Uchumi unakua, wananchi hohehahe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi unakua, wananchi hohehahe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Jul 6, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  KAMA takwimu zinaweza kudanganya, kwa mujibu wa Profesa Yule, basi inawezekana kwa asilimia kubwa zimetumika kuwadanganya wananchi wa Tanzania juu ya kukua kwa uchumi ilhali hali ya kipato binafsi ni ya kutia mashaka!
  Hata kama takwimu halisi zinazotolewa na serikali juu ya maendeleo ya kukua kwa uchumi kuna kila sababu ya kudhani kwamba, “takwimu za kiuchumi zinazotolewa hazikuzingatia hali halisi ya upimaji wa kina juu ya maendeleo ya vitu kwa manufaa ya watu.”
  Kama dhana, uchumi ni kuchuma! Ni chumo la watu pale wanapotumia mali ya asili na au rasilimali adimu kwenye mchakato wa kuzalisha ili kwa chumo (kipato cha kiuchumi) waweze kukidhi haja zao za kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa uwiano unaozingatia ugavi na utashi.
  Binadamu, kama kiumbe, ana mahitaji yake muhimu ambayo hukidhiwa kwa shughuli na au harakati za kiuchumi zinazowezesha upatikanaji wa mahitaji ya binadamu kama vile chakula, mavazi, nyumba, huduma za kijamii, ulinzi na usalama sawia.
  Uchumi ni sayansi ya matumizi makini na endelevu ya rasilimali. Kama nchi, Tanzania yenye mali ya asili na rasilimali zinazotosha kwa maendeleo ya watu, ni masikini japokuwa takwimu zinaonyesha uchumi unakua!
  Cha kustaajabisha ni hali ya viongozi wa kisiasa wa chama tawala na serikali yake kupigia mistari ukuaji wa uchumi unaokua pasipo kuweka mizania ya uhuru, haki na usawa baina ya hali hali ya kiuchumi inayowakabili wananchi wengi wa Tanzania.
  Ka ujumla, hali ya wananchi wengi wa Tanzania ni tete na yenye kutia simanzi kwa jinsi yake. Uchumi wa wananchi unaozaa kipato binafsi kwa sehemu kubwa ya wananchi unategemea harakati za kubangaiza kwenye sekta isiyo rasmi na inayotambuliwa kama uti wa mgongo, yaani, kilimo!
  Ni kweli kwamba kilimo, kama harakati muhimu ya uchumi katika Tanzania, inachukua takriban asilimia 75 ya wananchi hususan vijijini na maeneo yanayozunguka miji. Sehemu ndogo sana ya wananchi ndiyo wamebahatika kuwa kwenye sekta rasmi ya uchumi, kama vile ajira rasmi kwenye sekta ya umma au sekta binafsi.
  Ukweli wa kiuchunguzi (kisayansi) pamoja na mantiki yake unaifanya Tanzania kuwa nchi ya kilimo (agrarian). Na kwa jinsi yoyote ile, kilimo kitaendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa wananchi kwa kuwa ndiyo njia pekee inayowawezesha wananchi wengi kumiliki rasimali yao, yaani nguvu kazi.
  Kwa jinsi yoyote iwayo, na hii ni kweli na hakika tangu tulipopata uhuru miaka hamsini iliyopita, kwamba kilimo kilitangazwa kuwa, “ndiyo baba; ndiyo mama – kilimo ni kufa na kupona”! Pamoja na ukweli wote huu kilimo na wakulima (ambayo ndiyo sekta nyeti inayochukuwa sehemu kubwa ya nguvukazi ya Tanzania) imetelekezwa na kusahaulika kabisa!
  Serikali, pamoja na jitihada na au juhudi za hapa na pale katika kuboresha mazingira ya kilimo, bado inasuasua kwenye kuunda sera zisizokuwa na mikakati sahihi na makini ya kuleta tija na ufanisi kwenye maendeleo ya sekta ya kilimo, hususan kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao.
  Serikali imekosa uoni sahihi na wenye ubunifu angavu katika kuifanya sekta ya kilimo kuleta tija kwa wananchi na hatimaye kuinua uchumi jumla wa jamii na taifa sawiya. Kilimo kimekuwa sehemu ya uwekezaji usiyozingatia hali halisi, mazingira na wananchi.
  Kama kilimo hakina tija kwa wananchi waliyo wengi waishio vijijini ambako ndiko kwenye sehemu kubwa ya nguvukazi; matokeo yake ni kwa nguvukazi hiyo kutokutumika vema; na hata ile nguvukazi inayotumika inakosa muelekeo wa tija na maslahi ya kiuchumi na hatimaye uzalishaji hushuka na kusababisha kupungua kwa kipato binafsi na cha taifa (pato la taifa kwenye kilimo). Hakuna asiyefahamu kwamba wananchi wengi wa Tanzania hawana umiliki wa rasilimali isipokuwa nguvukazi yao isiyotumika. Kwa kuwa rasilimali watu (nguvukazi) ya wananchi wengi wa vijijini haitumiki kwenye kilimo; na kwa kuwa wengi wao wamekata tamaa ya kushiriki kwenye kilimo kilichotelekezwa cha jembe la mkono; na kwa kuwa kilimo cha jembe la mkono ni kazi ya harubu (ngumu na inayotumia nguvu nyingi); wananchi wengi wa vijijini wameacha kulima!
   
 2. Mazee

  Mazee Senior Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 6, 2007
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nafikiri labda mtu wa uchumi atusaidie hapa kwenye
  kwani ripoti zinasema inflation imekuwa kwa zaidi ya asilimia 12 sasa wakati in 2000 ilikwenda below 5 percent
  na uchumi unakuwa kwa asilimia saba recently sasas sijui hii inmaanisha nini
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hawa watakuwa wanapigia ukuaji wa uchumi wa mwezi na sio kwa mwaka kwa hiyo lazima iwe tofauti kwa mfano bei ya nyama mwezi wa 5 ilikuwa 4000 na mwezi 6 ilikuwa 4500 kwa mwa huu ukilinganisha na mwaka jana ambapo ilikuwa kati ya 3000 mpaka 4000 mbayo imeongezeka kwa 1000 kwa hiyo inflaton na price change ziwetofauti..
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wananchi wanaolima, kwa wale walioamua kufa na kilimo, wanafanya hivyo kwa jinsi ya kukidhi haja ya kupata chakula kwa minajili ya kubangaizabangaiza katika kuondokana na "adui njaa". Pamoja na hali ya mabadiliko ya tabia nchi, wengi wa wakulima wa vijijini wamechoka kulima kilimo kisichokuwa na tija.
  Huo ni upande wa wakulima na wananchi waishio vijijini na maeneo yanayozunguka mijini ambao kwa sehemu kubwa wanakitazama kilimo kama sekta iliyotelekezwa na hakika ndiyo chanzo cha kushuka ari ya uzalishaji mashambani.
  Upande wa pili wa mtazamo juu ya madai ya kukua kwa uchumi ni hali ya wafanyakazi kwenye sekta ya umma. Huku nako kuna hali mbaya na isiyoelezeka kwa urahisi kwa kuwa wafanyakazi wengi wanaishi maisha msoto na yenye msongo wa kiuchumi na kijamii. Kwa ujumla, hali ya uchumi wa wafanyakazi ni mbaya!
  Upo mtazamo wa kibepari na kibwanyenye kwamba wafanyakazi, hususan wa sekta ya umma hawazalishi bidhaa na ndiyo maana hawawezi kupimwa kwa jinsi ya kulipwa stahili na au stahiki kwa kigezo cha kuzalisha.
  Inafahamika na wote (wafanyakazi) wanafahamu kwamba uzalishaji ni wa aina mbili: kuzalisha bidhaa za viwandani; na kuzalisha huduma mbalimbali. Hali hii inaweza kuonekana kwa urahisi zaidi kama tutatumia mifano ya sekta ya umma na ile ya binafsi kama kielelezo.
  Mifano yote kwa jinsi yake inatosha kuonyesha juu ya utofauti wa ufahamu wa dhana ya uzalishaji wa kiuchumi na ukokotozi wa malipo kutokana na ushiriki wa wafanyakazi katika uzalishaji wa bindaa na huduma kadhalika.
  Wafanyakazi wa sekta ya umma, kwa mfano walimu wa aina zote (shuleni na vyuoni), watendaji wa serikali (kuu na mitaa), watumishi wa taasisi za umma na ulinzi na usalama, pamoja na kada nyingine ndani na nje ya mfumo rasmi wa kazi za uendeshaji wa nchi ni wazalishaji wa huduma na kwa jinsi hiyo wanalipwa kwa mujibu wa ukokotozi wa uzalishaji wa huduma na hawawezi kupimwa kwa mtindo wa thamani ya bidhaa isipokuwa huduma wanayotoa kwa umma. Pamoja na ukweli huu, wengi wa watumishi hao – hususan wale wanaopota kima cha chini (KCC) cha mshahara, wana maisha magumu ya kiuchumi. Bajeti za wafanyakazi wa umma kwenye mabano ya KCC ni zile zinazotegemea zaidi mikopo
   
 5. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Usishangae sulphadoxine, wataalam wetu wa takwimu (statisticians)
  huwa wana kipimo chao cha kuangalia ukuaji wa uchumi kwa kuchukua
  pato la walionacho (wachache) na wasionacho (wengi) na kutafuta wastani,
  kwa kutumia mfumo wa "Head in the OVEN and legs in the FREEZER, the
  average is COMFORTABLE"!

  Yaani unamchukua mtu, kichwa unakiweka ndani ya tanuru (oven), halafu
  miguu yake ndani ya jokofu (freezer) kisha unatafuta wastani, ambapo
  inamaanisha kuwa kama kichwani anaungua basi miguuni anapoa hivyo
  wastani wake katikati ya mwili (kiuno na tumbo) yuko poa...

  Hii ndiyo Tanzania
   
 6. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Uchumi is a broad term. Nashauri utumie neno pato la taifa badala ya uchumi.
   
Loading...