Uchu wa madaraka na ubinafsi unatukwamisha

MICHAEL SON

JF-Expert Member
Apr 17, 2020
458
536
Heshima kwenu WAKUU, Poleni na Hongereni kwa mchaka mchaka wa maisha.

Kume kuwa na wimbi kubwa la viongozi,,wenye nyadhifa kubwa kuacha nyadhifa zao na kugombea Nafasi ya UBUNGE kila unapofika uchaguzi Mkuu. Hasa wakuu wa Mikoa na wilaya.

Naam na ukiwasikiliza wengi wanajinasibu kua wanataka kutatua kero za Watanzania! Hebu fikiria kwa mfano Ndugu MRISHO Gambo, Alikua nia na pengine bado yupo mbioni kutangaza nia ya kugombea UBUNGE

Sasa kwa Nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa,,kuna kero ipi ambayo alishindwa kuitatua kwa kutumia resource na mamlaka yake,na angeweza kuitatua akiwa Mbunge? Nionavyo mimi yeye kama RC wa Arusha alikua na Nafasi kubwa zaidi ya kuwatumikia wana Arusha.

NCHI HII INAHITAJI WAZALENDO KWA NYAKATI ZOTE

Naam Hawa wanaotamani vyeo na madaraka ni sumu kwa Taifa hili.

Asalaam

Mwalimu wa Chemistry na Biology
 
Ubunge ni cheo kikubwa na unalipa zaidi kuliko ukuu wa mkoa sema tu umerahisishwa na huyu incompetent wenu.Mtu yoyete makini hutamani kugrow ni bahati mbaya tu Wana mwenyekiti incompetent.
 
Ubunge ni cheo kikubwa na unalipa zaidi kuliko ukuu wa mkoa sema tu umerahisishwa na huyu incompetent wenu.Mtu yoyete makini hutamani kugrow ni bahati mbaya tu Wana mwenyekiti incompetent
Mkuu kikatiba ipo Vipi nani mkubwa kati ya RC na MP. Vipi katika scope na boundary of management who is who?
 
Mkuu kikatiba ipo Vipi nani mkubwa kati ya RC na MP,,Vipi katika scope na boundary of management who is who?..
Kikatiba hao Ni viongozi wa mihimili miwili tofauti na katiba haijaeleza Nani mkubwa na Nani mdogo Ila katiba imeeleza namna wanavyopatikana.ila kwa mpunga Mbunge anapiga mlunga mkubwa while RC akiwa kwenye TGS
 
Heshima kwenu WAKUU, Poleni na Hongereni kwa mchaka mchaka wa maisha..

Kume kuwa na wimbi kubwa la viongozi,,wenye nyadhifa kubwa kuacha nyadhifa zao na kugombea Nafasi ya UBUNGE kila unapofika uchaguzi Mkuu. Hasa wakuu wa Mikoa na wilaya.

Naam na ukiwasikiliza wengi wanajinasibu kua wanataka kutatua kero za Watanzania! Hebu fikiria kwa mfano Ndugu MRISHO Gambo, Alikua nia na pengine bado yupo mbioni kutangaza nia ya kugombea UBUNGE

Sasa kwa Nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa,,kuna kero ipi ambayo alishindwa kuitatua kwa kutumia resource na mamlaka yake,na angeweza kuitatua akiwa Mbunge? Nionavyo mimi yeye kama RC wa Arusha alikua na Nafasi kubwa zaidi ya kuwatumikia wana Arusha.

NCHI HII INAHITAJI WAZALENDO KWA NYAKATI ZOTE

Naam Hawa wanaotamani vyeo na madaraka ni sumu kwa Taifa hili.

Asalaam

Mwalimu wa Chemistry na Biology
Ubunge Ingekuwa ni nafasi ya kujitolea tusingepata wafanyabiashara Bali wazalendo.
Mbunge hata kujenga tu choo hawezi ndo akuletee maendeleo
 
Back
Top Bottom