Udhalilishaji kada ya elimu utaisha lini?

Udhalilishaji kada ya elimu utaisha lini?

El'son

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2012
Posts
380
Reaction score
324
Binafsi naunga mkono swala la uhakiki wa watumishi wa umma linalofanywa na serikali kwa sasa. Ila imefika mahala njia zinazotumiwa na baadhi ya watendaji kuvunja miiko ya utumishi wa umma na kulifanya swala la uhakiki kuwa udhalilishaji.

Nimekutana na video hii sijui imetokea wapi lakini kwa mtadhamo wangu hawa walichokifanya ni kinyume na utaratibu, hvyo kulifanya jambo hili la uhakiki kuwa udhalilishaji kwa walimu wa shule husika.

Rai yangu ni kuwa ipo haja ya kufanya uhakiki, lakini ni vyema uhakiki huo ukafanyika kwa namna ambayo hautawaletea dhihaka wale wanaohakikiwa lah sivyo watahisi wananyanyaswa na kudhalilishwa. Naomba niwape pole waliofikwa na maswahibu hayo ila pia niwasihi kuwa wanapoona kuna hali ya udhalilishaji wasisite kuhoji. Pia wahusika ikiwemo chama cha walimu moja ya kazi zao ni kulinda walimu popote walipo hvyoo wanajukumu la kukemea udhalikishaji wote unaofanya dhidi ya walimu. Mwisho ni kwa wale wanaohakiki watumish hasa kwa walimu waliowengi nawasihi watumie njia rafiki zitakadho linda heshima ya mwalimu.

Asanthe nawasilisha
 
Hivi ni.mimi tu sijaiona hiyo video ama? Mkuu ungetoa na maelezo kidogo juu kilichotokea maana wengine visimu vyetu wakati mwingine ni changa.
 
Hii sasa too much... Kwa nn walimu jamaniiiiiiiiiiiiijii
 
Hao wahakiki nao ni mbumbumbu waamekosa ubunifu. Huko tunapoelekea askari tutawahakiki mbele ya mahabusu wao, madaktari na manesi mbele ya wagonjwa, mahakimu mbele ya wafungwa na wanasiasa nao wahakikiwa mbele ya wapiga kura wao.
 
Kabisa
 
Duh! Walimu wamekuwa kama nao ni wanafunzi? Kwa nini wasifanyie hilo zoezi ofisini?
 
Biunafsi naunga mkono swala la uhakiki wa watumishi wa umma linalofanywa na serikali kwa sasa. Ila imefika mahala njia zinazotumiwa na baadhi ya watendaji kuvunja miiko ya utumishi wa umma na kulifanya swala la uhakiki kuwa udhalilishaji.

Nimekutana na video hii sijui imetokea wapi lakini kwa mtadhamo wangu hawa walichokifanya ni kinyume na utaratibu, hvyo kulifanya jambo hili la uhakiki kuwa udhalilishaji kwa walimu wa shule husika.

Rai yangu ni kuwa ipo haja ya kufanya uhakiki, lakini ni vyema uhakiki huo ukafanyika kwa namna ambayo hautawaletea dhihaka wale wanaohakikiwa lah sivyo watahisi wananyanyaswa na kudhalilishwa. Naomba niwape pole waliofikwa na maswahibu hayo ila pia niwasihi kuwa wanapoona kuna hali ya udhalilishaji wasisite kuhoji. Pia wahusika ikiwemo chama cha walimu moja ya kazi zao ni kulinda walimu popote walipo hvyoo wanajukumu la kukemea udhalikishaji wote unaofanya dhidi ya walimu. Mwisho ni kwa wale wanaohakiki watumish hasa kwa walimu waliowengi nawasihi watumie njia rafiki zitakadho linda heshima ya mwalimu.

Asanthe nawasilisha

Mkuu unatumia DHA badala ya ZA
 
Pumbavu....
"Eti wanafunzi mnamjua huyu"
Ndiooooooooooox2
Though fani yenu mnaonewa sana ila infacts nyie ndo mlitengeneza hadi hawa viongozi
BIG UP WAALIMU WOTE; mama wa taaluma zote.
 
Pengine hilo ni tatizo na inaonekana kama kudharirishwa! Lakini kuna sehemu inashangaza pia. Mwalimu ni mgonjwa kwa zaidi ya miezi sita na hajaonekana popote. Jibu sahihi hakuna na mahali alipo hapajulikani. Mwl Mkuu na wasaidizi wake hawana jibu. Wanafunzi wanaitikia yupoooooo (kwa sababu walimuona miezi sita iliyopita?). Kuna walakini kila sehemu hapa na hata sijui nimlaumu nani.
 
Back
Top Bottom