Uchi wa mbuzi

Uchi wa mbuzi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,903
Reaction score
828,514
Kwa wale tunaoamini katika matendo makuu ya Mungu hatuwezi kuhoji uumbaji wake yeye pekee ndio anajua kwa hakika kwa hapa alifanya hivi na pale vile Mungu hahusiki na tafsiri za kibinadamu taratibu zake, njia zake hazifanani na za binadamu matendo yake si ya binadamu mtu akikwambia anataka akifika mbinguni awe tena kiongozi lichukulie hilo neno kwa tafakuri kuu kwamba huyu maisha yake yote yaliyosalia hapa duniani atabaki hapo alipo ili akifa aunganishe Mungu turehemu sana

Sijui neno uchi wa mbuzi asili yake ni wapi lakini maumbile ya mnyama mbuzi yanaweza kuwa ndio sababu uchi ni utupu kondoo kajaaliwa kuficha wake hata kuku pia na wengineo kuna tafsiri ya haya mambo katika maisha yetu kwamba mambo yetu binafsi ama siri zetu zimegawanyika katika makundi ya uchi wa mbuzi uchi wa kondoo uchi wa kuku nk .

Kuna mnyama ndege anaitwa mbuni ana nguvu nyingi ana mbio ni mjanja ana akili lakini sio makini wala sio mwerevu mbuni akishazika ardhini kichwa chake kidogo chenye macho makubwa anadhani keshajificha na mwili wake wote na ya kwamba haonekani na wengine hizi ndio akili za mbuni.

Kuna kitu kimeweza kuandikwa na mitandao ya kijamii tuu vyombo vingine vya habari vilishindwa kabisa kuandika wanajua wazi wangeishia wapi unajua mitandao ya kijamii ni sawa tu na uchi wa mbuzi huku vyombo vingine vya habari vikiwa havina tofauti na uchi wa kondoo na wahusika(wanaotengeneza headlines) wakiwa kama mbuni
Kuna jina kadiri siku zinavyozidi kusonga itakuwa ni uhaini kulitamka mwambi kimangwe cha bei kubwa alikuja na habari ya kilichoitwa kwa kinyaki compromising information... Mada yake tunayo humu.

Kisha dada mtukutu akaja na uchambuzi wa watoto wa kuhamia watoto wa kufikia, watoto wa kuzaliwa ndani na nje ukiungalisha makala ile ya cha bei kubwa na tamati ya mangwe unapata jibu la wazi lakini la kuogofya sana kwamba mbuzi anaweza kudhani uchi wake umefichama kama wa kondoo kumbe uko tupu kabisa hata inzi akitaka kula mambo ni free to air.

Kwamba mtu anaweza kudhani kuwa kajificha mwili wote haonekani kabisa kumbe kazika kichwa ardhini kama mbuni tuu mzazi anautambua uzao wake wote watoto wakati wa makuzi tabia na asili hujidhihiri na zikizidi hufika mahali kutaka kumhoji mzazi mama mbona huyu hatufanani tabia?

Matendo ya Mungu si ya binadamu hata uwe mkweli na mkamilifu kiasi gani huwezi kupata cheo hapo angani kwakuwa kule hakuna majungu unafiki roho mbaya kiburi majivuno ulafi uzandiki na mambo kama hayo kwakuwa kule ni ulimwengu wa roho wakati matendo yako ni ya mwili Sana sana utaishia kuwa shetani ama wakala wake

Wasalaam bebi yake chamdeko
Jr
 
Mganga wakipare kaanza na uchi wa mbuzi tena asubuhi na mapema hata Tanzania ya viwanda kwake kichwani haipo yeye na nyuchi za wanyama, leo mbuzi kesho sijui itakua wa ngedere au kasuku
 
Sawa lakini la mbuni kuficha kichwa chake ardhini umetudanganya....
 
Back
Top Bottom