Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,916
- 30,259
std7,Baada ya kufahamu udini umemlewesha huyo mzee nilianza kupuuza naandiko yake yenye sumu ya Udini kama sumu kuvu kwenye nafaka.
Ningekuwa naandika kuhusu Uislam (Dini).
Kitabu changu cha kwanza kisingechapwa mara nne kuanzia kilipotoka mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza wala kisingefanyiwa tafsiri ya Kiswahili ili kiwafikie wasomaji wengi.
Wala nisingekuwa mmoja kati ya waandishi 500 kutoka kila pembe ya dunia walioandika Dictionary of African Biography (DAB).
Wala nisingealikwa vyuoni ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kuzungumza.
Nimeandika historia ambayo haikuwako kwa miaka mingi na ilipofahamika ndiyo hamasa hii ikatokea ya watu kutaka kupata elimu mpya katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mimi ni mmoja katika waliohojiwa kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere katika kitabu hicho hapo chini.
Maktaba yangu imeandikwa ndani ya kitabu hicho ni kati ya maktaba tatu zenye historia kubwa ya Mwalimu: Maktaba ya Dr. Salim Ahmed, Mohamed Said na Brg. General Hashim Mbita.
Ningekuwa naandika dini nisingekuwa na nafasi katika kuandika historia ya Julius Nyerere na harakati za kupigania uhuru.
Angalia picha hizo hapo chini: