Hadithi za kama yale yanayotokea Libya ni maarufu sana masikioni mwetu. Rais Magufuli amekaririwa mara kadhaa akionya kwa kutolea mfano wa matukio ya Libya kwamba ilikuwa ni nchi ya asali.
Wengine pia huonya kwa kutumia Iraq.
Kuna haja ya kujikumbusha nchi hizi pamoja na Misri, zimekuwa kwenye mifumo ya kidikteta ya muda mrefu. Mahakama na Bunge vilikuwa ni rubber stamp institutions. Zinaamua yale yanayowapendeza wakubwa.
Usalama na amani vilitawaliwa na hofu. Minong'ono ya chini chini ndio iliyokuwa ikiendelea. Mabwana wakubwa kina Hosni Mubarak, Gaddaff na Sadam walikuwa wakikohoa tu kila mtu amefika.
Kule Iraq, wakurdi na mashia walipoteza maisha, Libya wapinzania walifungwa na kukimbilia uhamishoni, Misri jeshi likawa linamiliki zaidi ya 50% ya uchumi. Kwa mtazamo wa nje haya yalikuwa ni mafanikio maana kulikuwa hakuna uhuru wa vyombo vya habari.
Uhalisia ni kwamba utawala wa kidikteta ni kupoteza muda. Kama madikteta watajiona wanapiga hatua nne kwenda mbele, basi watarudi nyuma hatua sita. Hii ni kwa sababu wao hufanya maamuzi yao wenyewe na kusahau nchi ni taasisi.
Watu wanasahau nchi kama Taifa inahitaji dira na si maono ya mtu mmoja mmoja. Dikteta akifika ukomo, ambao ni lazima afike kwa kuondoka madarakani, equilibrium lazima ipatikane. Lakini kwa sababu dikteta haundi taasisi imara zaidi ya jeshi, mkwamo na mivurugano hujitokeza na nchi hurudi nyuma.
Yanayotokea Libya, Egypt,, Iraq na kwingineko ni harakati za kutafuta equilibrium maana wale madikteta waliwapotezea muda. Ni lazima tutambue taasisi imara tu ndio zitakazotuvusha na si maono au mawazo ya mtu mmoja.