Uchimbaji Uranium na kizungumkuti cha uzalishaji Umeme

SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Lile jinamizi la mikataba feki hapa Tanzania inaonekana halitakaaliishe, kutokana na ubabaishaji unaosababishwa na serikali legelege. Pamoja na serikali kukaa kimya kuhusu uchimbaji wa madini ya Uranium hapa nchini kuna taarifa kwamba madini haya yalianza kuchimbwa hapa miaka mingi, lilikuwa ni deal la wakubwa hadi leo hawajatosheka na ufisadi huo. Madini haya ambayo yanauwezo wa kuzalisha umeme na tukaondokana na mgao unaolikabili taifa lakini serikali haijachukua hatua madhubuti kuhakikisha umeme unapatikana kutokana na Uranium. Tumesikia kwamba eti mpaka baada ya miaka 15 ijayo ndipo umeme utaanza kupatikana kutokana na Uranium. Swali lakujiuliza hivi kweli tukae miaka yote hiyo bila umeme, wakubwa wao wanaendelea kuiba madini yetu!. Kwanza tangu wameanza kuchimba hayo madini nchini tumefaidikaje, ni kitu gani cha maana cha kujivunia tulichonacho hivi sasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom