Uchunguzi wa Afya Muhimbili (Health Check)

Dec 5, 2011
78
125
Kuna rafiki yangu aliniforwardia hili tangazo la health check muhimbili kama miezi sita iliyopita.
Jumamosi iliyopita nilienda kwa kweli nilifurahia sana huduma zao.
Nimeona sio vibaya kuliweka hili tangazo hapa kwa wana JF wenzangu nao wakalisoma na kwa wanaoweza kufanya hii check up angalau mara moja kwa mwaka wakajua sehemu ya kwenda kufanyia, hii kitu ni muhimu sana katika maisha. Tusiwe tunafanya service za magari tukasahau za miili yetu pia! Jisomee mwenyewe hilo Tangazo!

TANGAZO KWA WANANCHI WOTE KUHUSU UCHUNGUZI WA AFYA
Hospitali ya Taifa Muhimbili inafurahi kuwakaribisha wananchi wote kwenye huduma za upimaji wa afya kwa gharama nafuu. Baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu (high blood pressure) na saratani (cancer) hayana dalili zozote hadi yanapokuwa yameadhiri sehemu nyingi za mwili na kuleta madhara makubwa. Kwa mfano, wagonjwa wengi wa kisukari (Diabetes) hugunduliwa kwa sababu ya kupoteza fahamu ambayo hutokea ghafla baada ya ugonjwa kuanza. Shinikizo la damu (high blood pressure) inaweza kugundulika kwa mara ya kwanza mgonjwa anapopata kiharusi (Stroke) au anapogunduliwa kuwa na ugonjwa wa figo, moyo kushindwa kufanya kazi, n.k. Hali hii inathibitishwa na takwimu mbalimbli hapa hospitalini ambazo zinaonyesha kuongezeka kwa idadi kubwa ya wagonjwa ambao wanaletwa wakati wameshaathirika sana kiasi cha kuwa ngumu kwa madaktari na wahudumu wa afya kuwasaidia kurudi katika hali yao ya awali kitu ambacho kingeweza kuzuiwa kama hali hio ingejulikana mapema Huduma zinatolewa saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana kila siku za jumamosi katika jengo la wagonjwa wa nje (cold clinic) ambalo ni jengo la kwanza upande wa kushoto unapoingia kupitia geti la kuingilia magari Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Huduma hii inatolewa na wataalamu bingwa waliobobea kwenye fani zate za afya katika hospitalai hii ya Taifa. Huduma zinatolewa katika mfumo wa vifurushi (packages) zinazojumuisha mahojiano kati ya mteja na mhudumu wa afya kwa kina, upimaji wa mwili kitabibu vipimo vya maabara (FBP,Lipid profile, VDRL,Hepatitis, Blood Glucose, Renal profile, Liver enzymes, PSA, Urinalysis, Stool analysis), radiologia (Chest X­-ray, mammography) na kipimo cha moyo ECG. Vipimo kama Ultrasound,ECHO, CT-Scan na MRI vitafanyika vinapohitajika na sio sehemu ya vifurushi hivyo. Huduma hii ni ya kulipia lakini bei yake ni nafuu ulikinganisha na huduma ya kibingwa itakayotolewa kwa mteja. Gharama ya uchunguzi huu kwa kifurushi ni Tsh.188,000 kwa mwanaume na Tsh.193,000 kwa mwanamke. Mwisho wa huduma ushauri wa kitaalamu utatolewa kwa tatizo lolote litakaloonekana na mgonjwa ataingizwa katika clinic za hospitali za madaktari bingwa kutokana na tatizo lake. Kama hakuna tatizo lililoonekana ushauri utatolewa namna ya kujikinga au kuepuka magonjwa mbalimbali na jinsi ya kuishi kwa afya njema. Kwa mawasiliano na kuweka appointment wasiliana na afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Barua pepe (Email) healthcheck@mnh.ac.tz au mnhhealthcheck@gmail.com Pia unaweza kutembelea Website yetu www.mnh.ac.tz
KUMBUKA, KINGA NI BORA KULIKO TIBA
 

sakilo

Member
Oct 13, 2012
5
0
Nimejaribu kuwasiliana nao kupitia barua pepe kwa Email ulizotoa zote zinaonyesha hazi exist sielewi kwa nini.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
78,144
2,000
Poa kaka , tutakuja ,maana hivi vitambi vingine hadi mashaka ! Tumbo kubwa halafu shingo ndogooo ! Uchunguzi ni muhimu .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom