TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Bila Shaka umewahi kusikia kuhusu wachawi kula nyama za watu waliokufa, awali sikuwa nikiamini mambo haya lakini nilipoanza kupata akili za utambuzi ndipo nilianza kushuhudia mauza uza.
Nilikuwa kabla sijalala lazima nioge na kuwa safi kabisa lakini cha ajabu kila nikiamka asubuhi miguu ilijaa vumbi na udongo na kuchoka sana. Hali hiyo ilinitokea mara kadhaa kisha ikapotea, nikaanza kujiona kila nikilala usiku nilikuwa nanyanyuka na Nilikuwa nikitazama kitandani najiona nimelala.
Kisha nikawa napaa kama ndege naelea angani na nikawa naenda popote ila sikujua kwanini hali ile ilikuwa inanitokea pasipo ridhaa yangu. Ikafika mahali nikawa kila nikipaa natokea mahali nyumba ya mtu hata simjui, nakuta watu wengi kisha nakaribishwa sinia la nyama.
Hakika zilikuwa ni nyama za ng'ombe aliyechomwa vizuri nikawa nakula mpaka nashiba ndiii. Ilikuwa kila nikiamka asubuhi nimeshiba na hamu ya kula ikawa inaniondoka.
Haikuishia hapo ikawa nakutana na mwanamke mmoja amenona sana ila sura siikumbuki nikawa nabanjuka naye ipasavyo nikiamka nimechafuka ile ile. Hali ile ikaendelea kwa muda nikawa sasa usiku nikilala naona wachawi wanaoingia chumbani kwangu yaani nawaona kama mchana kabisa ila cha ajabu nipo usingizini.
Nilipokutana na mtaalamu mmoja ndipo akanieleza nilishalimishwa sana kichawi kisha baadae nikawa naweza kutoka na kupaa nilishalishwa sana nyama za watu pasipo kujua na nikawa na uwezo wa kuona watu pia nimeshazini na majini pasipo kujijua.
Ila nilipoanza kukemea hali ile ikapotea kabisa nikawa nalala kwa amani mpaka leo miaka kadhaa hali hiyo haipo tena katika maisha yangu.