Uchumi umekuwa Ila wapinzani ndio tatizo

Uchumi umekuwa Ila wapinzani ndio tatizo

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,735
Reaction score
167,778
Uchumi umekuwa Ila wapinzani wanaroga sana ili maisha yawe magumu.
>Wapinzani wameroga makinikia hatujalipwa hadi Leo.
>Wapinzani wameroga hadi wale jamaa waliokuwa wanaingiza milioni saba kwa dakika kwa kuibia TRA hawajulikani walioko
>Wapinzani wameroga hadi ndege yetu imekamatwa Canada
>Wapinzani waliroga hadi tukamtimua Yule mkandarasi wa ujenzi wa barabara kutoka Wazo Hill hadi Bagamoyo
>Wapinzani waliroga hadi TTCL ikaporwa kumiliki Celtel
>wapinzani waliroga hadi hostel za chuo kikuu zikapata nyufa
> Wapinzani waliroga mchakato wa katiba mpya
> Wapinzani waliroga Bomba la gesi ndio maana Kinyerezi Na kutumia gharama kubwa kujengwa lakini mradi unafanya kazi kwa kiwango cha asilimia sita tu ya uwezo wake.
 
Hivi wapinzani wetu wazamani walikuwa wakoloni hivi sasa tumekuwa sisi wenyewe au wametokea sayari nyengine..?
 
Serikali Ya Kenya Imezindua Ndege Zake Mpya Aina Ya Boeing 787 Dramliner Zenye Uwezo Wa Kubeba Abiria 234 Kila Moja Ambazo Zitafanya Safari Za Moja Kwa Moja Kutoka Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Jomo Kenyata (JKIA) Nairobi Hadi Uwanja Wa Ndege Wa John Kenedy (JFK) New York, Marekani.

Tiketi Za Kawaida Zinauzwa Ksh. 89,000 ($890). Kenya Airways Itafanikisha Safari Hizo Kwa Ushirikiano Na Shirika La Delta Airlines La Marekani.

Mambo Muhimu Kuhusu Safari Hiyo:
Safari Hiyo Itachukua Saa 15 Kutoka New York Hadi Nairobi Na Saa 14 Kutoka Nairobi Hadi New York.

Kila Ndege Itakuwa Na Marubani 4 Na Wahudumu 12.

Safari Zote Zitafanywa Na Ndege Za Kisasa Aina Ya Boeing 787 Dreamliner Ambazo Hubeba Abiria 234 Kila Moja.

Ndege Za Kwenda Marekani Zitaondoka JKIA Nairobi Saa 23: 25 Na Kufika JFK New York Kesho Yake Saa 06: 25.

Ndege Za Kurudi Nairobi Zitaondoka New York Saa 12:25 Na Kutua JKIA Nairobi Saa 10:55 Kesho Yake.
 
Wapinzani wamemroga hadi baba Jesca amekuwa hataki kuhudhuria misibani
 
Wapinzani wameroga hadi vyerehani tunaita kiwanda.
 
wapinzani wana hulka ya kusifia vya nje lakini vikifanyika hapa ndio wa kwanza kuvipiga vita.
 
Wapinzani wameloga baba j anatekeleza agizo la Mungu 'zaeni mkaongezeke'
 
Yan Umeamua Kusema Kwa Mafumbo Ili Kumkwepa Siro (uchochez) Me Nimesreen Shoot Post Yako Naipeleka Kule Upigwe Faini , , , , , , , , ,
 
Mkuu kwa Uzi huu inabidi uanze safari ya Zimbabwe mapema kabla hawajakuita mchochezi.
 
Wapinzani wamemroga hadi rowasa anataka kurudi ccm,wapinzani wameroga hadi wameahindwa chaguzi zote

Wapinzani wameroga hadi madiwani wake na wabunge wanahamia ccm

Wapinzani wameroga hadi chakula kimejaa nchini

Wapinzani wameroga hadi ccm inatoa elimu Bure

Wapinzani wameroga mpaka mradi wa reli ya kisasa kutoka dar to Moro ujenzi umeanza

Wapinzani wameroga mpaka viroba na madawa ya kurevya yamefutika nchini

Wapinzan wameroga mpaka hali ya uchumi hasa uchumi wa viwanda umepaa

Wapinzani wameroga hadi mradi wa flyovers umemeanza

Upinzani umeroga hadi kila kata inajengwa zahanati
 
Wapinzani wamemroga hadi baba Jesca amekuwa hataki kuhudhuria misibani
Nawakubali sana Wapinzani. Wapo vizuri.
Chezea mpaka mtu anakataza watu wasiseme vyuma vimekaza. Siyo mchezo. Ngoja Lissu apone.
Napenda sana yawepo mazungumzo ya kiingereza tuone pogba anavyopoteana km moshi
 
Wapinzani wameroga hadi Accasia imepunguza wafanyakazi

Wapinzani wameroga hadi benki 5 zimefilisika na kufungwa hatimae walioweka mamilioni kuambulia 1.5m... sijui nao tuwaite wapiga dili? Maana wapiga dili nchi hii ndio wanaishi maisha magumu km shetani

Wapinzani wameroga hadi viwanda km tbl na konyagi vimepunguza wafanyakazi zaidi ya 100

Wapinzani wameroga hadi bei ya mbaazi imeshuka kilo sh 500
 
Wapinzani ndio WAPINGA KRISTO tena ndio wanasababisha cherahani nne zisiwe kiwanda
 
Wapinzani wamemroga hadi rowasa anataka kurudi ccm,wapinzani wameroga hadi wameahindwa chaguzi zote

Wapinzani wameroga hadi madiwani wake na wabunge wanahamia ccm

Wapinzani wameroga hadi chakula kimejaa nchini

Wapinzani wameroga hadi ccm inatoa elimu Bure

Wapinzani wameroga mpaka mradi wa reli ya kisasa kutoka dar to Moro ujenzi umeanza

Wapinzani wameroga mpaka viroba na madawa ya kurevya yamefutika nchini

Wapinzan wameroga mpaka hali ya uchumi hasa uchumi wa viwanda umepaa

Wapinzani wameroga hadi mradi wa flyovers umemeanza

Upinzani umeroga hadi kila kata inajengwa zahanati
Wapinzani wameroga hadi umeamua kujitoa ufahamu ,daa kweli uchumi upaa maana kwa sasa hakuna mtanzani mwenye maisha magumu.
dawa, maji , umeme ,elimu vyote viko safi kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom