Uchumi wa Tz ukikua kwa kasi A.Mashariki, Uuzaji bidhaa za viwandani nje umeshuka kwa Sh700 bilioni

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
Wakati Serikali ikihimiza safari ya kuelekea uchumi wa viwanda, mauzo ya bidhaa za viwandani yameshuka hadi kufikia dola bilioni moja za Kimarekani (sawa na Sh2.3 trilioni), ripoti ya tathmini ya uchumi ya Benki Kuu (BoT) imeeleza.

Mwaka jana mauzo hayo yalifikia dola 1.32 bilioni za Kimarekani (sawa na Sh3.03 trilioni).

Tathmini hiyo iliyotolewa juzi inaeleza kushuka huko kwa mauzo kulichangiwa na kushuka kwa usafirishaji wa bidhaa za chuma na bati pamoja na mafuta ya kula.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa deni la nje limeongezeka mpaka dola 17.56 bilioni (sawa na Sh40.39 trilioni) wakati la ndani likifika Sh10.65 trilioni na kufanya jumla ya Sh51.04 trilioni.

Deni la nje liliongezeka kwa dola 102.2 milioni (235.06 bilioni) kutoka Februari mpaka Machi ilhal la ndani likipanda kwa Sh166.8 bilioni ndani ya muda huo. Ripoti inaeleza sehemu kubwa ya mikopo iliyochukuliwa ilielekezwa kufidia pengo la bajeti.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Diana Mwiru alisema kutofanya vizuri kwa sekta ya uzalishaji si jambo jema kwa kuwa huathiri sehemu nyingi.

“Viwanda hutumia malighafi za ndani, ajira na kuipa uhai sekta ya usafirishaji. Kutofanya vizuri kwa sekta hii, maana yake watu wengi wanakosa uhakika wa kipato,” alisema Dk Diana.

Dk Diana alisema katika biashara, mkopo huwa na manufaa ukielekezwa katika uzalishaji na kinyume chake ni kujiongezea mzigo.

“Juhudi za Serikali kubana matumizi yasiyo ya lazima na kupunguza mianya ya rushwa inapaswa kuondoa ulazima wa kukopa kwa ajili ya matumizi ya kawaida,” alisema.

Itakumbukwa kuwa hadi Februari, Serikali ilikuwa imetumia asilimia 34 tu ya Sh11.8 trilioni zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na miongoni mwa sababu zilizoelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ni kutokopa kutoka nje kama ilivyopangwa.

Ripoti ya BOT inaonyesha kuwa hali ilikuwa nzuri katika sekta ya madini na utalii ambako mapato yake yaliongezeka. BoT inabainisha thamani ya bidhaa na huduma zilizouzwa nje ya nchi kwa mwaka unaoishia Machi 2017 imeongezeka kwa Sh451.5 bilioni.

Ongezeko hilo ambalo ni kutoka dola 8.98 bilioni za Kimarekani zilizopatikana Februari mwaka 2016 mpaka dola 9.17 mwaka huu limechangiwa na kuimarika kwa mauzo ya dhahabu na utalii.

Mapato ya utalii yalipanda kwa asilimia 4.1 na kuliletea Taifa dola 2.13 bilioni (sawa na Sh4.9 trilioni) baada ya idadi ya watalii walioingia nchini kuongezeka.

Ripoti pia inaonyesha kuwa thamani ya usafirishaji wa mazao imepanda hadi dola 896.7 milioni (sawa na ongezeko la asilimia 17.8), ikichangiwa zaidi na mauzo ya korosho yaliyoongezeka kwa kiwango na thamani huku mauzo ya kahawa, katani, chai na karafuu yakishuka.

Ufasirishaji wa mazao yasiyo ya kilimo, hasa dhahabu, uliimarika zaidi na kuliingizia taifa dola 1.47 bilioni (sawa na Sh3.38 trilioni) baada kuongezeka kwa bei na kiwango kilichouzwa nje.

Madini na Utalii ndiyo mkombozi bado

Lakini swali lakujiuliza je sekta hizi zimeajiri watanzania wangapi? Watanzania wangapi wanabiashara kwenye hizi sekta?
 
Msijali wanajamvini wenzangu. BOT imepunguza bank deposit na kurudisha balance kwenye mabenki binafsi ili yaweze kukopesha zaidi, ongera governor kwa kusikia kilio chetu, uchumi utaendelea kuimalika sasa. uchumi unagusa maisha ya kila mtanzania, hivyo ni vyema husichezewe na mtu yoyote.
 
Imepeleka kiasi gani kwenye commercial banks?

Kwani utaratibu ndiyo upo hivi?

Nilidhani central bank inachofanya inapunguza kinaochotwa"required minimum balance" ambayo commercial bank inatakiwa iwenayo central bank?

Central bank ikifanya hivyo commercial banks zinapata fedha kwa urahisi zaidi na hatimaye kukopesha kwa wananchi. Hii njia ni poa haileti interruptions kwenye mzunguko wa fedha
 
central bank ilikua mpaka bank iweke deposit ya 60 billion ndio operation ziendele, but now it is 40 billion sababu ni kurudisha 20 bilion kwenye bank usika ili zikopeshe zaidi, yani ile dhamana imerudishwa kwenye mabenki usika.
 
Inaonekana uko vizuri kwa uelewa wako. Swali: Je wanakupesheka hao wakopaji? Kumbuka riba imepanda kwa mikopo ya kawaida kwa zaidi ya asilimia 4.
 
Hapa kazi tu. Uchumi umekua sana. Huku tunanunua kilo 1 ya sukar 3000 mpaka ifike 2020 tutanunus kwa 10,000 hii bei ni kwa wapinzani. Ccm wao huwa wananunua kwa 1800 tu. Ukienda duka lolote kununua sukari ww onesha kadi yako tu ya ccmu. Utapata kwa 1800
Anayesubiria nchi ya viwanda ni mwendawazimu na kiziwi. Siyo kwa uongoz wa ccm. Mtasubiri sana hivyo viwanda. Ccm ndiyo kawaida yao kuwadanganya watu,
Mtasubir viwanda mpaka miguu ingie tumbon. Viwanda ni kelele za wajinga tu.
Sukari 3000 sasa ukija kutahamaki 5000 kilo 1 na bado unaimba hapa kazi tu na nchi ya viwanda
 
Inaonekana uko vizuri kwa uelewa wako. Swali: Je wanakupesheka hao wakopaji? Kumbuka riba imepanda kwa mikopo ya kawaida kwa zaidi ya asilimia 4.
Central bank walipunguza discount rate kutoka 16 % to 12%. Unavyosema imeongezeka imekuwaje hapo?
 
Hizi hesabu za uchumi ni ngumu kuzielewa.Kipato chetu tulio wengi ni kile cha July 2015. Gharama ya Bidha zote za viwandani na chakula zimeongezeka kwa karibu 50%. Maana yake kuna uwezekano tukapata kizazi chenye afya duni na utapiamulo kutokana na wengi kushindwa kumudu gharama za chakula na tiba.

Lakini eti uchumi umekua.Hii inafanana na baba wa familia aliye waachisha watoto shule kisha kuwashindisha njaa nyumbani kisa pesa yote amenunulia gari:Ambapo mtaani majirani wanamsifu kuwa ameendelea kwakuwa kanunua gari
 
Central bank walipunguza discount rate kutoka 16 % to 12%. Unavyosema imeongezeka imekuwaje hapo?
NAzungumzia wakopaji wadogo wadogo hasa waajiriwa..sio business loan ambayo huwa determined na muda wa mkopo. Hizo hata discount zilizowekwa hazija effect changes
 
hawajapunguza discount rate, walichopunguza ni reserve requirement rate.
ded0d7faf2038e4e2b8d22b8ce3843c6.jpg

Nadhani hukuliona hili tangazo la tar 3/3. Kwa mantiki hiyo pia tunategemea interest rate kushuka kwa kiasi fulani combined with effect ya minimum reserve requirement pesa inaweza kuongezeka mtaani
 
yeah mkuu sikuiona hii, ila hata hiyo 12% for discount rate is still high. kwa average inflation ya 5% basi hiyo discount rate wangeifanya 9%-10% ili na commercial banks nao wapunguze interest rate zao zifikie walau 14%-15% . maana saiv loan is too expensive 20%-23%.
 
Hapa kazi tu. Uchumi umekua sana. Huku tunanunua kilo 1 ya sukar 3000 mpaka ifike 2020 tutanunus kwa 10,000 hii bei ni kwa wapinzani. Ccm wao huwa wananunua kwa 1800 tu. Ukienda duka lolote kununua sukari ww onesha kadi yako tu ya ccmu. Utapata kwa 1800
Anayesubiria nchi ya viwanda ni mwendawazimu na kiziwi. Siyo kwa uongoz wa ccm. Mtasubiri sana hivyo viwanda. Ccm ndiyo kawaida yao kuwadanganya watu,
Mtasubir viwanda mpaka miguu ingie tumbon. Viwanda ni kelele za wajinga tu.
Sukari 3000 sasa ukija kutahamaki 5000 kilo 1 na bado unaimba hapa kazi tu na nchi ya viwanda
Povu la Komoni.
 
Je na changamoto ya vifungashio inachangia pamoja na wafanyabiashara kupewa elimu juu ya kuipa thamani bidhaa ili zikidhi viwango husika.
 
yeah mkuu sikuiona hii, ila hata hiyo 12% for discount rate is still high. kwa average inflation ya 5% basi hiyo discount rate wangeifanya 9%-10% ili na commercial banks nao wapunguze interest rate zao zifikie walau 14%-15% . maana saiv loan is too expensive 20%-23%.
Exact mkuu. Nominal interest rates kwa developing countries ni kubwa nno. Kwa sasa kwenye formal banks tuna borrow kwa hizo percent ulizozitaja sasa hiyo ni cost ya kitu kimoja tu (capital) kwa maana hiyo price utakayoset baada ya uzalishaji ni lazima ikave iyo 20-22 pc so at the end biashara inakuwa ngumu sana. Pia kitu kinachotuathiri sana ni jinsi banks zetu zinavyofanya business kuna namna inawezekana wanakaa na kupanga rates ili ushindani wao usishushe sana rates ndo mana rates zao zinaendana sana, hili ni kosa na China wameshawapiga penalty kubwa sana benki zinazofanya iyo michezo ila kwetu huku bado mambo kama hayo hatuyajui. Anyway rates zitaweza kushuka kwa kiasi fulani kutokana na combination ya hizo initiatives BoT walizozifanya
 
Kwaiyo rate mpya itaanza kutumika lini kwa commercial bank na wale walikopa kabla punguzo ya rate itakuwaje?
 
Kwaiyo rate mpya itaanza kutumika lini kwa commercial bank na wale walikopa kabla punguzo ya rate itakuwaje?
Sijafahamu imekaaje ( km ni kibiashara yaani forces za demand na supply au imekaa kisheria zaid yaan km BoT inaweza kuforce bank kupunguza rates ila so far theoretically kuna mechanism inaitwa moral sassuation (km cjakosea spelling) ila kinachofanyika ni kwamba benki kuu inazishawishi commercial banks either kuongeza au kupunguza rate ila kuaffect economy pale ambapo njia za kisheria zimekwama)
 
Nimekuelewa sana mkuu ila it seems atakama BOT wamepunguza rate kupelekea commercial bank wapunguze rate kwa wananchi lakini kwa kiwango kidogo sana,je wangepunguza atleast 9-10% ili commercial banks wasiweke rate kubwa kiuchumi ingeleta hasara au faida?
 
Back
Top Bottom