UCHUMI WANAYAUKA!!

Joined
Apr 23, 2012
Posts
76
Reaction score
71
Gazeti la JAMBOLeo, jumapili, 16-10-2016 linaandika,

'UCHUMI WANYAUKA'..,
Benki Kuu yakiri hali mbaya karibu kila sekta muhimu....

.., najiuliza hapa maswali sipati jibu.., huyu Gavana wa benki kuu, Profesa Beno Ndulu, mwezi uliopita (Septemba) alitoka mbele ya waandishi wa habari na kuwaeleza watanzania kwamba UCHUMI UNAIMARIKA KWA KASI SANA..., mwezi haujamalizika mwingine, zinatoka taarifa zingine...

Mwaka huu tutaona, tutasikia na tutasadiki mengi sana, sitaki kuamini hata wale wasomi wetu katika taifa hili wameamua kujivika miwani za mbao na wanapiga makofi kusifia 'kitumbua' chao na kumfurahisha mfalme!

Tunafanya kazi kwa ajili ya wananchi wa taifa hili au tunafanya kazi ili kumgurahisha mfalme...!!? Kwanini tumeamua kuacha akili zetu na maarifa yetu yote sasa tunaishi kwa kusadikika!!?

Huyu anasema uchumi unakuwa kwa kasi (kumbe hali ni tete).., yule anasema dawa zipo za kutosha (kumbe ni maigizo).., yule anasema kuna ukaguzi na uhakiki (kumbe ni maziongaombwe ya kuchelewesha ajira rasmi).., yule anasema makusanyo yameongezeka (kumbe ni hadithi za soga za mzawa)..

Mimi ni shuhuda.., nitashuhudia mengi sana.., hili ni ajabu la 36 tangu novemba 2015.., naendelea kuyarasimisha maajabu hayo!

Martin Maranja Masese,
Mwananchi wa kawaida.
 

Hali mbaya sana waliokuwa wanaficha ukweli sasa maji yamewafika shingoni wameamua kusema ukweli.
Uchumi wanyauka.
 
Sababu ya escrow, waliohusika wakamatwe na kufikishwa mahamani
 
Tufanye jitihada za kuumwagilia uchumi wetu ustawi.
Kumbe sababu ni mfuko umepwaya hadi mtukufu ameamua kujificha kwenye kivuli cha uhakiki watumishi hewa na kuamua:
1. Kusitisha ajira mpya
2. Kusitisha kupandishwa madaraja
3. Kusitisha kuwalipa waliopanda madaraja

Tutaelewana tu awamu hii.
 
Tunashughulika kwanza na vyeti hewa wanafunzi hewa,

Hadi tukifika kukagua UCHUMI Hewa basi jua mashetani wote tutakuwa tumekufa na njaa mtabaki Malaika tu
 
Ndio maana Tanzania kila kukicha inakua masikini kutokana na kauli za wasomi makanjanja hata huyo Ndulu nae yupo katika hilo kundi...
 


Lakini hebu tuwe na akiba ya maneno, hili gazeti Jambo leo halijaonyesha source ya headline yake! Hii sidhani kama ni kauli rasmi ya Benki kuu au Gavana Ndulu 4 that matter! Tutafute ukweli usio na shaka licha ya hali mbaya ya wananchi mitaani.
 
Kweli kabisa inasikitisha sana pale ambapo unasaliti taaluma yako na kufanya mambo ili kumfurahisha mtu
Kunamwananchi aliniambia tanzania hakuna wasomi nilimbishia sana
Mwingine akasema kiutafiti watanzania wengi ni wagonjwa wa akili nikashangaa Ila kwa yanayotokea sasa looo yote ni kweli
 
Nilimpenda Mbalawa akijibu swali bungeni bila porojo kama tulizozizoea za mawaziri wabunge wa kijani na manjano. Alisema "mpango ni kuzitengeneza barabara zote ila tatizo ni pesa, pesa ikipatikana utekelezaji utafanyika" No longolongo za kipuuzi
 
Lakini hebu tuwe na akiba ya maneno, hili gazeti Jambo leo halijaonyesha source ya headline yake! Hii sidhani kama ni kauli rasmi ya Benki kuu au Gavana Ndulu 4 that matter! Tutafute ukweli usio na shaka licha ya hali mbaya ya wananchi mitaani.
Kama hiyo taarifa haina ukweli ....... ni UCHOCHEZI....
 
Kama hiyo taarifa haina ukweli ....... ni UCHOCHEZI....


Ndio! Jambo leo watwambie chanzo cha taarifa yao "Uchumi wanyauka!" Inatisha na kusikitisha sana. Hatujaona, kusoma wala kusikia popote taarifa rasmi ya Benki kuu wala Gavana Ndulu!
 
Mbona tuliambwia kuwa uchumi unakuwa Kwa kasi Na mfumko wa bei umeshuka ?
 
Hv kuna mtu atakuamisha umeshiba wakati unanjaaa??
 
Uchumi unanyaukaje wakati TRA kila mwez mapato yanakusanywa ya kutosha na bado sehem nyingne za makusanyo ya kodi yataongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…