UDA/simon group yazindua mabasi 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDA/simon group yazindua mabasi 15

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 8, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  KAMPUNI ya Simon Group, imekabidhi mabasi 15 kwa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) yenye thamani ya sh bilioni 2.1 kwa lengo la kurahisisha usafiri jijini yatakayoanza kufanya kazi leo.
  Akizungumza na waandishi wa habari katika makabidhiano hayo, Mwenyekiti Mtendaji wa Simon Group, Robert Kisena, alisema huo ni mpango wa muda mfupi wa uwekezaji na uendelezaji katika UDA, lengo likiwa ni kuingiza mabasi mapya 300 ifikapo Machi mwaka 2013 yenye thamani dola milioni 25 za Marekani.
  “Kati ya mabasi 300 kutakuwa na mabasi maalumu 20 ya kubeba wanafunzi ambayo yatagawanywa katika njia zote kuu jijini hapa, lengo likiwa ni kuwaondolea watoto wetu adha ya kunyanyaswa, kutukanwa na wakati mwingine kusukumwa na kuumizwa na makondakta wa daladala wasiokuwa na roho ya utu,” alisema Kisena.
  Kisema alifafanua kuwa kutakuwa na mabasi maalumu ya kubeba wanawake pekee yatakayojulikana kwa jina la ‘Malaika’ ambapo kama ilivyo kwa mabasi ya wanafunzi kwamba watayagawanya katika njia zote kuu.
  Alisema lengo ni kuwapunguzia usumbufu kina mama wa Dar es Salaam ambao alidai kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiteseka kupigana vikumbo na wanaume katika kugombania usafiri maeneo mbalimbali.
  Alisema mazingira mabovu ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam mara kwa mara yamekuwa yakisababisha udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake, huku akikumbushia kisa cha ‘Maumba’ aliyekuwa akiwadhalilisha wanawake katika baadhi ya daladala zamani.
  Alisema pia kutakuwa na mabasi ya daraja maalum ambayo yatatoa huduma kwa watu wasiotaka kutumia usafiri wa umma ambayo yatakuwa na kiyoyozi, huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusoma magazeti, vinywaji baridi na kwamba watumiaji watalipa nauli kubwa tofauti na usafiri wa umma.
  Alisema lengo la kuweka usafiri wa aina hiyo ni kuwapunguzia gharama za usafiri wananchi wa Dar es Salaam, wanaomiliki magari ambao kwa sasa wanatumia zaidi ya sh 100,000 kama gharama za mafuta ya magari yao.
  Alisema pia UDA itakuwa na mabasi mengine maalumu kwa ajili ya kukodisha kwa taasisi mbalimbali za umma na binafsi ambazo zinataka kubana matumizi ya usafiri kwa wafanyakazi wake.
  Kisena alisema kuwa kampuni hiyo licha ya kusaidia usafiri katika jiji la Dar es Salaam, dhamira nyingine ni kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana kwani mabasi 300 yatakayoingizwa yatazalisha ajira 900 za moja kwa moja na ajira 2000 ambazo zitapatikana kupitia wafanyazi 9000 kwa wategemezi wao.


   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ile kesi ya Idd simba kufisadi UDA imeishia wapi? au kwa vile Idd simba ni m/kiti wa wazee wa Dar es salaam!

  Hawa simon Group inaelekea watapata dili la kuendesha mradi wa mabasi ya kasi hapa Dar.
   
 3. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Picha tafadhali.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huu ni upuuzi wa hali ya juu!. Dar es Salaam haihitaji mabasi, kinachotakiwa ni Trams na train, basi!
  Nani amekuja na idea ya mabasi 300? Huyo mtu anatakiwa apelekwe Keko, hafai kabisa na hana la maana la kuongeza kwenye jiji linalokuwa kama Dar es Salaam.

  Mabasi 300, kwanza hiyo pollution watu watapita wapi? Na pia bei ya hayo mabasi si ingetosha kukarabati njia za train? Au zingechangia kuwekeza kwenye njia za Trams?
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Barabara zenyewe zipo wapi?
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hii group si ilikuwa na kashfa ya mabasi? Wameendelea kuwepo tu!!!
   
 7. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Duuu wameamua kuongeza foleni za barabarani sasa, Mwakyembe lete treni zako bana
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Magumashi matupu...hii deal sio illegal?
   
Loading...