Udhaifu na ushupavu wa viongozi wetu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhaifu na ushupavu wa viongozi wetu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Jun 25, 2012.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hili la udhaifu wa kiongozi wa nchi limeongelewa sana katika vyombo vingi kufutia matamshi ya John Mnyika bungeni. Hivyo mawazo tofauti na dhana nyingi zimekuja ama kuunga mkono ama kupinga udhaifu uliotamkwa. Nimevutwa kuleta hoja kwani nilijikuta saa moja na robo asubuhi ‘ghafla' nikilitamka bila kujua- nilisema hivi "Mungu, Mwenye enzi yote, Baba wa Rehema. Mimi niliye maskini na DHAIFU na kuzaliwa katika hali ya dhambi naungama mbele zako dhambi zangu zote, nilizofanya kwa kuwaza na kwa kunena na kwa kutenda. Nimekukasirisha mara kwa mara. Nikastahili adhabu yako lakini nazijutia dhambi zangu na kutubu kweli ……"

  Najua tuko wengi ambao tuliungama hivi jana na kila jumapili (Mh John ulisali jana?).
  Swali langu kwa wadau ni je, uligundua kuwa unatamka 'neno la wiki' ? na je, ulifanya tafakari juu yake? Kwa wale wanaopenda tafakari hii ni fursa usiipoteze kwani hata kama ni mmoja wa wanaosema hayo ni ya mambo ya wabunge, ya wanasiasa, ya wanaharakati n.k. siyo kweli hata wewe mbona unalitamka?

  Katika mijadala ya wiki hii yako makundi mengi yaliyojadili mimi naongelea moja lile la wale wanaotaka tuamini kwa upande mmoja kuwa udhaifu ni upole na pia utu wema na pia ni demokrasia na pia ni utawala wa sheria na pia ni utawala bora …na kwa upande mwingine ushupavu wa kiongozi ni udikteta na pia ukatili na pia ni kukosa uvumilivu na pia ni kuvunja haki za binadamu …
  Mbona naona mtizamo huu una mushkeli?

  Nasema hivi kwani naamini kinyume chake ni kweli. Ushupavu wa kiongozi wa kizazi hiki ndiyo tegemeo la wanyonge, maskini, walala hoi ambao siku zote wameendelea kunyonywa, kunyanyaswa, kunyimwa haki, kunyimwa elimu na huduma zote za msingi na hata kufa kutokana na magonjwa mengi yanayoepukika na haswa hili donda ndugu liitwalo 'RUSHWA' .

  Tukiacha yote tuangalie hili donda ndugu rushwa, ambalo kweli linatutafuna na limekwamisha kabisa kila jitihada za serikali yetu, wafadhili na kila taasisi iliyotaka kumuondolea mtanzania umaskini. Ni ukweli usiopingika kuwa tumeshindwa vita hii, kuwa na taasisi mahsusi kushughulikia mapambano ya rushwa hakujatusaidia sana kumetuongezea mzigo wa taasisi nyngine ya kubeba.

  Kwa bahati mbaya watanzania tukiongozwa na viongozi wetu tumejijengea tabia au niseme ni hulka ya kusema uongo. Yako mengi ambayo yametushinda kama taifa na tumendelea nayo sasa kama hali ya kawaida. Tumekubali yasiyokubalika - kwa wananchi ni kutokana na kukata tamaa na kukosa msaada(na huu udhaifu) na kwa viongozi ni ‘business as usual'. Iko mifano mingi ambayo imefika mahali hata mtoto mdogo atakupa ukimuuliza. Baya zaidi ya yote ni pale hata viongozi wetu wa dini ambao ndiyo tulitegemea letu la mwisho nao hawasemi ukweli nao wamejiunga na jamii kuongopa au kwao watumia mbinu tofauti kwa kukaa kimya(huu ni udhaifu mkubwa). Kwa mtu yoyote mwenye uelewa wa kawaida anajua hakuna tofauti ya msingi kati ya kusema uongo na kunyamazia uovu na uongo. Niache hili la tabia ya kutokusema ukweli ili kwa leo niendelee na lile la rushwa na udhaifu wa viongozi wetu.

  Tupo hapa tulipo na rushwa kwani tumekosa mwenye ushupavu wa kupambana na rushwa. Maneno ya kupambana yanaonesha wazi siyo jambo la mchezo, huwezi ukafanya kama jana na ukaiweza rushwa lazima ujitoe mhanga na kuwa tayari kufa ndipo utatazamia mafanikio. Kwa tunavyopambana kila mmoja hashangai kuona tunashindwa iko wazi, dhamira ya dhati iko mbali na matendo na maneno yetu.

  Nakumbuka maneno ya rais Kagame wa Rwanda pale Arusha "I am proud to be a President of a country that has zero tolerance on corruption" tamko hili linatia moyo haswa pale unapojua asemaye anamaanisha.

  Tanzania tunakumbuka mifano ya ‘zero tolerance' iliyowahi kuoneshwa na viongozi wetu- nikumbushe mifano miwili, vita dhidi ya nduli Iddi Amini ambapo tulimpiga hadi akaikimbia nchi yake. Hapa chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere tulionesha hatutaki kumsikiliza yoyote juu ya hili. Mfano mwingine ni vita dhidi ya uhujumu uchumi chini ya kiongozi wetu shupavu Marehemu Moringe Sokoine. Tuliokuwepo tunajua yaliyotokea, kila mmoja alijua kweli kuwa tulikuwa na ‘zero tolerance'.

  Nikumbushe tu kuwa zero tolerance ni zero tolerance haitoi mwanya wa visingizio vya aina yoyote. Tunajua katika mapambano kuna wachache watakaopatwa na ‘friendly fire' hili linajulikana hata Iraq wapo wamerekani waliouwawa na wenzao lakini siyo kisingizio cha kutosonga mbele.

  Nasema tuukatae udhaifu wa viongozi wetu kwani 'mchezo wao ni mauti yetu'.
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Baadae kidogo jirani tutaonana!ngoja niingie msikitini kidogo nikaungame UDHAIFU wangu.
   
 3. L

  Luiz JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena.
   
Loading...