Wana masikio lakini hawasikii, wana macho lakini hawaoni, wana pua lakini hawanusi wana mikono lakini hawapapasi. Asante leo nimeuona uchi wa mbuzi live
Hiki ndio nilimaanisha... Nimeandika fasihi kutokana na mapokeo.. Ni kama nilivyoulezea uchi wa mbuzi.. Ule ni uumbaji lakini sisi tukaupa tafsiri zetu... Wewe kwenye ishu ya mbuni ulitaka kupinga kuwa sio kweli na ukaweka na ithibati... Jambo ambalo ni sahihi lakini sio muktadha wa mada! Unajua ni kwanini mpaka wazungu wakaja na utafiti!? Ni kwamba hilo jambo lipo... Lakini je ni kweli mbuni akiingiza kichwa chake ardhini anajificha!? Hii ni tafsiri ya binadamu, je kama hapo alipoingiza ni tunduni na anatafuta chakula!?
Nimachojaribu kufanya ni kukufunulia muktadha wa mada sio kupingana na tafiti zako labda kama uwe hujaelewa msingi wa hii mada katika ujumla wake