Uchangishaji wa pesa mashuleni

Bengazuu

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
1,029
1,236
Wakuu naomba kuuliza hili swala la uchangishaji wa pesa mashuleni maana kuna shule ipo mkoani iringa "malangali boys secondary school" sijaelewa lengo la mkuu wa shule hiyo kuwalazimisha wadogo zetu kulipa gharama za umeme kwa kila mwanafunzi tsh 30, 000 na huo umeme kwa maelezo yake alikua anatarajia asubiri hadi ufike wa "REA" pia makubaliano ya utoaji wa pesa hizo haukuwa wa makubaliano baina ya walimu na wanafunzi na walimu na wazazi .

Lengo langu hasa naomba kujua kama kusaka haki kwa tatizo kama hili nitaanzia ngazi gani maana siwezi vumilia pesa ikiteketea kizembe umeme wa "REA" alisema utafika mwaka jana mwezi wa pili lakini hadi sasa hivi hali tete na analazimisha watu watoe noti hizo!

Nitaanzia wapi wakuu kutafuta suluhu la hili jambo?
 
Wasiliana kwanza na bodi ya shule na uwaeleze tatizo lako,kama kweli mchango huo upo utakua na baraka toka bodi ya shule.
 
Sawa mkuu japo barua yao ya awali inaonesha bodi wamebariki ila wamesema kutoa sio lazima ni hiyari ya mwanafunzi sasa nashangaaa imekua lazima tena
 
Ahaa hapo nimekuelewa asante sana wacha nilifanyie kazi
ahsante kwa kunielewa, usisahau kutupatia mrejesho wa majibu utakayopewa huko, ili yawe msaada kwa wengine wenye jambo kama hilo, stay blessed
 
Wakuu naomba kuuliza hili swala la uchangishaji wa pesa mashuleni maana kuna shule ipo mkoani iringa "malangali boys secondary school" sijaelewa lengo la mkuu wa shule hiyo kuwalazimisha wadogo zetu kulipa gharama za umeme kwa kila mwanafunzi tsh 30, 000 na huo umeme kwa maelezo yake alikua anatarajia asubiri hadi ufike wa "REA" pia makubaliano ya utoaji wa pesa hizo haukuwa wa makubaliano baina ya walimu na wanafunzi na walimu na wazazi .

Lengo langu hasa naomba kujua kama kusaka haki kwa tatizo kama hili nitaanzia ngazi gani maana siwezi vumilia pesa ikiteketea kizembe umeme wa "REA" alisema utafika mwaka jana mwezi wa pili lakini hadi sasa hivi hali tete na analazimisha watu watoe noti hizo!

Nitaanzia wapi wakuu kutafuta suluhu la hili jambo?

Hilo mbona lina unafuu....mwanafunzi anayechangia ananufaika moja kwa moja kwa kusomea kwenye taa...Je ungekuwa na mtoto anayesoma Loyola High school inayowataka wazazi kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ( "kupanda mbegu') wakati shule hiyo ni ya binafsi na wazazi hawana hisa za umiliki wake!
 
Back
Top Bottom