UDHAMINI SIMBA SC:Dewji asaka maoni ya wadau | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDHAMINI SIMBA SC:Dewji asaka maoni ya wadau

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Jan 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MBUNGE wa Singida Mjini Mohammed Dewji ameanza kusaka maoni kupitia mtandao wa facebook ili kujiridhisha kabla ya kumwaga wino wa kuidhamini tena Simba.

  Dewji maarufu 'Mo' ambaye wiki moja iliyopita alielezwa na gazeti hili kuwa amekubali kurejea Simba kwa miaka miwili ameweka nia yake ya kuidhamini tena klabu hiyo kwa miaka miwili kwa mkataba maalumu.

  Lakini, ameeleza kuwa iwapo klabu hiyo itafanya vizuri kwenye michuano yake ya klabu bingwa na Ligi Kuu Tanzania Bara, basi ataongeza mkataba huo.

  Awali, katika mtandao wa facebook, Mo alisema, "Nafikiria kuidhamini tena Simba, nahuzunishwa sana kuona klabu hii haifanyi vizuri kwenye mashindano, nakumbuka mara ya mwisho nilipokuwa mdhamini wake nilihakikisha kuwa naifunga Zamalek ya Misri nam Simba ilifanikiwa kuwa miongoni mwa timu 10 bora Afrika,"alisema Mo.

  Aliwaomba mashabiki na watu wengi kujitokeza na kumshauri juu ya dhamira yake hiyo ya kutaka kuidhamini tena Simba.

  Akitoa maoni yake mdau wa michezo, Norbert Brown alisema, "Tanzania inahitaji watu kama wewe, Simba inakuhitaji, tunataka kuitoa TP Mazembe kwenye mashindano na pia kuwa tena bora.

  Naye Jabir Mfinanga alisema, "Ndio Mo pamoja na Rage kuna tatizo, tunahitaji kuifunga Mazembe."

  Akizungumzia suala hilo, mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema, "Hili suala lipo kwenye mchakato bado halijakamilika, sawa sawa tungependa Mo arudi na tutamkaribisha kwa mikono miwili na kiukweli tunamuhusudu sana."

  Mo, aliwahi kuiambia Mwananchi kuwa ana mpango wa kuidhamini tena klabu hiyo ambayo aliitosa miaka michache iliyopita kutokana na mwenendo mbovu wa timu ikiwa ni pamoja na uongozi na kuamua kuinunua Mbagala Market iliyopanda daraja na kuibadili jina na kuitwa Africa Lyon.

  Hata hivyo, Mo aliiacha Africa Lyon msimu huu baada ya kudai kuwa alikuwa amepata hasara kubwa tofauti na alivyotarajia na kuamua kuiuza kwa mmiliki wa kampuni ya mafuta ya RBP Oil, Rahma Al Kharoos, ambaye pia ni mlezi wa timu ya taifa ya soka ya wanawake,Twiga Stars.
   
 2. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Udhamini ni biashara, na huyu jamaa nadhani anao washauri wake ktk mambo ya biashara, kama hana hilo ni suala jingine, sasa badala ya kutafuta maoni from anybody, akae na washauri wake wafanye hesabu zao waone watafaidika vipi na udhamini na Club itafaidika vipi ndipo waende mezani kuzungumza mkataba, otherwise labda kama kuna Dili ya nguvu kwenye hizi mechi 2, v/s Wacomoro na Mazembe
   
 3. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  kwanza alipe pesa ya chapati wanazodaiwa Simba na yule bimkubwa, na kisha mengine yafuate...

  Nimepita tu watani
   
Loading...