habari zenu wana jamwi,
mimi ni mchimbaji mdogo ninayechimba dhahabu katika mkoa wa Geita, nimefanikiwa kupata vitalu sita (6) vya uchimbaji wa dhahabu vyenye ukubwa wa jumla ya heka 147.
nimepungukiwa vifaa vya uchimbaji ambavyo ni
1. excavator
2. bulldozer
3.air compressor( for blasting)
4. waterpump
vifaa vingine vya sehemu ya kuchenjulia dhahabu ninavyo,
hivyo basi nahitaji mtu au kampuni ambayo nitaingia nayo ubia wa kufanya kazi pamoja.
Ndugu wana jf kwa yeyote ambaye ana vifaa hivi au anaweza kuvipata vifaa hivi, tuwasiliane.
NB: Documents za uthibitisho nitaweza kuziweka wazi kwa yule atakayekuwa na utayari wa kufanya kazi na mimi. na tutaweka mkataba wa kisheria kuhakikisha usalama wa uwekezaji wake.
Kwenye biashara ya bia mwenye empty crate, viti na meza tayari anayo bar, ukae ukilijuwa hili.
Hivyo basi kwenye mambo ya madini mtu mwenye hivyo vifaa ni zaidi ya huo mgodi wako.
Sijui kama unanielewa.
Rostam Aziz hajawekeza kwenye migodi bali amewekeza kwenye equipment za migodini na yeye ndio mkodishaji mkubwa wa vifaa hivyo migodini kupitia kampuni lake la Caspian.
Ushauri wangu ni kwamba tafuta wawekezaji wa kuwauzia hiyo migodi wafanye kazi.
Nawachukia sana watu wa aina yako ni kero kubwa sana Tanzania kila sehemu mnaleta kiwingu kuziba fursa kwa watu wenye uwezo wa kufanya mambo kwa tamaa zenu ya cha juu.
Hilo ndilo limetokea hadi kwenye viwanja, mtu anahodhi viwanja kujenga hawezi unatuwekea mapori na nyoka tu.
Wazembe na wasiokuwa na akili watakupongeza kwa kukuona una akili kumbe ni matope tu.
By the way hayo maeneo utakuja kunyang'anywa na serikali kwa sababu utashindwa kulipia leseni ya Primary minning licence. Utashindwa kulipia kwa sababu hakuna utakachopata hapo.
Nikupe tip tu ili uelewe, Escaveta moja kwa masaa 8 linakodishwa kwa laki 8 na opareta unalimpa elfu 50 kwa hayo masaa, diesel lita 200 na usafiri wa kulileta site na siku ya kurirudisha lilipotoka ni juu yako pia.
Sasa hapa jibu unalo, hayo mashamba uliuziwa bei gani? Ambayo leo unayaita migodi.