Udanganyifu mitihani drs la saba serikali mmeyataka wenyewe.

Udanganyifu mitihani drs la saba serikali mmeyataka wenyewe.

Kwisaro

Member
Joined
Mar 28, 2018
Posts
30
Reaction score
45
Ukiangalia suala la udanganyifu wa mitihani ya drs la 7 kwa shule za umma serikali inaweza ikawa imechangia kwa kiasi kikubwa. Sababu kubwa ni posho za walimu wakuu laki 2 ambapo walimu wakuu ambao wataonekana kutofanya vizuri kwenye matokeo ya drs la 7 wako hatarini kupoteza nyadhifa zao pamoja na posho!Hivyo hivyo kwa maafisa elimu kata.Kwa upande wa maafisa elimu hofu yao ni kushushwa madaraka. Kwa upande wa shule binafsi wao wako kibiashara ili waonekane wamefanya vizuri ili kupata idadi kubwa ya wanafunzi.Tusilaumiane hayo ndio matokeo ya BIG RESULT NOW
 
Tanzania Tanzania ni nchi ya kishoo shooo? Aliponzwa James Delicious tukamlaumu lakini kumbe hata mawaz.....Ni mashooshoooshoooo
 
Wanataka kufaulu kwa kuvunja rekodi wakati hakuna miundombinu ya elimu mizuri
 
Tatizo ni kwamba wakuu wa mikoa na walaya ambao ni wateule wa mkulu ndiyo wanaharibu kwa kuingilia mambo ya elimu kisa aonekane mkoa au wilaya yake imefaulisha si wameambiwa wakachape kazi,sasa wanashinikiza kufaulisha watoto na wanachokifanya ni kutoa maelekezo kwa afisa elimu mkoa,wilaya na kata ambao na wao wanatoa mikakati kwa walimu wakuu kwa kuwapa mikakati ya kufaulisha bila kujali uelewa wa watoto maana mkuu wa mkoa anataka aonekane mkoa wake umefanya vizuri kitaifa.
Hii cheni ni ndefu hata hao walimu wakuu ni kama kuwaonea tu maana yeye anaambiwa tu tunataka watoto wafaulu sasa wanachokifanya ni kuiba mtihani maana hakuna asietaka cheo jamani.
 
Hao walikuwa wapumbavu...walitaka kufaulisha kwa 100%•••

Wenzao wanang'ata kidogo na kupuliza.
 
Nimekuwa nikilizungumza hili mara kwa mara. Tutahangaika tu kumtafuta mchawi wakati tunamjua. Miaka inazidi kwenda, hali ya maisha ya mwalimu yanazidi kuzorota, waalimu hawaoni nuru katika kazi yao ila hawana wa kuwatetea, hakuna wa kuwasemea. Wao wakiwa wanalipana posho na mishahara minono, mwalimu huku Magumu ndiyo yanayomstahiili.
 
Nsanzu mwalimu baada ya kumsaidia mwl wanawaza namna ya kumdhoofisha kwa kuona leseni ndio suluhisho
 
Back
Top Bottom