraka.tukishindwa kuweka mikakati kama nchi tukabaki kulalamika tu hatufiki 2015, na kama wenye dola hawatachukua hatua zozote ikiwa ni pamoja na nilizozitaja hapo juu, tutajua ya kwamba wapo nyuma ya kadhia hii,na siku ya siku watalipia upuuzi huu unaoendelea, hata wakikimbia tutawafuata walipo popote duniani tuwawajibisha
 
Ndugu yangu usimshangae sana ndivyo sie watanzania tulivyo, kuna misemo miwli inayosema hivi 1. Ukilipenda boga upende na ua lake, 2. usimtupe jongoo na mti wake. Sasa inategemea ye aliamua kuutupa na mti wake, hivyo hasikii wala kuona, achilia mbali kuelewa. maana haihitaji degree kuelewa alichokisema mh. Zitto
 
u have think brother, viongozi wa dini acheni unafiki, wana siasa msiongozwe na matumbo vile vile acheni unafiki kusema huyu ni wa dini ile chama hiki na cha kidini, bila ushahidi madhara yake ndio hayo, or chama cha wachaga, maana mkimaliza huko mtasema tuue na wachaga sasa
 
Kwakuwa serikali haina dini itekeleze wajibu wake. Iwakamate wachochezi wote kwakuwa wanajulikana.
 
Dah! Maneno mazito sana.

Nadhani wale wanombeza Zitto sasa naona watakubali kuwa Zitto ni kichwa kikali. Udini upo na kuna watu wapo na wanaishi kwa nguvu ya udini tu,ingekuwa kuna haki na bila kuzingatia udini basi mambo mengine yangeenda sawa. Kuna watu wanawafadhili toka ulaya huko wapo hapa kwaajili ya kutugawa.

Vyombo vya habari ndio balaa na ndio vitakuja kusababisha maafa maana kuna magazeti kilasiku huandika habari za uchochezi tu,pia kuna radio naz kazi yake ni kuponda tu. Mauaji ya kimbari ya Rwanda hayakuanza ghafla tu bali zilikuwepo makala, vipindi vya radio na hotuba makanisani za kuhamasisha mauaji. Haya sasa na kwetu ndio yanayotokea na yanaendelea.

Tumuombe Mungu amani yetu izidi kudumu.

Mimi ni mmoja kati ya watu ambao wanamtilia mashaka sana ZITO!... Ndani ya chama chake yeye ndiye kiongozi wa makundi hatarishi. Yanayohubiri ukanda, ukabila na udini!... Na wafuasi wake hata baada ya kuhamia CCM wanahubiri UDINI, UKABILA NA UKANDA. ...Shonza na Mtela wamefanya kazi hii kwa muda mrefu na mwanasiasa huru - Habib Mchange kueneza sumu hii!.

Swali langu kwa Zito amesaidiaje kumnyamazisha ustaadhi - Hassan ambaye alitoa CD agosti mwaka jana kuagiza wakristo wauawe!.. Au atasema hajaziona?!.. CD hizi zimepelekea wapadri wawili Zanzibar wapigwe risasi!...

IGP huyu na serikali hii haitaaminiwa na wakristo waliowengi kama USTAADHI ILUNGA hatafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
 
u have think brother, viongozi wa dini acheni unafiki, wana siasa msiongozwe na matumbo vile vile acheni unafiki kusema huyu ni wa dini ile chama hiki na cha kidini, bila ushahidi madhara yake ndio hayo, or chama cha wachaga, maana mkimaliza huko mtasema tuue na wachaga sasa

Mkuu hizi ndizo hotuba za ccm. UKABILA, UDINI na ukanda ni propaganda za kuulia upinzani. Mimi naona hizi zitaua TAIFA si vyama vya siasa.
 
udini unatumiwa na chama fulani kuangamiza chama fulani, ushahidi upo tusimungunye maneno, ndugu Zitto hilo analijua anazunguka tu.

wanataka kulinda madaraka kuwa njia yoyote ile , kwani mkichinjana wao wana hasara gani wamewekeza mipesa ya kutosha huko uswiss mpaka wafe, wakiona vipi watasepa si tayari wana uhakika.

wana dola wanashindwa nini kudhibiti upuuzi unaoendelea

ukweli ni kwamba wameshindwa kuongoza nchi hata kama ndugu Zito hataki kukiri udhaifu wao

si ni hao wanawalipa vijana fulani, hata jana walisika kwenye radio maarufu, wakichochea udini, eti chama fulani ni cha kidini??

kuna magazeti, radio huko morogoro na baadhi ya viongozi wa dini wanachochea maasi wanajulikana nani ana jukumu la kudhibiti??

nini kifanyike?? nashauri
ili suala hili lisiendelee kutuathiri,

1.kwanza serikali itekeleze wajibu wake wa kuchukua hatua kwa wachochezi

2.upelekwe mswada bungeni ili yaanzishwe mabaraza ya maridhiano kuanzia serikali za mitaa, kata wilaya mkoa hadi taifa yawe na wajumbe wa dini zote na viongozi wa kiserikali, itawafanya viongozi wa dini kuwa karibu zaidi na kuweza kubaini tatizo mapema kabla maafa kama ya Geita hayajatokea

2.kuanzia sasa kuwepo kampeni mahususi ya kupinga udini matangazo,mihadhara,mikutano semina matamasha nakadhalika,kampeni hii iongozwe na baraza la vijana la taifa kw kuwa ndio waathirika wakuu wa udini, isiwe na itikadi za vyama. iwe ni kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwa weka pamoja vijana wakatae udini. huu uwe mkakati endelevu kuelekea 2015 il tuvuke salama

3.tukubali tumeishaharibu mfumo kwa tamaa za madaraka.tukishindwa kuweka mikakati kama nchi tukabaki kulalamika tu hatufiki 2015, na kama wenye dola hawatachukua hatua zozote ikiwa ni pamoja na nilizozitaja hapo juu, tutajua ya kwamba wapo nyuma ya kadhia hii,na siku ya siku watalipia upuuzi huu unaoendelea, hata wakikimbia tutawafuata walipo popote duniani tuwawajibisha

HILI SUALA SIYO SIRI!.. CCM ni chama kinachohubiri UDINI!.. Walianza na CUF mwaka 2000 na kuhamia CHADEMA 2005 na 2010. Ilifika mahali mzee Makamba anakemea udini makanisani, lakini misikitini anahamasisha.
 
Mh. Zitto kaanika maneno yenye "busara" kuhusu suala hili lakini nachelea kusema hayatuelekezi kwenye kiini cha kuibuka kwa kasi kwa tatizo la udini katika awamu hii ya serikali. Hoja aliyoitoa ni rahisi kwa mtu yeyote mwenye upeo mzuri kuielewa lakini ni ya kawaida na ya ujumla sana. Tishio la udini liko kila mahali duniani. Hata wakati wa Nyerere lilikuwepo na alilizungumzia mara kwa mara. Lakini aliweka mikakati ya muda mfupi na mrefu kulidhibiti "lisivuke mstari". Serikali zote makini duniani zinafanya hivyo. Huwezi tu kuwatafadhalisha wananchi wajichunguze na kuondoa tatizo. Blanket resolutions do not help. The average man is self-centered and irrational when it comes to personal interests. Ndio maana kuna sheria, taratibu na vyombo vya udhibiti.

Raisi na serikali yake wawe wakweli kuhusu tatizo hili kufikia hatua hii ya militancy. Kwa mfano, ni nani aliyeanzisha na kueneza hoja ya nchi kuendeshwa na "mfumo kristo"? Kwamba hata wakijaa waislamu kwenye uongozi wa juu bado hawana uwezo wa kuudhibiti mfumo huo unaowadhulumu waislamu haki zao; kwamba Kardinali Pengo akiongea serikali nzima inagwaya na kubadili msimamo wake! Kama serikali haihusiki na sumu hiyo, basi ijitokeze wazi na kukanusha kwamba kuna mfumo huo wa kidini uliopora madaraka yake ndio maana inashindwa kusimamia "haki za waislamu" hata kukubali Zanzibar iwe "huru"!

Akina Zitto wataongea "maneno mazuri" lakini bila kuwatwisha wajibu wanaohusika wachukue hatua kwa mujibu wa madaraka tuliyowapa na kutarajia sie wananchi "tujirekebishe", basi tukae kusubiri miujiza. Watu waanzishe na kupalilia janga halafu yakiharibika tunaanza kuleta hadithi za Oprah: eti tujichunguze na kujirekebisha! Mwambie mwizi atumie busara (awe muungwana) asiibe - eti sio kitu kizuri! Ibelieve they love that kind of naïvette.The real world doesn't work that way! We just need able leadership in this case.
 
Haya anayosema ZITTO no ya kweli kabisa 2010, kulikuwa na udini wa hali ya juu, bahati mbaya sana hata hao tunaowaamini ambao ni viongozi wa dini walikuja na kukanusha harakaharaka, mgombea tuliyekuwa tunamuunga mkono 2010, alikuwa ni mkristo, ila tulimuunga mkono si kwasababu ya dini yake ila kwasababu ya weledi wake, bahati mbaya sana wachungaji wakaanza kumpigia kampeni kanisani, soma Mwananchi 2010, around April, then waislamu nao wakaamua kumpigia kampeni yule mwislamu ambaye japo alikuwa mbunge alikuwa hajafanya lolote, Matokeo yake Mgombea tuliyemuunga mkono alidondoka kweli. Hivyo tunahitaji kuujenga ukuta huu ulioboomoka.

Nadhani hotuba ni ya 2008, sasa anzia Uchaguzi wa 2005, maana huko nakumbuka tulikuwa na chaguo la Mungu na la Shetani, unakumbuka?
 
udini unatumiwa na chama fulani kuangamiza chama fulani, ushahidi upo tusimungunye maneno, ndugu Zitto hilo analijua anazunguka tu.

wanataka kulinda madaraka kuwa njia yoyote ile , kwani mkichinjana wao wana hasara gani wamewekeza mipesa ya kutosha huko uswiss mpaka wafe, wakiona vipi watasepa si tayari wana uhakika.

wana dola wanashindwa nini kudhibiti upuuzi unaoendelea

ukweli ni kwamba wameshindwa kuongoza nchi hata kama ndugu Zito hataki kukiri udhaifu wao

si ni hao wanawalipa vijana fulani, hata jana walisika kwenye radio maarufu, wakichochea udini, eti chama fulani ni cha kidini??

kuna magazeti, radio huko morogoro na baadhi ya viongozi wa dini wanachochea maasi wanajulikana nani ana jukumu la kudhibiti??

nini kifanyike?? nashauri
ili suala hili lisiendelee kutuathiri,

1.kwanza serikali itekeleze wajibu wake wa kuchukua hatua kwa wachochezi

2.upelekwe mswada bungeni ili yaanzishwe mabaraza ya maridhiano kuanzia serikali za mitaa, kata wilaya mkoa hadi taifa yawe na wajumbe wa dini zote na viongozi wa kiserikali, itawafanya viongozi wa dini kuwa karibu zaidi na kuweza kubaini tatizo mapema kabla maafa kama ya Geita hayajatokea

2.kuanzia sasa kuwepo kampeni mahususi ya kupinga udini matangazo,mihadhara,mikutano semina matamasha nakadhalika,kampeni hii iongozwe na baraza la vijana la taifa kw kuwa ndio waathirika wakuu wa udini, isiwe na itikadi za vyama. iwe ni kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwa weka pamoja vijana wakatae udini. huu uwe mkakati endelevu kuelekea 2015 il tuvuke salama

3.tukubali tumeishaharibu mfumo kwa tamaa za madaraka.tukishindwa kuweka mikakati kama nchi tukabaki kulalamika tu hatufiki 2015, na kama wenye dola hawatachukua hatua zozote ikiwa ni pamoja na nilizozitaja hapo juu, tutajua ya kwamba wapo nyuma ya kadhia hii,na siku ya siku watalipia upuuzi huu unaoendelea, hata wakikimbia tutawafuata walipo popote duniani tuwawajibisha

HILI SUALA SIYO SIRI!.. CCM ni chama kinachohubiri UDINI!.. Walianza na CUF mwaka 2000 na kuhamia CHADEMA 2005 na 2010. Ilifika mahali mzee Makamba anakemea udini makanisani, lakini misikitini anahamasisha.
 
Taifa linalia, wenye dhamana ya kuongoza wapo kimya ama kuongea kwa unafiki.
 
Zitto kwa asilimia kubwa nakubaliana na maoni yako lakini ni lazima utambue kwamba matatizo ya udini Tanzania yameanzishwa na baadhi ya wanasiasa wa CCM kwa malengo ya kubakia madarakani. Tatizo sasa kuna baadhi yetu sasa kwa ufadhili wa taasisi za dini na taifa moja la kigeni wamepokea kijiti hiki cha moto,ukichanganya na udhaifu/ombwe kubwa la uongozi tunaelekea ktk machafuko makubwa ktk nchi yetu. Kuna taasisi za kidini na watu binafsi wanapewa pesa toka nje kuharibu amani ya nchi yetu. Ndugu zangu Waislamu nawaomba mwuwamlike watu wanaotumia dini yenu kuvuruga amani ya nchi yetu kwa ufadhili wa makundi toka nje.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom