Uchovu wa mume kitandani wamponza

Uchovu wa mume kitandani wamponza

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,674
Reaction score
37,852
Uchovu wa Mume Kitandani Wamponza
4458502.jpg

Michelle ThomasMonday, May 10, 2010 6:56 AM
Mwanamke wa nchini Marekani ambaye hakuridhishwa na pafomansi ya mumewe kitandani anashikiliwa na polisi kwa kumjeruhi mumewe kwa mkasi.Michelle Thomas, 26, alikamatwa jumanne wiki iliyopita baada ya polisi kuitwa kwenye nyumba yao kwenye majira ya saa saba usiku.

Tukio hilo lilitokea Texas, Marekani wakati Michelle alipokasirishwa na uwezo mdogo ulioonyeshwa na mumewe kitandani siku hiyo.

Mume wa Michelle aliwaambia polisi kuwa Michelle alipatwa na hasira baada ya gemu la malavidavi kuisha bila ya Michelle kuridhishwa kimapenzi.

Alisema kuwa Michelle alichukua mkasi na kuutumia kumkatakata kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake.

Polisi walimkuta mume wa Michelle akiwa na majeraha makubwa kifuani, mkononi na miguuni.

Michelle amefunguliwa mashtaka ya kudhuru mwili kwa kutumia silaha hatari ingawa mumewe hakutaka kufungua kesi dhidi yake, liliripoti gazeti la Lufkin Daily News.

Michelle huenda akatupwa jela miaka 20 iwapo atapatikana na hatia.
 
Back
Top Bottom