Uchumi wa Afrika kuporomoka

Uchumi wa Afrika kuporomoka

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Uchumi wa Afrika kuporomoka

Benki ya dunia imesema uchumi wa bara la Afrika,Kusini mwa jangwa la Sahara utaporomoka kwa kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu miaka 25 iliyopita,kutokana na virusi vya Corona

Mripuko wa virusi vya Corona unaozidi kusambaa unatarajiwa kuzisukuma nchi za Afrika,Kusini mwa Jangwa la sahara katika mporomoko wa kiuchumi katika mwaka huu 2020 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25. Huo ni utabiri uliotolewa na benki ya dunia.

Ripoti ya benki ya dunia kuhusu hali ya kiuchumi barani Afrika imesema kwamba uchumi wa bara hilo utashuka asilimia 2.1 na kufikia asilimia 5.1 kutoka kiwango cha ukuaji cha mwaka jana cha asilimia 2.4.

Aidha mripuko huu wa virusi vya Corona utazigharimu nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika dola bilioni 37 hadi dolla bilioni 79 ambayo ni hasara itakayoonekana mwaka huu kufuatia kuvurugwa kwa shughuli nyingi za kibiashara na kiuchumi miongoni mwa sababu nyinginezo.

Hali ilivyo barani Afrika

Bara la Afrika lina alau visa 10,956 vya watu waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, vifo 562 na waliopona wakiwa ni 1,149 kwa mujibu wa mahesabu yaliyofanywa na shirika la habari la Reuters kwa kuzingatia taarifa zilizokwishatolewa na serikali na data za shirika la afya duniani WHO.

Makamu mwenyekiti wa benki ya dunia kwa ajili ya Afrika Hafez Ghanem amesema janga la ugonjwa wa Covid-19 linapima uwezo wa mwisho wa jamii na nchi zote ulimwenguni na kuna uwezekano hususan kwa nchi za Afrika kuathirika zaidi.

Jitihada za utoaji wa fedha za dharura

Benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa IMF zinakwenda mbio kutoa fedha za dharura kwa nchi za Afrika na nyinginezo kukabiliana na virusi vya Corona ili kupunguza athari zitakazosababishwa na hatua za kufungwa kwa shughuli za kimaisha zinazochukuliwa nchi mbali mbali ulimwenguni kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo vya Corona.

Ikumbukwe kwamba janga la virusi vya Corona limesababisha kufutwa kwa safari za kimataifa katika nchi nyingi za bara hilo la Afrika hali ambayo imeathiri kwa kiwango kikubwa sana sekta mbali mbali kama vile sekta ya utalii.
Serikali mbali mbali za bara hilo la Afrika zimetangaza hatua ya kufunga miji au nchi kwa maana ya kwamba hakuna shughuli za kawaida za kimaisha haziruhusiwi tena kufanyika au baadhi ya nchi zimetangaza kuzuia watu kutoka nje,hizi zikiwa ni hatua zinazodhamiriwa kupunguza kusambaa kwa virusi vya Corona ambavyo kwa hakika vimechelewa kuingia Afrika lakini sasa vinasambaa kwa kasi kubwa barani humo kwa mujibu wa W.H.O.

Kutokana na hali hii benki ya dunia inasema ukuaji wa pato la ndani utapungua kwa kiwango kikubwa na hasa katika nchi tatu zenye uchumi mkubwa katika bara hilo,Nigeria,Angola na Afrika Kusini. Kadhalika nchi zinazouza mafuta pia zitaathirika sana.
 
Sasa ndio tutalilia fedha tulizotumia kununulia ndege ambazo zimekuwa grounded.

Hatuna focus na wala hatujui vipa umbele vyetu ni vipi, hii ndio shida ya kukosa katiba inayo-guarantee checks and balances kwa mihimili ya nchi. Tutasota sana huko mbele.
 
Hiki ndio kipindi cha mabeberu kutunusanusa makalio yetu halafu sisi tunabaki tunachekacheka huku tukiwasifu kwa nyimbo na mapambio kua wao ndio wadau wa maendeleo.
......kunuswa tena...🙄🙄🙄....
Hizi comments nyingine balaa.
 
As a nation tunasababu kusali zaid kutokana na anguko la uchumi dunian limeukuta uchumi wetu ukiwa na mzigo mzito wakujenga miundo mbinu tukitegemea cash ya ndani which means our budget is cash budget jambo nilahatari zaidi. Sina uhakika kama tuna reserve yakutosha kwasababu tulikuwa tuna tumia 😋 zote kwenye ujenz wa miundo mbinu. Sitaki kulaumu japo kama taifa kuna darasa tunalipata kuwa upo uwezekano serikali ikashindwa mzigo mzito wa maden ya wafanyakaz hivyo ikapunguza watu jambo lita affect pia sector binafsi kama ma bank why? Zaid ya nusu ya budget serikal inalipa mishahara kila mwez na inategemea kodi ili ilipe mshahara as i write kodi kwa mwez wa nne nkuendelea uwenda ikashuka sasa kwakuwawe base on cash budget je pesa watatowa wapi? Let pray for nation
 
Sasa ndio tutalilia fedha tulizotumia kununulia ndege ambazo zimekuwa grounded.

Hatuna focus na wala hatujui vipa umbele vyetu ni vipi, hii ndio shida ya kukosa katiba inayo-guarantee checks and balances kwa mihimili ya nchi. Tutasota sana huko mbele.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] UNANUA BMW, UNASAHAU KUKARABATI PAA LA NYUMBA YAKO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ndio tutalilia fedha tulizotumia kununulia ndege ambazo zimekuwa grounded.

Hatuna focus na wala hatujui vipa umbele vyetu ni vipi, hii ndio shida ya kukosa katiba inayo-guarantee checks and balances kwa mihimili ya nchi. Tutasota sana huko mbele.
We kidampa kwahiyo nchi zote hizo zitakazoathiriwa zimenunua ndege?
 
[QUOTE="TumainiEl, post: 34951567, member: 20912"
Zaid ya nusu ya budget serikal inalipa mishahara kila mwez na inategemea kodi ili ilipe mshahara as i write kodi kwa mwez wa nne nkuendelea uwenda ikashuka sasa kwakuwawe base on cash budget je pesa watatowa wapi? Let pray for nation
[/QUOTE]
Wataprint nyingine. Usjali
 
Hiki ndio kipindi cha mabeberu kutunusanusa makalio yetu halafu sisi tunabaki tunachekacheka huku tukiwasifu kwa nyimbo na mapambio kua wao ndio wadau wa maendeleo.
Sisi ndio muda wetu wa kuwachapa vibao vya matako! Mchina ni jamaa yetu tumtumie kupiga hela maana huko ulaya washapoteana.
 
[QUOTE="TumainiEl, post: 34951567, member: 20912"
Zaid ya nusu ya budget serikal inalipa mishahara kila mwez na inategemea kodi ili ilipe mshahara as i write kodi kwa mwez wa nne nkuendelea uwenda ikashuka sasa kwakuwawe base on cash budget je pesa watatowa wapi? Let pray for nation
Wataprint nyingine. Usjali
[/QUOTE]
hi unajuwa hathar za ku print money? nadhani hujanielewa niliposema tusal
 
Tusiwasikilize hao, tuwasikilize viongozi wetu.

Wao wanavyoweka lockdown wanategemea nini? sisi hatuweki lockdown na tutaunusuru uchumi wetu.
 
Tajiri anamjua zaidi masikini kuliko masikini anavyomjua tajiri
Wanajua fika kuwa simu zimezidi kwa kuombwa hela na wanajua kinachoendelea
Huu ni wakati wa kusitisha miradi mikubwa inayokula hela na kujiwekea akiba
Kama Coronavirus haitatutandika njaa itatumaliza na wa kuwaomba ndio hao saccos
Tutasaini mikataba ya masharti ambayo ni mabaya zaidi ya yale tuliyoyakataa na kila mmoja wao tutamsifia kwa kuokoa jahazi



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
We kidampa kwahiyo nchi zote hizo zitakazoathiriwa zimenunua ndege?
Kila moja aongelee ya kwake, ukisema ninafanya kosa kisa na wengine nao wanafanya ni utaahira tu huo.
 
Hiki ndio kipindi cha mabeberu kutunusanusa makalio yetu halafu sisi tunabaki tunachekacheka huku tukiwasifu kwa nyimbo na mapambio kua wao ndio wadau wa maendeleo.
Beberu ananusa kikojoleo halafu anabinua midomo kuelekea juu kama ishara ya kumshukuru mungu.
 
Tajiri anamjua zaidi masikini kuliko masikini anavyomjua tajiri
Wanajua fika kuwa simu zimezidi kwa kuombwa hela na wanajua kinachoendelea
Huu ni wakati wa kusitisha miradi mikubwa inayokula hela na kujiwekea akiba
Kama Coronavirus haitatutandika njaa itatumaliza na wa kuwaomba ndio hao saccos
Tutasaini mikataba ya masharti ambayo ni mabaya zaidi ya yale tuliyoyakataa na kila mmoja wao tutamsifia kwa kuokoa jahazi



Sent from my iPhone using Tapatalk
Hapo kwenye kusimamaisha miradi itakuwa ni ngumu maana hiyo miradi ndio ajenda ya kisiasa ya kuombea kura.
 
Hapo kwenye kusimamaisha miradi itakuwa ni ngumu maana hiyo miradi ndio ajenda ya kisiasa ya kuombea kura.

Basi tusubiri tu maana kama ni umasikini tumo ila tutakuwa zaidi
Hili janga linawapiga vibaya matajiri na sisi ni waombaji tu wa kusubiri kupewa
Sasa kama kuna kuwaza kura mda huu yatakuwa ni maajabu



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom