mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,125
- 1,757
Jiji la Mwanza kuna vituo vingi vya redio nikimaanisha Local/regional radios, kama
Jembe fm, Lake fm, Metro fm, Afya radio, Dira fm, Passion fm, Sauti fm, Iqrafm, Kwa Neema fm naomba nisiziweke RFA na KISS FM
Redio hizi zilianza kwa kasi sana lakini kwa sasa zinaonekana kama kushuka kwa kasi nakupoteza umaarufu
sijajua tatizo ni kuzoeleka masikioni, watangazaji wanaopendwa kuondoka, menejimenti kubadilishwa, mishahara midogo au kukosa matangazo
Naomba nizungumzie redio kadhaa ambazo nilizishuhudia kuanzishwa kwake kipindi nipo huko na kwa sasa nilivosikia na nimezifatilia hata nikiwa mbali through online (TuneIn)
JEMBE FM
Moja kati ya redio iliyoanza kwa kasi miaka ya 2015 na niseme ilileta ushindani mkubwa na timu yake ya watangazaji ilikuwa nzuri na ni redio maarufu yenye usikivu safi, ila kwa sasa naona kama imepunguza kasi kidogo tofauti na hapo awali sijajua shida ni nini
METRO FM
Naweza kusema hii ni moja kati ya redio za mwanza ambayo inajitahidi kumantain huwa haishuki wala haipandi sana na inasikilizwa sana sana nikili hilo nadhani nikutokana na customer base iliyojiwekea, ni redio ambayo mtangazi aondoke au menejimenti ibadilike huwezi ona kama imeyumba
PASSION FM
Ni redio ya muda mrefu sana ila huwa nashindwa kuielewa mpaka kesho, hpo zamani ilikuwa Dar kuna studio na Mwanza sijafahamu kwa sasa, ni redio ambayo haibadiliki iko vilevile miaka nenda rudi
LAKE FM
Ni redio ambayo pindi inaanzishwa mwaka 2016 tulijua italeta mapinduzi makubwa, ila naweza sema ni redio ambayo inapitia wakati mgumu na ni redio ambayo imepitia changamoto nyingi, kukatishwa tamaa naweza sema na vihujuma vya hapa na pale, kwa asilimia kubwa redio hii imeshuka sana sana, timu ya kwanza kuanzisha reio hii ilikuwa timu baab kubwa na ingeifikisha redio hii mbali, ila ile timu naona sahizi kila mtu anafanya issue zake na fursa zingine, pia kubadilika kwa watangazaji mara kwa mara yaani inakata sana, menejimenti pia naona inabadilika sana. Kama redio hii ikipata menejimenti nzuri na watangazaji wazuri watakaokaa muda mrefu itatisha siku zijazo.. Hii redio huw inaniuma sana
DIRA FM
Redio hii tangu nimeanza kuisikiliza naona iko tofauti kidogo na naweza sema kwa sasa Mwanza ndio redio pendwa sijajua ni kwa sababu ya miziki inayochezwa na madj kila kipindi bila sauti ya mtangazaji au ni nini, ila nimepita sehemu nyingi sana naona inasikilizwa, Bg up kwao wamefanya mapinduzi. Kuna mdau alionesha moja ya picha ya studio mara ya kwanza kabisa inaanza kurusha matangazo nilicheka sana ila nikaona picha zingine ni bonge moja la transformation
AFYA RADIO ni redio pia yenye base yake na ni redio niseme inayotoa watangazaji wakali sana ambao hunyakuliwa na media zingine za mwanza, hii redio huwa haipandi wala kushuka iko pale pale ni redio kongwe pia kwa mwanza, SAUT FM Redio ya chuo ambayo ni community based hii pia ina base yake na haiwezi kuchuja kwa wasikilizaji wake kwa sababu imeishajiwekea msingi flani,
Naomba niishie hapo nisizungumzie KWA NEEMA FM na IQRA FM, Hizi ndio media zetu na sisi tunazojivunia zinazoleta maana ya Jiji
I love rock city