Uchumba wa Mahesabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumba wa Mahesabu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Petu Hapa, Feb 1, 2012.

 1. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jana tulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo ya uchumba. Watu wazima walidai vigezo vya kuchagua wachumba vimebadilika sana siku hizi. Zamani, watu walikuwa wanaangalia sana tabia, uzuri, kabila, familia aliyotoka binti na mapenzi kwa ujumla wake. Mara nyingi, mwanaume ndie alikuwa mchaguaji, lakini, kinamama wakapinga wakasema "mwanamke ndio huchagua ama kuamua kwanza, wakadai, kama mwanamke hakutaki hutampata"

  Vijana wakadai, uzuri peke yake haulipi wala jina la familia kwa mazingira ya sasa – labda mwanzoni mnapotokeana. Bali, watu mpaka kuamua uchumba maswala ya kiuchumi yanapewa uzito sana siku hizi kwa pande zote mbili, huku maswala ya elimu na ajira ndio kama msingi wa mahusiano.

  Duh! ya kweli haya? Yaani mapenzi ya kudumu kuangaliwa kama kitengo cha uchumi?
   
 2. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,375
  Likes Received: 3,208
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi msichana akiwa na wowowo na rangi ya kunde anatosha mengine nitavumilia tuuuuu
   
 3. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ndio viwango hivyo! mapenzi yanaanza kwa kuona
   
Loading...