Uhaba wa Degree Programmes za Literature Vyuo Vikuu unasababisha uhaba wa Walimu wataalamu wa Literature mashuleni

May 10, 2021
12
8
Habari wakuu.

Tunapozungumzia kufundisha Literature tunazungumzia walimu wabobevu wa lugha ya kiingereza kwasababu hakuna fasihi bila lugha.

Kwa muda mrefu nimekua nikitatizwa na upungufu wa walimu wa somo la English literature mashuleni. Hivyo nimesukumwa kufuatilia suala hili kwa undani na kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya kwenye websites na prospectus za vyuo mbalimbali nimegundua kua course za literature zinatolewa na vyuo vichache sana.

Vyuo vingi vinajumuisha Literature ndani ya course za English mfano unakuta Bachelor of Arts With Education (Geography & English) English literature inajumuishwa kidogo sana ndani ya English kitu ambacho kinapelekea kushindwa kutengeneza walimu ama wataalamu madhubuti wa fasihi ya lugha ya kiingereza.

Ikumbukwe kwamba fasihi ni pana sana na inahitaji isomwe kwa upana wake na si kama ifanywavyo kwamba mwalimu wa fasihi atasoma poetry kidogo, drama kidogo na prose kidogo bila kuzama ndani zaidi. Suala hili linatengeneza walimu ambao si competent kwenye literature na wengi wao hujikuta katika hali ya kujilazimisha kufundisha somo hili mashuleni bila kuwa na utaalamu wa kutosha.

Ukija vyuoni pia utakuta walimu wa literature ni wachache sana kwasababu vyuo havitoi kipaumbele kwenye course hii.

Literature ni muhimu sana na ina opportunities nyingi ambazo bado vijana wengi hawazijui na kwa kusema hivyo ningependa kushauri vyuo vikuu vyenye social sciences au language centers kuandaa utaratibu wa kuanzisha degree programmes za literature.

Wasalam.

(NB: Mada hii ni ndefu na pana sana inahitaji majadiliano ya kina na kwa bahati mbaya nimeandika hapa JF kwa haraka ili angalau kufikisha ujumbe. Itapendeza zaidi kama kuna wataalamu wengine hapa waiongelee kwa mawanda mapana)
 
AKITOA JIBU LA MAANA,
NI_TAG FASTA.
Mpaka hapa naweza kusema hakuna jibu litakalokua la maana kwako. Kumbuka ulimwengu hauongozwi na fikra zako nyembamba kama unavyolazimisha iwe. Wakati mwingine kabla ya ku disvalue fikra za watu iruhusu akili yako ngumu kujifunza usiyoyajua ambayo unadhani unayajua.
Asante 🙏
 
Kuna walimu wengi sana wamesoma literature lakini wapo mtaani tu.
Hili limechagizwa na hapo awali serikali kutoipa kipaumbele English literature. Ni matarajio yangu mtaala mpya unaofanyiwa kazi unaweza kua mwarobaini wa hili
 
Samahani Mwalimu hivi ni ENGLISH LITERATURE au ni LITERATURE IN ENGLISH?
 
Mpaka hapa naweza kusema hakuna jibu litakalokua la maana kwako. Kumbuka ulimwengu hauongozwi na fikra zako nyembamba kama unavyolazimisha iwe. Wakati mwingine kabla ya ku disvalue fikra za watu iruhusu akili yako ngumu kujifunza usiyoyajua ambayo unadhani unayajua.
Asante

POVU HALITAKUSAIDIA CHOCHOTE MKUU.
LETA JIBU LA MAANA JUU YA FURSA ZA LITERATURE KWA NCHI HII!!!
 
  • Thanks
Reactions: K11

POVU HALITAKUSAIDIA CHOCHOTE MKUU.
LETA JIBU LA MAANA JUU YA FURSA ZA LITERATURE KWA NCHI HII!!!
Fursa zinaendana na utayari na uptitude za watu. Hatuwezi kukulazimisha tunachokiona fursa kwetu kiwe fursa kwako pia kama tayari umeshajenga solid mentality against it. Hakuna povu mzee wangu ni ugumu tu wa uwezo wako wa kuelewa pale unapoelekezwa.
 
Habari wakuu.

Tunapozungumzia kufundisha Literature tunazungumzia walimu wabobevu wa lugha ya kiingereza kwasababu hakuna fasihi bila lugha.

Kwa muda mrefu nimekua nikitatizwa na upungufu wa walimu wa somo la English literature mashuleni. Hivyo nimesukumwa kufuatilia suala hili kwa undani na kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya kwenye websites na prospectus za vyuo mbalimbali nimegundua kua course za literature zinatolewa na vyuo vichache sana.

Vyuo vingi vinajumuisha Literature ndani ya course za English mfano unakuta Bachelor of Arts With Education (Geography & English) English literature inajumuishwa kidogo sana ndani ya English kitu ambacho kinapelekea kushindwa kutengeneza walimu ama wataalamu madhubuti wa fasihi ya lugha ya kiingereza.

Ikumbukwe kwamba fasihi ni pana sana na inahitaji isomwe kwa upana wake na si kama ifanywavyo kwamba mwalimu wa fasihi atasoma poetry kidogo, drama kidogo na prose kidogo bila kuzama ndani zaidi. Suala hili linatengeneza walimu ambao si competent kwenye literature na wengi wao hujikuta katika hali ya kujilazimisha kufundisha somo hili mashuleni bila kuwa na utaalamu wa kutosha.

Ukija vyuoni pia utakuta walimu wa literature ni wachache sana kwasababu vyuo havitoi kipaumbele kwenye course hii.

Literature ni muhimu sana na ina opportunities nyingi ambazo bado vijana wengi hawazijui na kwa kusema hivyo ningependa kushauri vyuo vikuu vyenye social sciences au language centers kuandaa utaratibu wa kuanzisha degree programmes za literature.

Wasalam.

(NB: Mada hii ni ndefu na pana sana inahitaji majadiliano ya kina na kwa bahati mbaya nimeandika hapa JF kwa haraka ili angalau kufikisha ujumbe. Itapendeza zaidi kama kuna wataalamu wengine hapa waiongelee kwa mawanda mapana)
Una uhakika graduates wote wa Literature wamepata ajira mpaka udai kuna uhaba wa programmes hizo chuoni?
Au mpango wako degree zitolewe tu after that wakafuge nguruwe
 
Kwanza jifunze na ufuatilie government employing capacity dhidi ya current population na trend yake throughout.

Pili umefanya kosa kudogosha ufugaji wa nguruwe kuna watu wanaendesha maisha kwa hiyo shughuli. Hii inaonesha ni kiasi gani bado uko nyuma kifrikra.

Tatu ni wazi kabisa hujui malengo ya kua na degree na kama unayo basi ulivamia kusoma. Nenda kajifunze UQF na university curriculum development.

Itakusaidia sana mkuu
 
Wewe uliyejifunza ndio nimekuuliza, ukitazama public na private vacancies zilizopo dhidi ya graduates waliopo unaona kuna uhaba wa wasomi wa Literature?

Mwenye Degree ya Literature hawezi itumia kufugia nguruwe, akienda uko anazidiwa na mwenye certificate ya Animal Health au mfugaji mzoefu wa mwaka tu.

Kama hailipi na haina nafasi kubwa private na public sector yawezekana ndio maana haipewi nafasi kubwa tena. Ni matumizi mabaya ya rasilimali chache kumfundisha mtu viima na viharifu alafu akafuge nguruwe. Kwani kozi za ufugaji hakuziona?

Mimi nilijipangia mwenyewe nisome nini, malengo yangu niliyajua hivyo sikuvamia fani. Na nimejiajiri kupitia elimu hiyo.

Ninachotaka ni kila mtu asome vitu vyenye tija. Sio kuburuza watoto wengi wa maskini uwakopeshe mamilioni HESLB alafu wasome vitu havina matumizi makubwa kwenye soko.
 
Lengo la kusoma si kuajiriwa. Unaposoma chochote lenga kutumia elimu yako bila kuajiriwa na mtu no matter ni nini unasoma with exception ya vitu vichache sana. Hao waliko mtaani ni jukumu lao kutumia elimu yao kuifanyia kazi kama jinsi ambavyo wewe umefanyia kazi yako. Tuna mifano mingi ya waliosoma animal science, aquatic culture, agriculture na vingine vingi na bado wanasubiri ajira. Ni jukumu la mtu mwenyewe kutumia elimu yake vyuo havina kazi ya kukufuata mtaani vikutafutie kazi baada ya kukufundisha wakati wote. Unachokiita viima na viarifu ni kitu ambacho kinafanya watu wanaendesha maisha vizuri sana. Si kwakua huelewi ama hujawahi kuona basi utape haki ya kusema hakina faida wakati tupo ambao tunaona matunda yake na tunatamani wengine pia wafaidike kama sisi.
 
Wewe uliyejifunza ndio nimekuuliza, ukitazama public na private vacancies zilizopo dhidi ya graduates waliopo unaona kuna uhaba wa wasomi wa Literature?

Mwenye Degree ya Literature hawezi itumia kufugia nguruwe, akienda uko anazidiwa na mwenye certificate ya Animal Health au mfugaji mzoefu wa mwaka tu.

Kama hailipi na haina nafasi kubwa private na public sector yawezekana ndio maana haipewi nafasi kubwa tena. Ni matumizi mabaya ya rasilimali chache kumfundisha mtu viima na viharifu alafu akafuge nguruwe. Kwani kozi za ufugaji hakuziona?

Mimi nilijipangia mwenyewe nisome nini, malengo yangu niliyajua hivyo sikuvamia fani. Na nimejiajiri kupitia elimu hiyo.

Ninachotaka ni kila mtu asome vitu vyenye tija. Sio kuburuza watoto wengi wa maskini uwakopeshe mamilioni HESLB alafu wasome vitu havina matumizi makubwa kwenye soko.
Tz ina watu 61+M na capacity ya kuajiri serikalini na private haifiki 2M. 61M-2M=59M. sasa ukisoma na kusubiri uajiriwe ujue unafanya gambling. Serikali haina na haitowahi kuwa na uwezo wa kuajiri kila msomi na wakati programs zinatengenezwa vyuo vinajua hili.
 
Swali langu la msingi hujibu, wewe literature ulifaulu vipi kama swali wazi huwezi kuling'amua hizo tamathali utazijuaje.

Narudia kuuliza: Unadai programmes za Literature hazitolewi kwa wingi vyuoni, je una uhakika hata wakitoa kwa wingi soko lina uhitaji?
Kwenye soko la public na private (ambalo hili kwa maelezo yako naona hujui kuwa humo kunahusisha pia kujiajiri) kunaonyesha upungufu wa wataalamu hao?

Usije kuwa unataka kufufua umuhimu wa kozi, kumbe mahitaji yake madogo ndio hayaipi umuhimu.
 
Back
Top Bottom