Uchukuaji wa sample Liganga utaisha lini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchukuaji wa sample Liganga utaisha lini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hakikwanza, Nov 7, 2011.

 1. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Nimetembelea eneo la madini ya chuma Liganga Mundindi Ludewa, Kunakampuni inacholonga miamba yenye madini na kuchukua sample sasa ni takribani miezi kadhaa imepita.Ninacho jiuliza muda wote huu wanachukua sample? Na ili upate sample unachukua mawe mengi namna hii? Hapa ni sawa na unachunguzwa kama unamalaria na mtu wa maabara anachukua damu lita moja kwa ajili ya uchunguzi, hivi mgonjwa si atakufa kama sio kuishiwa damu? Hii nchi siasa na uhuni kwenye madini sijui itaisha lini. Nawasilisha.
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu hizo c sample ndo uchimbaji wenyewe huo, hapo sample tu watakuwa wamechukua tani za kutosha na sample zinaweza chukuliwa hata miaka mitano,

  hii ndo bongo,shamba la bibi
   
 3. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 882
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Kwa mtu asiyeelewa atakimbilia kusema tunaibiwa madini, lakini ukweli ni kwamba sample huwa ni kubwa sana. Hasa kama unataka kuweka mradi mkubwa utaohitaji u-raise capital kupitia mabenki. Huwa inabidi utengenezee kitu kinaitwa "Bankable Feasability Study", ambayo huakikiwa na watu wengi, wakiwapo wataalamu wa mineralization - Assayers. Inabidi upeleke sample zako kwenye lab zaidi ya moja.

  Vile vile huwa inabidi uchimbe kina kirefu sana na kuchukua sample ili uweze kuelewa ore-body imekaa vipi. Namna hiyo ore body ilivyokaa itaamua kama utafanya open cast mining au underground mining. Pia itaamu ni kiwanda cha aina gani inapaswa kujengwa.
   
 4. V

  Vitalino mlelwa Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thats lil but unajua kwanini watu wanasema haya ni kwa kuwa wanaichi hawana imani na watendaji that's why hata unavo mhudumia mgonjwa ni lazma umweleze nini unataka kufanya na kwa muda gani na hatima. sasa wewe ukifika na kuanza kucholonga eti kwa madai ni vitu vya kitaramu unauhakika wanainchi wana huo uelewa.so we should be care hasa watu wanapokuwa wamepoteza imani kwa magamba kama hv sasa.unaweza kuitwa fisadi hata kama unania safi lakini ndani ya mfumo mbovu.
   
 5. N

  Nandoa Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hiyo ni kawaida sana kuchukua sample za kutosha kwaajili ya kuangalia ukubwa wa hiyo ore body, namna ilivyokaa ili uamue unaichimba vipi, etc hivyo kucholonga mawe na kuchukua sample nyingi ni jambo la kawaida katika utafiti wa kijiolojia.
   
Loading...