Uchumba hatarini kuvunjika!!!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Rafiki yangu SR yamemkuta yakumkuta. Alianza kuwasiliana kwa PM na mwanadada 'mmoja' humu JF. Mawasiliano yakanoga na kukolea kwelikweli. SR na mwanadada wa JF wakapanga kukutana mahali fulani kwa PM.Wakatajiana muda na sehemu ya kukutana hapo.Wakati huo kwa PM hizo hizo walishatongozana na kukubaliana. Kila mmoja alisita kumpa nambari ya simu mwingine.

Lakini walikubaliana kukutana sehemu 'maalum' kwa muda 'maalum'. SR alikuwa wa kwanza kufika na akaweka 'mazingira' tayari. Mara ngo! ngo! ngo! Kufungua anaingia mdada. Ni mchumba wa SR. Kila mmoja akaanza kumwagia mwenzake maswali mfululizo kama mvua. Nusura zipigwe na ngumi humo humo. Kila mmoja anamwona mwenzake si mwaminifu. Na uchumba wao uko mashakani. SR anaomba ushauri wenu waungwana. Karibuni!
 
Utakubalije kukutana na mtu hamjawahi hata kuongea kwa simu?! Mmoja anaweza kuwa kilaza ila sio wote wawili.
 
Watu wasiwe vilaza, ukikutana njemba mwenzako ndani ya chumba cha gesti utakimbilia wapi?
Ni kweli.Kuna matukio hata kufikirika hayafikiriki.Lakini hili ni la leo.Nami ndiye niliyekwenda kushuhudia na kuwatenganisha.
 
wazimu wangu ukinipanda hata nguo nitavua.....
Nalog off
 
Ni kweli.Kuna matukio hata kufikirika hayafikiriki.Lakini hili ni la leo.Nami ndiye niliyekwenda kushuhudia na kuwatenganisha.

Waambie waendelee tu. . .kama wamevutiana tena bila kujua they are meant to be.
 
Hapo ameshndwa kuamua mwenyewe?ye anawaza nin?
 

hawa wanapendana kweli huoni wametongozana tena hata bila kuonana na bado wakapendana, wana mapenzi ya kweli hata wakikimbiana watatongozana tena.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…