UCL Final: PSG Vs Bayern Munich

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
21,161
46,263
Leo jumapili ya 23/08/2020 baada ya watu kumaliza shughuli zao, kazi itakuwa ni moja tu, huko Estadio da Luz, nchini Ureno ambapo kutapigwa Fainali ya aina yake kati ya PSG Vs Bayern Munich.

Ni fainali inayowakutanisha PSG ambao wameingia fainali yao ya kwanza dhidi ya mabingwa mara 5 wa kombe hilo Bayern Munich.

Ni Fainali inayozikutanisha timu zinazocheza mpira wa kushambulia tangu dakika ya kwanza mpaka ya mwisho, hasa Bayern Munich yenye vijana wenye kasi sana!

PSG itaingia uwanjani ikiwategemea zaidi Neymar na Mbappe huku Bayern Munich maarufu kama "The Bavarians" wakiwategemea zaidi Mshambuliaji hatari zaidi kwasasa ulinwenguni Robert Lewandowski na Thomas Muller mzee wa nafasi.

Bayern Munich anapewa nafasi kubwa ya kutwaa ndoo kutokana na soka lao linalotengeneza zaidi nafasi nyingi za magoli.

Mechi itapigwa saa 4:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki!

Utabiri wangu ni baada ya mechi kuisha namuona Captain Thiago Silva wa PSG akienda kubeba ndoo! PSG atashinda 2-1

Tupia na wewe utabiri wako...
IMG_3688.JPG
 
mzee baba hii ni final ngumu sana.mbona umechagua optn ya magoli mengi?
Sio ngumu hii kwa psg kupata magoli,bayern wanafunguka sana,kitu ambacho neymar ,mbappe,di maria hawataweza kukosa goli 3 pale.kingine bayern wanatengeneza nafasi nyingi za magoli,nao watafunga mengi tu,suala la nani kushinda litaamuliwa na mwenye uwiano mzuri wa kufunga na kufungwa magoli.nina imani goli zipo nyingi tu kama game ya sevilla na inter
 
Sio ngumu hii kwa psg kupata magoli,bayern wanafunguka sana,kitu ambacho neymar ,mbappe,di maria hawataweza kukosa goli 3 pale.kingine bayern wanatengeneza nafasi nyingi za magoli,nao watafunga mengi tu,suala la nani kushinda litaamuliwa na mwenye uwiano mzuri wa kufunga na kufungwa magoli.nina imani goli zipo nyingi tu kama game ya sevilla na inter
Umechambua vizuri umenipatamaa.ila ngoja tuone mpira dk 90.
 
Jana nilisikia Clouds FM jamaa wanatoa statistics, kwamba Chelsea ilinunuliwa na tajiri ikaja kuchukua kombe baada ya miaka tisa, iliingia Final na hawa Bayern Munic.

PSG nayo ni miaka 9 toka inunuliwe na matajiri wa mafuta, imeingia Final na Bayern Munic.

Probably, historia nyingine inaenda kuwekwa.
 
Leo katika hisia zangu nayaona maajabu yanaenda kutokea huku ndani ya PSG kukiwa na ahadi nyingi kutoka kwa mwarabu wao kama mmiliki wa club.

PSG kama watashindwa kushinda mechi hii basi wasitarajie tena kufika robo fainal ya UCL.

Maoni yangu:

PSG kama watahitaji heshima ya kuwa club kubwa kama wenzao Bayern au big club ambazo zimewahi kutwaa ubingwa wa mabingwa wa ulaya, basi wanatakiwa kushinda game ya leo japo battle itakuwa kubwa sana.
Hivo basi kama leo PSG atashinda utabiri wangu ni huuCorrect score PSG 2:1 Bavaria.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom