Uchumi wa nchi unakua- Gavana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi wa nchi unakua- Gavana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, May 28, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wadau,
  Matunda ya serikali yetu sikivu hayo, hili ni jambo la kitaalamu msiweke siasa. tuipongeze serikali sikivu.


  Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, amesema uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa asilimia 6.4 kwa mwaka 2011 zaidi ya ilivyokadiriwa kuwa ungekua kwa asilimia 6 kwa mwaka.
  Alisema ukuaji huu ni mkubwa hasa katika sekta ya usafirishaji na mawasiliano kwa asilimia 11.3 ikifuatiwa na masuala ya fedha kwa asilimia 10.7, ujenzi kwa aslimia 9.0, biashara kwa asilimia 8.1 na uzalishaji wa asilimia 7.8.
  Akitoa mada katika mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya inayofanyika mjini Dodoma, Profesa Ndullu alisema mpaka hivi sasa Tanzania bado inakopesheka kinyume na taarifa mbali mbali zisizo rasmi zinazotolewa.


  Profesa Ndulu alisema kilimo bado kinaongoza katika kuliingizia Taifa mapato kikifuatiwa na biashara uzalishaji na ujenzi.
  Aidha, aliishauri Hifadhi ya Taifa ya Chakula (National Grain Reserve) kuanza kuwa na mkakati wa kuhifadhi mpunga badala ya mahindi pekee kwani itasaidia kupunguza mfumuko wa bei kwa kuwa mchele ni moja ya nafaka inayotumiwa sana na kaya mbalimbali.
  Profesa Ndullu alisema kwa ujumla kushuka kwa thamani ya fedha kumepungua kutoka asilimia 19.7 hadi kufikia 19.0 katika mwaka 2002.
  Alieleza kuwa kushuka kwa thamani ya fedha ilitokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hasa katika eneo la nishati na mafuta.


  Alisema hadi kufikia hivi sasa asilimia 75 ya Watanzania wanategemea kilimo, hivyo ili Tanzania iweze kupiga hatua katika maendeleo, kilimo kimetakiwa kutiliwa mkazo mkubwa.
  Naye Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango Dk Phillip Mpango, aliwataka viongozi kuongoza kwa mifano na kuondokana na suala la kuongoza kwa nadharia ili kujua changamoto zinazowapata wale wanaowaongoza.


  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Baba Ndulika is another bozzo we got to get rid off, kwanza hajui hata ku-update information huyu kweli hataweza kuja na mbinu za ku-manipulate our economy no wonder we are in this situation. Hivi huyu JK huwa ana waokotea wapi hawa ma-Professor uchwara.
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  unamwamini?
   
 4. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  yani huyu mu baba ataanakotoka kwao kwa baba na mama yake hakuna umeme tu sijui umekuaje, tabu sana siasa ndani ya ukweli........
   
 5. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,639
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Bila shaka Shibuda ni mmoja wa wahudhuriaji wa hiyo semina
   
 6. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is a very high risk, for the Central Bank to manipulate our economic grow.
  The growth of prospects of Tanzania economic may have been slowed, to zero
  growth. Let say our econmic are still in the recovery mode, the goverment
  practice always destined to failure. They do not understand the machinery that
  is the national economy and how to make it work and grow. But for the other
  mean the economy is flat.
   
Loading...