Ijapokuwa kumekuwepo na kasumba ya kuamini ushirikina wa kila aina tulioukuta humu duniani lakini nachelea kusema kuwa hapatatokea uchawi ghali zaidi duniani kama matumizi sahihi ya uwezo wa kufikiri (akili) tuliokuja nao kutoka huko tusipopakumbuka. Ni imani yangu mengi mazuri yawe gunduzi za zama zile au hata hizi za hivi sasa na hata zile nyingi zijazo, ni kwamba nyingi kama si zote zinategemea matumizi sahihi ya uwezo wa mtu binafsi kufikiri zaidi.
Nikirejea nyumbani barani Afrika na hasa kwenye huu ukanda wa Afrika Mashariki kunako ndani ya taifa langu pendwa Tanzania, ni dhahiri kabisa mengi yanashindikana kwenda kwa sababu ya kutoshughulisha mbongo zetu vile ipasavyo, kwa mfano mafanikio ya mtu binafsi hayapaswi kuwa na taswira ya kielelezo kutoka kwa wale wahamasishaji wanaolenga namna ya kumfanya mtu awe mbinafsi zaidi yeye mwenyewe pasina kuhimizana kuleta au hata kuchochea mambo hasa gunduzi zenye kuleta tija kwa wanajamii wote wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Hoja ibaki kuwa matumizi sahihi ya uwezo wa kufikiri, binafsi nadhani uwe ni uchawi stahili kwetu sisi watu wa nchi za dunia ya tatu vinginevyo bila ya kujitengenezea uwezo huo tutabaki na mazingaombwe yetu yenye kutesana wenyewe kwa wenyewe sababu ya husda na chuki za kuona mwenzio anakuzidi uwezo wa kufikiri. Uchawi huu wa matumizi sahihi ya uwezo wa kufikiri nadhani yataleta tija zaidi katika maeneo yafuatayo:-
Kilimo, kabla ya kuwajengea watu dhana ya kulima na kutajirika, watu wajijenge kuwa na fikra tunduizi za namna gani ya kuweza kulima kwa kuisimamisha nchi ulimwenguni katika ulimaji au upatikanaji wa uhakika wa zao au mazao fulani.
Teknolojia, hapa hakuna uchawi huo wa kishirikina bali ni uwezo sahihi wa matumizi ya mbongo zetu kwa maana ya watu waweze kufikiri vizuri kuona namna gani ya kuitafuta na kuipigania teknolojia itakayoendana na mazingira yetu bila ya kupata kiwewe kutoka kwa wenzetu ambao kwa mfano hata kwa uwezo wao wa kiteknolojia hatupaswi sana kutegemea nyenzo zao sababu kiafya au kiusalama ni rahisi zaidi kuingiliwa na pengine hata kuhatarisha zaidi uimara wetu kwa hizi nchi zetu za barani Afrika na hasa Tanzania.
Rai yangu ni kwamba matumizi sahihi ya uwezo mzuri wa kufikiri (akili) yana tija na ni uchawi halisi wa maendeleo mengi ulimwenguni katika vitu vingi sana kwa mfano kwenye hizi siasa zetu natamani tungepata walau hata kupima baadhi ya wanasiasa sana sana wale wanaoligharimu taifa kwa chaguzi za marudio marudio na hata wale wasiothamini uzalendo wa taifa letu linapokuja suala la uongozi uliopo sasa unapofanya mambo mema kwa ajili ya maslahi ya taifa zungumziwa, pia kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, tunahitaji mantiki ya kuajiri watu kulingana na uwezo wao mzuri wa kufikiri kuliko matumizi ya mabavu hata pale pasipohitajika.
Karibuni kwa kutoa na kujadili maeneo mengine yanayohitaji uchawi huu ghali zaidi ulimwenguni.