Udanganyifu wa umri ni tatizo sugu

Mungu Mweusi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
1,474
1,079
Wanajamvi habari za jioni?

Napenda kufahamu kwa nini tumekuwa tukitumia umri baada ya kuzaliwa na ilihali tunaacha miezi 9 ya kabla ya kuzaliwa? Pia kama ni hivyo Je? Kwanini mmea huesabiwa umri tangu tarehe ya kupandwa lakini kwa binadamu ni tofauti?
 
Binadamu huanza kuhesabiwa pale anapozaliwa. Wewe kaa tumboni hata miaka kumi... utaitwa mimba ya miaka kumi. Ukitoka ndiyo utahesabiwa kama mtu mzima..
 
Binadamu huanza kuhesabiwa pale anapozaliwa. Wewe kaa tumboni hata miaka kumi... utaitwa mimba ya miaka kumi. Ukitoka ndiyo utahesabiwa kama mtu mzima..

Kwa nini? Naomba hoja maana kama ni hivyo kuna uongo mkubwa katika umri, unapotoka kuzaliwa unakuwa binadamu kamili kwa nini wanapima kilo ulizozaliwa Nazo umri wako wanaacha kuhesabu?
 
Kwa nini? Naomba hoja maana kama ni hivyo kuna uongo mkubwa katika umri, unapotoka kuzaliwa unakuwa binadamu kamili kwa nini wanapima kilo ulizozaliwa Nazo umri wako wanaacha kuhesabu?
Kabla ya kuzaliwa hakuna tofauti na baada ya kufa. Ukifa miaka inaanza kuhesabiwa moja...
 
Kwa mawazo yangu mimi nikifikiria jinsi tulivyo na mambo mengi muhimu yanayohitaji kukuna vichwa vyetu ili kuyapatia ufumbuzi sidhani kama na hii hoja yako inahitaji muda na resources zingine kulifikiria.

Na kama nalo ni tatizo linalohitaji mjadala basi jibu lake ni rahisi tu. Kwamba kwa sababu imeshazoeleka kuhesabu umri wa binadamu kwa kuanzia tarehe aliyozaliwa ukitaka kumhesabia tangu mimba yake kutungwa ongezea tu miezi tisa na kupata umri wake kimoyomoyo. Kama alizaliwa njiti ni kumwuliza mhusika ili uongeze miezi au siku pungufu kwenye umri wake.

Na kuhusu mimea uliyotolea mfano nayo inahitaji tusihesabu umri wake tangu ilipopandwa na badala yake tuhesabu na siku zilipopatikana hizo mbegu zake, muda ziliokaa zikiwa zimehifadhiwa hadi siku ya kuzipanda?
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini? Naomba hoja maana kama ni hivyo kuna uongo mkubwa katika umri, unapotoka kuzaliwa unakuwa binadamu kamili kwa nini wanapima kilo ulizozaliwa Nazo umri wako wanaacha kuhesabu?
Basi We Anza Kujihesabia tangu ulipokua mimba,acha sisi wengine tuendelee na utaratibu wetu.
 
Watu wengi sana wanadanganya umri wao hata baada ya kuzaliwa ukiacha hata iyo ya mimba kutungwa. Hili nalo jipu lazima magu alishtukizie na kulitumbua maana tumechoka
 
Watu wengi sana wanadanganya umri wao hata baada ya kuzaliwa ukiacha hata iyo ya mimba kutungwa. Hili nalo jipu lazima magu alishtukizie na kulitumbua maana tumechoka
Magufuli mwenyewe amempa unaibu Waziri Bwana Masauni yule alietimuliwa UVCCM kwa kashfa ya kufoji umri.
 
Kwa mawazo yangu mimi nikifikiria jinsi tulivyo na mambo mengi muhimu yanayohitaji kukuna vichwa vyetu ili kuyapatia ufumbuzi sidhani kama na hii hoja yako inahitaji muda na resources zingine kulifikiria. Na kama nalo ni tatizo linalohitaji mjadala basi jibu lake ni rahisi tu. Kwamba kwa sababu imeshazoeleka kuhesabu umri wa binadamu kwa kuanzia tarehe aliyozaliwa ukitaka kumhesabia tangu mimba yake kutungwa ongezea tu miezi tisa na kupata umri wake kimoyomoyo. Kama alizaliwa njiti ni kumwuliza mhusika ili uongeze miezi au siku pungufu kwenye umri wake. Na kuhusu mimea uliyotolea mfano nayo inahitaji tusihesabu umri wake tangu ilipopandwa na badala yake tuhesabu na siku zilipopatikana hizo mbegu zake, muda ziliokaa zikiwa zimehifadhiwa hadi siku ya kuzipanda?

Usiwe mwepesi kiasi hicho kudharau hoja za wengine, utakuwa na katabia ka kukurupuka wewe
 
Usiwe mwepesi kiasi hicho kudharau hoja za wengine, utakuwa na katabia ka kukurupuka wewe

Hapana mkuu. Siko hivyo. Ila kubali kwamba hoja yako ya kutaka umri wa mtu uanze kuhesabika tangu siku mimba inaingia siyo "kipaumbele". Ukitaka kuamini ninachokwambia anza kwa kuhesabu idadi ya wachangiaji hadi sasa.
 
Back
Top Bottom