UDABRT/SUMATRA IPI NAULI HALALI MBEZI POSTA V/S


H

hps300

Senior Member
Joined
Feb 20, 2016
Messages
171
Likes
149
Points
60
H

hps300

Senior Member
Joined Feb 20, 2016
171 149 60
Uongozi wa UDABRT na SUMATRA ni wakati mwafaka sasa mjitokeze kutueleza ipi nauli halali Mbezi/Posta au Mbezi/Moroco ama kinyume chake. Nasema hivi kwa sababu mlitueleza kuwa nauli toka njia za pembeni kuunganisha njia kuu itakuwa shilling mia nane (800) lakini kwa sasa hali ni tofauti kwa abiria wa Mbezi kwani hata kama una kadi ukifika Kimara lazima uscan card yako kutoka kituoni na unapoingia kwenye gari uscan kadi kuingia kwa maana ya kwamba ulipe shilingi mia sita hamsini toka Posta, jumlisha mia nne toka Kimara Mbezi. Jumla ni shillingi 1050/=.

Ni mwananchi huyu huyu ambaye ni mfanyakazi , amelipa kodi (PAYE) anenda benki kuchukuwa kamshahara kaliko baki analipa tena tozo ya asilimia 18% VAT, Akirudi mtaani mwenye nyumba naye kapandisha kodi ili kubalance Tangazo la Serikali kulipa kodi ya nyumba, Sukari ambayo kabla alinunua shilingi 1900 leo ni shilingi 2600-3000 ongezeko la shilingi 700 mpaka 1400. Kodi aliopunguziwa yeye ni asilimia mbili tu ya mshahara wake.

Akirudi Dawasco ametangaziwa kuna ofa ya kupata maji, kajipiga piga kavuta maji. Maji hayatoki na vituo vya kuuza maji vinauza maji kila siku. Kama anafamilia badala ya kutumia maji ya elfu 20 mpka 30 anatumia elfu 60 mpaka 90 kwa mwezi.

Ni hitimishe kwa kurudi kwenye hoja yangu ya msingi, UDABRT tulitarajia mlete unafuu lakini tofauti yake ni shida juu shida, nauli juu, magari hayafiki vituoni kwa wakati, asubuhi tunalazimika kukaa kituoni kwa zaidi ya dk 20 mpaka 30 kusubiri gari, watu ni wengi kuliko namba ya magari. Kuelekea Mbezi ndo usiseme kabisa, unapanga Mstari kusubiri gari zaidi dk 30 mpaka 40. Mbaya zaidi ikifika saa tatu usiku tayari hamna gari ya kwenda Mbezi ili hali kuna magari yenu ya kutoka Kariakoo, Posta na Moroco kwenda Kimara. Kwa nini na ya Mbezi yasifanye kazi mpaka Muda huo?

Tunaomba mtueleze nauli halali ya Route zenu, Mbezi Posta, Mbezi Kariakoo na Mbezi Moroco. Moroco Mbezi, Kariokoo Mbezi na Posta Mbezi. Natambua hamna Route ya moja kwa moja lakini mlituambia kuna Feeder Route ambazo ndo zinakamilisha nauli ya shilingi 800. Sio tatizo kulipa elfu moja lakini iwe documented na sio ionekane tu kwenye media na siyo halisi. Mimi ni mtumiaji mzuri tu wa mabasi haya kadi yangu 2000 0029 9063

Naomba ni mnukuu Mkurugezi wa Sumatra, Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya Kimara kwenda Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo – Kivukoni.

Amesema nauli ya Sh800 Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.

“Chombo chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa reseni za biashara zao” amesema.
Source:Mwananchi
 
Chuck j

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Messages
2,276
Likes
583
Points
280
Chuck j

Chuck j

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2011
2,276 583 280
Wanakulabmatapishi yao
 

Forum statistics

Threads 1,237,319
Members 475,533
Posts 29,284,392