winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 408
- 638
Mgodi ambao unatema kila siku.
Mgodi ambao wenyeje wanaachwa na maandaki bila kubaki na chochote. Mgodi ambao wajinga ndio wanaofanyishwa kazi na werevu wanahepa na dhahabu za kunufaisha Taifa lao.
Leo hii kandarasi na zabuni zote zinazotoka zenye "pesa ndefu" wote wanaoshiriki ni wachina peke yao na sisi kupitia viongozi wetu tunafurahi na kujipongeza kwamba tunailetea Tanzania maendeleo.
MIRADI MIKUBWA YOTE YA BARABARA inatekelezwa na wachina. YOTE! Je, ni kweli kwamba sisi ni wajinga sana na hatuna utalaamu wa kufanikisha hii miradi au ni mfumo wetu umejikita zaidi kujivua wajibu wa MZAWA KWANZA MGENI BAADAE?
Tumefika mahali tunaitukuza sana China kwamba bila yenyewe tusingekuwa hapa tulipo! Aibu kwetu kwa kuwa wazembe na wajinga miaka nenda rudi karne hadi karne.
Wizara zinazochukua bajeti kubwa ya Taifa ni pamoja na wizara ya ujenzi na uchukuzi lakini wabunge wetu watakaa pale bungune kujadili Ph.D. za kupewa na kutokupewa wakimaliza wataondoka. Wataacha kabisa kuangazia vipa umebele vya nchi ili pesa tunayokopa ibaki ndani na ikiwezekana tuwawezeshe watanzania kuwekeza nchi za nje.
Tatizo sio Katiba, tatizo ni uvivu wetu Watanzania maana asilimia 100% ya viongozi wetu ni Watanzania na hivyo wanatuwakilisha tuliowengi wazembe na wavivu.
Hivi tukishajenga hizi barabara baada ya hapo zinatusaidia nini kama hatuna uwezo wa kuzitumia kukuza kipato cha ndani? Pesa zote na maarifa yanaelekea China. Fanyeni tafiti wachina wote wanaokuja kufanya kazi nchini Tanzania ni wanafunzi na wakija wakishapata uzoefu wanapelekwa nchi zinazojitambua kufanya kazi kwa bidiii.
Damn it!