'Udikteta': Lowassa na sizitaki mbichi hizi

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kati ya waliokuwa makada waandamizi wa CCM waliokataa waziwazi,kwa maneno,ujio wa katiba mpya alikuwa ni Edward Ngoyai Lowassa. Alipofuatwa na waliokuwa Wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba,Lowassa alitaka katiba mpya isubiri uchaguzi wa 2015.

Hoja na kivutio cha Lowassa kwenye katiba ya sasa ni Urais wenye nguvu. Aliiona katiba mpya kama chombo cha kuminya madaraka na mamlaka ya Rais. Alitamani kuwa Rais mwenye nguvu kubwa kikatiba. Kwa katiba ya sasa. Hakuitaka katiba mpya. Katiba mpya ikakwama kweli.

Lowassa akaukosa Urais wenye nguvu. Akaupata Mhe. Dr. J. P. Magufuli. Leo hii,Lowassa ni kati ya wanaoupinga Urais wenye nguvu. Wanauita udikteta. Ni mambo ya sizitaki mbichi hizi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Nakubaliana na wewe mzee, Lowassa ni dikteta mwingine
 
Kapatikana huyo, hana ujanja, aendelee kusota rumande
 
Hoja yako ni ubinafsi wa Lowasa au ubabe wa Magufuli kwa kuvunja katiba mbovu?
 
Lowasa naye mnafki tu,sijawahi mkubali hata kidogo,LAKINI UKUTA UPO PALE PALE
 
Kati ya waliokuwa makada waandamizi wa CCM waliokataa waziwazi,kwa maneno,ujio wa katiba mpya alikuwa ni Edward Ngoyai Lowassa. Alipofuatwa na waliokuwa Wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba,Lowassa alitaka katiba mpya isubiri uchaguzi wa 2015.

Hoja na kivutio cha Lowassa kwenye katiba ya sasa ni Urais wenye nguvu. Aliiona katiba mpya kama chombo cha kuminya madaraka na mamlaka ya Rais. Alitamani kuwa Rais mwenye nguvu kubwa kikatiba. Kwa katiba ya sasa. Hakuitaka katiba mpya. Katiba mpya ikakwama kweli.

Lowassa akaukosa Urais wenye nguvu. Akaupata Mhe. Dr. J. P. Magufuli. Leo hii,Lowassa ni kati ya wanaoupinga Urais wenye nguvu. Wanauita udikteta. Ni mambo ya sizitaki mbichi hizi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Tegemea mashambulizi makali kutoka kwa wafikiriao kwa kutumia moyo.
 
Uzi huu unakwepwa na ulipo tupo wengi!!!!
 
Kati ya waliokuwa makada waandamizi wa CCM waliokataa waziwazi,kwa maneno,ujio wa katiba mpya alikuwa ni Edward Ngoyai Lowassa. Alipofuatwa na waliokuwa Wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba,Lowassa alitaka katiba mpya isubiri uchaguzi wa 2015.

Hoja na kivutio cha Lowassa kwenye katiba ya sasa ni Urais wenye nguvu. Aliiona katiba mpya kama chombo cha kuminya madaraka na mamlaka ya Rais. Alitamani kuwa Rais mwenye nguvu kubwa kikatiba. Kwa katiba ya sasa. Hakuitaka katiba mpya. Katiba mpya ikakwama kweli.

Lowassa akaukosa Urais wenye nguvu. Akaupata Mhe. Dr. J. P. Magufuli. Leo hii,Lowassa ni kati ya wanaoupinga Urais wenye nguvu. Wanauita udikteta. Ni mambo ya sizitaki mbichi hizi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mkuu, leo umetoka kivingine kabisaa.
 
Aliteleza, ila UKUTA upo kwa kila aitakiae mema nchi hii
 
jambo moja unalotakiwa kujua unapokuwa ndani ya ccm lazina uongee kwa maslahi ta chama tofauti na hapo utaambiwa hayo nimawazo yake binafsi au unaweza hojiwa maswali magumu hadi kifo kama yaliyomkuta kolimba
Kati ya waliokuwa makada waandamizi wa CCM waliokataa waziwazi,kwa maneno,ujio wa katiba mpya alikuwa ni Edward Ngoyai Lowassa. Alipofuatwa na waliokuwa Wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba,Lowassa alitaka katiba mpya isubiri uchaguzi wa 2015.

Hoja na kivutio cha Lowassa kwenye katiba ya sasa ni Urais wenye nguvu. Aliiona katiba mpya kama chombo cha kuminya madaraka na mamlaka ya Rais. Alitamani kuwa Rais mwenye nguvu kubwa kikatiba. Kwa katiba ya sasa. Hakuitaka katiba mpya. Katiba mpya ikakwama kweli.

Lowassa akaukosa Urais wenye nguvu. Akaupata Mhe. Dr. J. P. Magufuli. Leo hii,Lowassa ni kati ya wanaoupinga Urais wenye nguvu. Wanauita udikteta. Ni mambo ya sizitaki mbichi hizi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Kumbe figisu figisu zote kwenye mjadala wa katiba mpya unatokana na CCM kung'ang'ani "Urais wenye nguvu!" Asante sana mzee Tupatupa kwa kutudokeza siri nzito ya huko Umagambani.
 
Back
Top Bottom