Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,703
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni
Maswali yangu Kwa Kamati ya Nape:
1. Waziri wa Habari ametumia kifungu cha sheria ipi (ITAJE SHERIA na KIFUNGU) ndani ya Tanzania kuunda kamati ile ya uchunguzi? Je Kamati Ilizingatia Haki za Kikatiba na za Kisheria za walalamikaji (clouds) na mlalamikiwa (RC) katika uchunguzi wake??
2. Mamlaka ya Waziri wa Habari Kusimamia "media" yanamruhusu Waziri Kutoa Hukumu kwa Wanaodhaniwa Kuvunja Sheria? Kumbuka Hata Kabla ya Kamati Kuchunguza na Kutoa Taarifa, Tayari Waziri Alishasema Kwamba Makonda AMEINAJISI tasnia ya habari.
Kutokana na Kauli Hiyo, Je Kamati Ingetenda Haki Kiasii Gani Kwa Makonda Wakati Tayari Amehukumiwa Kabla ya Kusikilizwa????
3. Kamati inasema Makonda alivamia Clouds. Je tafsiri yao ya neno UVAMIZI ni ile inatambuliwa na Sheria ya Kanuni za Adhabu (The Penal Code) au ni tafsiri ya Kimtaani???? Kisheria, hakuna "UVAMIZI" uliofanywa na Makonda Clouds. Makonda alifunguliwa mlango au "kwa namna yoyote" aliruhusiwa au kutambuliwa na walinzi na wakamruhusu kuingia, sasa hapo UVAMIZI WA KIJINAI ukowapi????
Narudia tena, kisheria, ni kwa vipi useme Makonda alivamia clouds???? Tutofautishe "dhana ya uvamizi wa KIJINAI" na kile kilichoendelea mle ndani BAADA YA KUINGIA (Wanasheria Watanielewa).
4. Ni Upi Uhalali wa Kisheria wa Kamati ya Nape Endapo ITABAINIKA Haikuwa na Mamlaka ya Kisheria Kufanya Kazi ya Uchunguzi Uliofanyika???
5. Ni Upi Uhalali na UBORA wa Ushahidi Uliokusanywa (The Probative Value of the Evidence Collected) na Kamati ya Nape ILIHALI Tayari Hata Wanakamati Wenyewe Walikua Wameshamhukumu Makonda Hata Kabla ya Kumsikiliza? Neutrality na Objectivity Ikowapi??? Je Ushahidi Huo Unaweza Kusimama Mahakamani??
6. Nini Maana ya Kamati ya Nape Kwa Afya ya Serikali Yetu Chini ya Rais Dr.Magufuli??? Rais alipokuwa Ubungo Alieleza Kwamba Anafahamu Namna Mkuu wa Mkoa wa Dar anavyosakamwa Mitandaoni etc, na akamuasa MAKONDA Kuendelea Kuchapa Kazi Zake Kwa Bidii.
Nape kama Msaidizi wa Rais Kupitia Wizara ya Habari Kamati yake inatoa tafsiri gani? Je hii sio insubordination kwa Mkuu wa Nchi??
Naomba tutafakari Maswali Hayo Bila Mihemko na Tumtendee Haki Makonda. Tusimsakame Makonda na Kujaribu Kukwamisha Juhudi Zake za Kimaendeleo Katika Mkoa wa Dar