Ni yeye! Ni nani?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,953
2,840
LITANIA YA USHINDI

Ee Mungu Baba kwa namna ya pekee utuvushie mtu huyu kwa salama ili naye atuvushe kutokea sasa na hata baadae ili akiingia kuwa kiongozi wa nchi, basi aiweke misingi ya kiutawala kwa namna ambayo hata akija kiongozi mwingine isiwe tabu kwake kuongoza. Baba ujue tunahitaji taasisi imara na si watu imara. Watu imara wawe ni kwa ajili ya kuongoza na kusimamia taasisi imara na sio mawazo binafsi.

  • Mbeba maono Tuvushe
  • Mbobezi wa sheria Tuvushe
  • Mkwepa mauti Tuvushe
  • Kiboko ya wajuaji Tuvushe
  • Kipenzi cha wengi Tuvushe
  • Jabali la hoja Tuvushe
  • Ngome ya ushindi Tuvushe
  • Ngao ya haki Tuvushe
  • Mussa ajaye Tuvushe
  • Kiongozi jasiri Tuvushe
  • Mfuasi wa haki Tuvushe
  • Kimbilio la wanyonge Tuvushe
  • Kiongozi makini Tuvushe
  • Chungu cha maarifa Tuvushe
  • Msaliti wa hujuma Tuvushe
  • Mfano wa mchungaji Tuvushe
  • Haiba ya uongozi Tuvushe
  • Kitanzi cha dhuluma Tuvushe
  • Shubiri ya wapenda madaraka Tuvushe
  • Mwanazuoni Tuvushe
  • Kiama cha mahasidi Tuvushe
  • Mkweli na muwazi Tuvushe
  • Heshima ya Taifa Tuvushe
  • Tunu ya thamani Tuvushe
  • Amiri Jeshi ajaye Tuvushe
Ni Yeye hakika. Ni kama wakati uliosubiriwa sana, na ambao unatimia. Tangu mauti hadi uzima, ni nani wa kuizuia mvua isinye juu ya nchi? Ni nani wa kuyazuia maji katika mkondo wake? Hakika haki huinua Taifa. Na wakati uliokubalika ni sasa



NA IWE HIVYO
 
Back
Top Bottom