Ni Aibu Kubwa kwa EAC.

Ni Aibu Kubwa kwa EAC.

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,943
Hizi taasisi za mataifa ya Afrika sijui kama zina faida yoyote nyingine zaidi ya kutoa ajira kwa baadhi ya watu!!

Leo ni siku ya 3 tangu maandamano makubwa yaanze nchini Kenya, yanayotishia uwezekano wa kutokea maafa makubwa ya uhai wa watu na mali. Mpaka sasa vifo 13 vimethibitika na wakuu wa mahospitali, lakini wanasema kuna uwezekano mkubwa waliouawa ni zaidi ya hao 13.

Maandamano yalikuwa ya amani, mpaka polisi walipoanza kutumia risasi za moto na kuua waandamanaji.

Kenya ni mwanachama wa EAC, ni mwanachama wa AU, mambo haya mabaya na ya hatari yanayotokea kwa nchi mwanachama wa EAC na AU, lazima yatakuwa na athari kwa jumuia hizi kama taasisi na yana athari kwa mataifa wanachama, kama nchi jirani. Lakini jambo linaloshangaza sana, mpaka sasa, si jumuia ya EAC, AU wala nchi mwanachama mmoja mmoja ambayo imetoa kauli yoyote au kufanya jitihada za kuhakikisha ndugu zetu hawa hawaishii kwenye ubaya wa kutisha. Labda nchi wanachama zote zinaongozwa na viongozi Chura Viziwi!!

Mataifa ya mbali, kama US wamekwishatoa kauli ya kuikemea Serikali ya Kenya kwa mauaji ya waandamanaji.

Pongezi nyingi kwa viongozi wa dini wa Kenya waliomtaka Ruto kuwarudisha wanajeshi makambini, na suala la kuyalinda maandamano libakie mikononi mwa Polis, maana ndiyo kazi yao, kwa mujibu wa katiba ya Kenya.

Hii EAC na Au inaonekana haina msaada kwa wananchi wa Afrika. Watu wanaweza kuuawa kwa mamia kwenye nchi mwanachama na taasisi hizi zikawa kimya tu. Kama EAC na AU haziwezi kuwahakikishia usalama wananchi wa mataifa wanachama, kimsingi taasisi hizi zinakuwa hazina maana yoyote, maana kwa mwanadamu, jambo la kwanza muhimu kuliko yote, ni uhai wake.
 
Sawa kuwa na subira utapata wachangiaji wanakuja..
 
Hizi jumuia zinazojuisha watu kama kina Samia na Museveni ni ma-kanyaboya tu. Hata jumuia ya panya ina coordition ya maana kuliko hawa majuha.
 
Third world country 🪜🙂😑😐
 
Hao ni Waarabu wa Pemba. Labda utawasikia wakipeana salamu za pongezi au pole ya misiba na maafa mengine. Ila siyo kwenye kukosoana.
 
EAC shughuli zimesimama hawana pesa, wanahitaji bilioni 40 kurudi kwenye ramani.
 
Unategemea kiongozi wa nchi yetu kutoa kauli gani.....mfano ungekua kama waziri wetu wa fedha ungesema nini ukinukuu kauli ile ya wanaopinga tozo wahamie Burundi!!!
 
Hizi taasisi za mataifa ya Afrika sijui kama zina faida yoyote nyingine zaidi ya kutoa ajira kwa baadhi ya watu!!

Leo ni siku ya 3 tangu maandamano makubwa yaanze nchini Kenya, yanayotishia uwezekano wa kutokea maafa makubwa ya uhai wa watu na mali. Mpaka sasa vifo 13 vimethibitika na wakuu wa mahospitali, lakini wanasema kuna uwezekano mkubwa waliouawa ni zaidi ya hao 13.

Maandamano yalikuwa ya amani, mpaka polisi walipoanza kutumia risasi za moto na kuua waandamanaji.

Kenya ni mwanachama wa EAC, ni mwanachama wa AU, mambo haya mabaya na ya hatari yanayotokea kwa nchi mwanachama wa EAC na AU, lazima yatakuwa na athari kwa jumuia hizi kama taasisi na yana athari kwa mataifa wanachama, kama nchi jirani. Lakini jambo linaloshangaza sana, mpaka sasa, si jumuia ya EAC, AU wala nchi mwanachama mmoja mmoja ambayo imetoa kauli yoyote au kufanya jitihada za kuhakikisha ndugu zetu hawa hawaishii kwenye ubaya wa kutisha. Labda nchi wanachama zote zinaongozwa na viongozi Chura Viziwi!!

Mataifa ya mbali, kama US wamekwishatoa kauli ya kuikemea Serikali ya Kenya kwa mauaji ya waandamanaji.

Pongezi nyingi kwa viongozi wa dini wa Kenya waliomtaka Ruto kuwarudisha wanajeshi makambini, na suala la kuyalinda maandamano libakie mikononi mwa Polis, maana ndiyo kazi yao, kwa mujibu wa katiba ya Kenya.

Hii EAC na Au inaonekana haina msaada kwa wananchi wa Afrika. Watu wanaweza kuuawa kwa mamia kwenye nchi mwanachama na taasisi hizi zikawa kimya tu. Kama EAC na AU haziwezi kuwahakikishia usalama wananchi wa mataifa wanachama, kimsingi taasisi hizi zinakuwa hazina maana yoyote, maana kwa mwanadamu, jambo la kwanza muhimu kuliko yote, ni uhai wake.
Yakwetu yanatushinda kuyatolea kauli kwa wakati sembuse ya jirani Kwa hili tunajifunza kwamba viongozi wetu hawana uwezo wa kukabiliana na majanga, 'Murphy's law'
 
EAC siyo Jumuiya ya kisiasa,ipo zaidi kijogroafia,kiuchumi na kibiashara.
Kwani nchi wanachama karibu zote zina matatizo kwa lugha ya ubwabwa yamebatizwa changamoto.
Hivi unategemea South Sudan,Congo ya DRC,wakupe jibu gani?
 
Back
Top Bottom