UCHAMBUZI: Yaliyoachwa Kwenye Kashfa ya Uvujishaji Taarifa za Wana JF.

Feb 18, 2019
50
532
Wana JF poleni na majukumu ya siku nzima. Naomba nisiwe na maneno mengi tuingie moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Leo asubuhi kulisambaa taarifa kwamba taarifa zetu za siri humu JF si salama kwani zinafikika kirahisi ama kwa makusudi moderators wanazivujisha kunako mamlaka husika. Hii taarifa wengi waliipata twitter kupitia kwa mtu mmoja anayejiita Kigogo2014 ambapo alidai taarifa zake za siri kama email zimevuja pasipo yeye kujua.

Baada ya kutweet hivyo wengi walikimbilia kumshambulia mwanzilishi wa JF ndugu Maxence Melo kwamba anavujisha siri za watumiaji wa JF kwa sababu ya sekeseke anazozipata kutoka mamlaka za sheria. Wengi hawakujishughulisha kujua huyu bwana anayejiita Kigogo2014 kajuaje kama taarifa zake zimevuja?

Sasa huyu bwana alijua kwamba taarifa zake zimevuja baada ya Cyprian Musiba anayejinasibu kama mwanaharakati huru kufanya press conference leo asubuhi na kusema ya akwamba Kigogo2014 amekuwa akimtukana Rais akijua ya kwamba ni anonymous kumbe taarifa zake wanazo. Kwa kuthibitisha hilo ndipo akaonesha printed page yenye account details za Kigogo2014 anazotumia humu JF hasa email.

Namnukuu Musiba:
"Kuna account moja ambayo na hii mtashangaa sana, inaitwa Kigogo, kwa watu mnaopitia kwenye mitandao ya kijamii huyu Kigogo2014 ndivyo ilivyojisajili, lakini kuna bendera pale ya Kenya. Ana accounts zaidi ya nne mpaka tano. Huyu jamaa, ndiyo anaendesha account ya dada mmoja anaitwa Glory Mziray. Sijui kama waandishi wa habari na Watanzania mnamkumbuka, alikufa idara ya habari maelezo ya zamani, akiwa anaongea na waandishi kama hivi. Akadondoka tuu hapo chini akafariki.

Huyu Glory Mziray, aliasisiwa na wana mtandao, marehemu Glory Mziray kwa ajili ya kuwaelekeza Watanzania namna ambavyo wanamtandao wanaweza wakachukua nchi hii. Huyu Glory Mziray alizaa na mtu anaitwa Emmanuel Nchimbi, sijui kama mnanielewa vizuri, alizaa na mtu anaitwa Emmanuel Nchimbi,na mtoto wake anaitwa Dosha. Sasa baada ya kufa huyu dada Glory Mziray, baada ya kufariki account hii inaendeshwa na mtu anaitwa John Nchimbi. John Nchimbi aliwahi kupita TSN, kwa wale waandishi wa habari mnaowajua wamiliki wa magazeti ya HABARI LEO na DAILY NEWS.

Sijui kama ana mahusiano na Emmanuel Nchimbi, sina hakika lakini anaitwa John Nchimbi. Account hii inamtukana Mh Rais asubuhi, mchana na jioni, na inapotosha kuhusu utendaji wa serikali hii asubuhi mchana na jioni na ajenda ya account hii ni kuwa maarufu kwa sababu wanaamini kwamba ukimtukana Mh Rais, utakuwa maarufu, ukishakuwa maarufu watu wengi watakufollow na itakuwa kama vile alivofanya yule dada wa marekani."


Hiyo ni part ya aliyoyasema bwana Musiba kuhusu hii account ya Kigogo2014. Mengine aliyoyasema ni pamoja na kwamba huyu bwana John Nchimbi anafanya kazi taasisi ya NACTE kwa sasa na akatoa maneno ya vitisho kwamba kama umeajiriwa na serikali basi si sahihi kupingana nayo.

Kingine alichosema ni kwamba kuna viongozi kadhaa wa kisiasa wanai-follow kwa hiyo ni kama wanamtumia kupingana na mipango ya Mh Rais. Baadhi ya aliowataja ni Ridhiwan Kikwete, January Mkamba, Nape Nnauye, Zitto Kabwe, Freeman Mbowe, Emmanuel Nchimbi. Akaongezea kwamba kila anapoenda Bernad Membe basi na huyu John Nchimbi anayeendesha hizi account za Kigogo anakuwepo.

Ukiusoma mchezo mzima hapa utaona hawa watu wametumia mbinu kali mnoo ili kuwatisha watumiaji wa JF. Kifupi wametumia hii account ya Kigogo kujenga series ya matukio ya uongo ambayo kweli watu wameingia mkenge wa kuamini.

Sasa kwa hayo machache hebu tujiulize haya mambo kuhusu huyu bwana Kigogo2014:

1. Siku chache zilizopita huyu bwana Kigogo2014 ndio aliongoza harakati za kupatikana kwa msaidizi wa Zitto Kabwe aliyetekwa na kupatikana huko Mombasa Kenya. Kwa taarifa alizokuwa anazitoa kuhusu hao watekaji watu wengi waliamini jamaa ni untouchable kama nyanja ya intelijensia kwani alijinasibu kuwa anamjua mtekaji nje ndani kwa kutoa mpaka picha za nyumba anayoishi plus details zingine ambazo mtu wa kawaida ni vigumu kuzijua. Kwa kufanya hivyo alijijengea auntenticity kubwa sana mitandaoni.

Hivyo alijijengea trust kubwa sana kiasi kwamba leo alipopost tuhuma zake kwa mods wa JF watu hawakufikiria mara mbili mbili bali walimuamini palepale. Je, Hii ilitumika kama catalyst tuu ya kutuaminisha credibility ya huyu jamaa kwamba ni mwanaintelijensia mkali sana? Kama ndivyo, inakuwaje kwa mtu mwenye intelijensia ya namna ile aweze kudukuliwa kirahisi namna hiyo? Kama hakudukuliwa na kweli mods wamevujisha details zake inakuwaje hakulijua hili tangu mwanzo kwani yeye ana intelijensia kali sana?

2. Kwa nini Kigogo2014 kakubali tuhuma za Musiba haraka kiasi hiko? Ni kama walikuwa pamoja ile Musiba amepost press yake youtube na yeye Kigogo2014 akapost tuhuma zake twitter. Hivi tuseme hakujua impact yake itakuwaje? Hivi hakujua kwamba watakaoathirka ni JF na sio yeye? Kwa mwanaintelijensia mkali kama yule tulitegemea kama alichokisema Musiba ni kweli basi angekaa chini akafanya kauchunguzi kake kwanza kabla ya kutoa comments zozote.

Hata kama ni kweli zile details ni zake kulikuwa kuna haja gani kuzikubali publicly? As long as umetumia username fake nani atakulazimisha kwamba zile details ni zako?

3. Kwa nini Kigogo2014 atumie username na avatar ileile kwenye mitandao ya kijamii? Hili halina tatizo kama mtu unatumia original names zako. Lakini kwa mtu anayehitaji privacy/anonymity hatukutegemea atumie username na avatar kwenye social media mbili tofauti. Hii ina maana ya kwamba wakiweza kujua identity ya social media yako moja basi wanakuwa washajua na social media ya pili! Kwa mwanaintelijensia kama huyu hatukutegemea afanye grave mistake kama hii.

4. Lengo la haya yote lilikuwa kuwatisha watumiaji wa JF wajione hawako salama, je Kigogo2014 hakulitambua hili? Tutaamini vipi kwamba yeye hakuwa part ya huu mpango kwa sababu siku si nyingi alituaminisha kwamba yeye anajua mambo mengi yaliyo nyuma ya pazia? Kama kweli Kigogo2014 ameshajulikana alipo na anatuhumiwa kumtukana Mh Rais kwa nini wasimfuate pale NACTE na kumkamata bali wamekuja mitandaoni kutangaza kwamba wanajua taarifa za siri za watumia mitandao! Kama lengo sio kuwatisha watumiaji ni nini? Kigogo2014 ina maana kwa hiyo IQ yako hukuyajua yote haya?

5. Kama kweli Kigogo2014 wa kwenye twitter ndiye wewe Kigogo wa JF, kwa nini umeacha kupost chochote humu JF toka mwaka 2018 na ukajikita zaidi twitter? Kati ya twitter na JF wapi ni salama zaidi? Kwa tunaofikiria mbali tukisema ni kama ulienda twitter kwa mission maalumu ambayo ndio hii ya kuihujumu JF tutakuwa tunakosea?



Kwa kifupi kuna dilemma nyingi sana kuhusu huyu bwana na inabidi atuambie kinagaubana nini hasa lengo lake.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 
KIgogo ishakula kwake tayari, kigogo wa twitter ndio huyu wa humu JF na kosa kubwa alofanya ni kuweka namba yake ya simu hadharani.

Na ni mtu mmoja simple sana ukioneshwa huwezi kusema ndio ana jeuri ya kumtukana Mh. Rais kwa masaa24. Naona Musiba kaamua kulivalia njuga hili swala...

All in all Jamii Forum ya bwana Maxemence Mello ni sehemu salama sana, sema baadhi yetu humu ndani tumekuwa wepesi wa kuaminiana sana mpaka kupelekea kugawa taarifa zetu kwa watu, hilo la kusema JF inauza watu wake nakataa kabisa...
 
KIgogo ishakula kwake tayari, kigogo wa twitter ndio huyu wa humu JF na kosa kubwa alofanya ni kuweka namba yake ya simu hadharani.

Na ni mtu mmoja simple sana ukioneshwa huwezi kusema ndio ana jeuri ya kumtukana Mh. Rais kwa masaa24...
ntakuwa wa mwisho kuamini, hawa ni watu tofauti kabisa
 
ntakuwa wa mwisho kuamini, hawa ni watu tofauti kabisa
fanya kuangalia baadhi ya michango yake mwandiko na jinsi anavyowasilisha hoja zake humu jf ni sawa ni sawa na ile anayotumia twitter..

Ni vihumu sana mtu kuacha character yake chief..
 
Mleta mada ni kama anamlalamikia Kigogo na sio kujadili imekuaje Msiba amdukue account ya Jf na sio ile ya tweeter.

Mbona watz sio wajinga!
 
fanya kuangalia baadhi ya michango yake mwandiko na jinsi anavyowasilisha hoja zake humu jf ni sawa ni sawa na ile anayotumia twitter..

Ni vihumu sana mtu kuacha character yake chief..

Nimeliona hilo pia kigogo wa twitter ndo huyu huyu wa JF mwandiko unafanana kabisa

Na kingine kusema kaacha kupost toka 2018 ni hoja dhaifu ya kipumbavu na kijnga sana
 
Cha muhimu wakuu kwenye haya maisha usimuamini mtu.... hata wazazi..... sometimes hata wewe mwenyewe usijiamini sana ukapitiliza ....utaumia..
Mimi simuamini kuanzia mods ,wewe mtoa maada, kigogo , msiba n.k n.k
Kweli kabisa mkuu,kama mimi nisivyokuamini ww,huyu mtoa mada,na wengine wote.....
 
Nimeliona hilo pia kigogo wa twitter ndo huyu huyu wa JF mwandiko unafanana kabisa

Na kingine kusema kaacha kupost toka 2018 ni hoja dhaifu ya kipumbavu na kijnga sana
Ngoja tuone hiyo ijumaa kama musiba atatoa picha yake halisi, maana kwa kiasi fulani amechukia taarifa zake kuibuliwa leo kawa mpole sana huko twitter....
 
Back
Top Bottom