UDART huduma zenu ni duni

UDART huduma zenu ni duni

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
388
Reaction score
666
cc4c72f5ffff545fe08c735a817bccaa.jpg

Nimekuwa mtumiaji wa Huduma za UDART maarufu kama usafiri wa mwendokasi.

Binafsi Huduma za taasisi hii kiukweli zinatolewa chini ya kiwango tofauti na nchi nyingine duniani ambako huduma za namna hii zimekuwa zikifanyika..

Tukianza na Huduma ya CARD

Pamoja na kuwepo huduma hii katika taasisi hii lakini upatikanaji wake ni wa tabu japo wahusika wamekuwa wakirudisha lawama kwa wateja kuwa hawapendi kutumia card pindi wanapopanda gari zao lakini kwa upande wa Wateja wengi wanatoa lawama kwa UDART kuibiwa nauli zao kupitia card jambo ambalo limewafanya wateja wengi kuachana na issue ya card na kuamua kutumia risiti.

Naamini kuna ukweli katika kuibiwa kwa sababu ukiangalia center zote za mwendo kasi kuna Mashine ambazo mtumiaji anatakiwa kupanch ili aingie au atoke. Endapo mteja atatumia card kuingia na wakati wa kutoka akaacha kupanch card yake system inaendelea kumhesabu kuwa bado anatumia huduma na inaendelea kumkata pesa katika card.

Naamini huu unakuwa ni wizi sababu kuna center zingine mashine zimeharibiwa makusudi ili wasafiri wapite bila kupanch kama kituo cha Kimara Terminal Mashine hazina huduma hiyo japo zina huduma ya kuingia lakini kutoka unatoka free.

Upande wa Madereva

Wengi hawapo makini na kazi yao na hata ufuaji wa uniform kwao ni tatizo unaweza kupanda katika bus hizo unakutana na dreva kavaa kanzu na kiremba na mwingine kavaa pensi hafanani na mtoa Huduma hili linaonyesha kutokuwepo manager ambae anaratibu nidham kwa watumishi.

Kupitishwa vituo

Hili ni jambo la kawaida sana japo kuna kengele katika bus hizo nyingi hazifanyi kazi.

Madereva kuwabana abiria kwenye milango

Hili ni jambo ambalo linajitokeza mara nyingi na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kwa madereva.

Naamini kama tumeamua kuishi kistar basi tukimbizane na jua.
 
Kwani hata dereva akivaa Boxer shida iko wapi.???
Kubanwa milango si mnaamua kukomaa kama daladala gar imejaaa af unakomaa ujibanze kwnye mlango huo ni upuuzi
Kupitishwa kituo labda jangwani sabab hakina watu weng vingine hvo sijawaiona. mengine hayo sijui
 
Kinachotuponza sisi wa Wabongo ni ulimbukeni. Mtu amepewa ajira ya kusimamia usafirishaji wa abiria (watanzania wenzake), Badala ya kuifanya kwa heshima na kwa ustadi yeye anaona ni mahali pa kujikweza na kuonyesha wateja wake kuwa yeye ndo kila kitu katika usafiri huo. AIBU SANA.

Nyakati za jioni watu wanaoendelea na safari kwenda Mbezi wanacheleweshwa bila sababu. Magari yapo lakn eti ni mpaka gari moja lijae liondoke ndo waanze kupakia lingine, wakati abiria wamejaa kama utitiri!!

Kwa nini wasipakie kwa mpigo magari 2 au ma3??? Kwani msimamizi hawez kujiongeza? Kama ni kuhakikisha magari yanajaa, si abiria wapo wa kutosha? Siku abiria ni wachache si wataonekana? ACHENI ULOFA

Magari hayasimami pale stop ova watu wanakaa sana, hasa nyakati za asubuhi.
 
Hizo changamoto zitashughulikiwa but huduma yetu duni inasababishwa na mradi kuendeshwa kisiasa mfano East Africa nchi pekee ambayo mwanafunzi analipa transport charge ndogo ni Tz nchi zngne zote mwanafunz analipa half ya mtu mzima kwaiso operating cost ndzo zinatufanya tutoe huduma duni sababu ya hasara tunazozipata
 
cc4c72f5ffff545fe08c735a817bccaa.jpg

Nimekuwa mtumiaji wa Huduma za UDART maarufu kama usafiri wa mwendokasi.

Binafsi Huduma za taasisi hii kiukweli zinatolewa chini ya kiwango tofauti na nchi nyingine duniani ambako huduma za namna hii zimekuwa zikifanyika..

Tukianza na Huduma ya CARD

Pamoja na kuwepo huduma hii katika taasisi hii lakini upatikanaji wake ni wa tabu japo wahusika wamekuwa wakirudisha lawama kwa wateja kuwa hawapendi kutumia card pindi wanapopanda gari zao lakini kwa upande wa Wateja wengi wanatoa lawama kwa UDART kuibiwa nauli zao kupitia card jambo ambalo limewafanya wateja wengi kuachana na issue ya card na kuamua kutumia risiti.

Naamini kuna ukweli katika kuibiwa kwa sababu ukiangalia center zote za mwendo kasi kuna Mashine ambazo mtumiaji anatakiwa kupanch ili aingie au atoke. Endapo mteja atatumia card kuingia na wakati wa kutoka akaacha kupanch card yake system inaendelea kumhesabu kuwa bado anatumia huduma na inaendelea kumkata pesa katika card.

Naamini huu unakuwa ni wizi sababu kuna center zingine mashine zimeharibiwa makusudi ili wasafiri wapite bila kupanch kama kituo cha Kimara Terminal Mashine hazina huduma hiyo japo zina huduma ya kuingia lakini kutoka unatoka free.

Upande wa Madereva

Wengi hawapo makini na kazi yao na hata ufuaji wa uniform kwao ni tatizo unaweza kupanda katika bus hizo unakutana na dreva kavaa kanzu na kiremba na mwingine kavaa pensi hafanani na mtoa Huduma hili linaonyesha kutokuwepo manager ambae anaratibu nidham kwa watumishi.

Kupitishwa vituo

Hili ni jambo la kawaida sana japo kuna kengele katika bus hizo nyingi hazifanyi kazi.

Madereva kuwabana abiria kwenye milango

Hili ni jambo ambalo linajitokeza mara nyingi na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kwa madereva.

Naamini kama tumeamua kuishi kistar basi tukimbizane na jua.
Juzi kati dereva aliwapitisha vituo jamaa,daaah ile kuwashusha pale shekilango wakaenda kumtolea uvivu dereva ,nusura wamtolee dirishani bahati nzuri mlinzi alifika haraka kutuliza fujo.
 
Back
Top Bottom