Uchambuzi wa kitabu cha I, STEVE by Steve Jobs

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446





Nukuu yake ya “Your time is limited so don’t waste it living someone else’s life” . tafsiriye Usipoteze muda kuishi maisha ya mtu mwingine ukakosa kuishi wewe kama wewe. Hii ni nukuu muhimu sana kwa kila mmoja atakaye kuishi maisha toshelevu na kuhakikisha siku anayokufa basi anakuwa mtupu aendapo katika kaburi kwa kuishi katika utoshelevu na kutoa mchango mkubwa katika siku za uhai wa mtu. Karibu katika kujifunza mambo 25 alokuwa ameandika Steve Jobs ambayo ni muhimu katika kuyapa uzito na kuyatumia katika maisha ya ubunifu, kutanua masoko na kuathiri dunia kwa uchanya wake.


1. Kitu chochote cha Mafanikio makubwa kina msingi wake mkubwa katika muunganiko wake, mfano ni katika bidhaa ya ‘Apple’ ni muunganiko wa vipaji, teknolojia, mifumo bora na wafanyakazi wastadi kuhakikisha bidhaa ifikapo sokoni inakuwa bora sana. Hivyo muunganiko ni nguvu ya kitu kikubwa, bora na chenye nguvu duniani


2. Fungua macho uone, ina maana kuwa na fikra huru kuona mambo yanavyoenda katika dunia itakusaidia sana katika kupata mawazo na kuja na ubunifu mkubwa duniani. Watu wale wanaoruhusu kuwa na fikra huru na wazi ndio wanaofaidika na namna mambo katika dunia yaendavyo hasa katika eneo la teknolojia na masoko ya bidhaa au huduma.


3. Tafuta nukta hadi nukta unganisha siku zote. Duniani kila kitu kinatafuta umoja na unapokosekana umoja ni matatizo makubwa, mwili ukikosa umoja basi ni hatari sana katika maisha ya huyo mtu, ndivyo hata maisha ya kila siku mambo yakikosekana umoja ndio mwanzo wa matatizo makubwa, lakini ukijifunza kutafuta umoja wa vitu na mambo utaona mambo kitofauti sana na kuona uzuri wa mambo katika dunia.


4. Fanya tafiti kwa kitu chochote. Wanasema kama huna utafiti huna haki ya kuzungumza ni kweli kabisa. Utafiti ndio kiini cha kufanya mambo yazidi kuwa bora na kuongeza maarifa katika uso wa dunia, unataka kufanya kitu fanya tafiti kwanza hasa eneo la biashara kuwa na umakini mkubwa sana katika kutafuta na kutafiti masoko au mahitaji ya watu


5. Ukitaka kufanikiwa kwa kitu chochote tafuta nyenzo sahihi za kutumia ili uweze kufanikisha kile unachotamani kufanikiwa.


6. Malalamiko, shida na mahitaji ya wateja ni fursa kwa mfanyabishara au mjasiriamali katika kujitafakari juu ya huduma zake na namna gani atakuja na mbinu za kutatua hayo.


7. Kuwa tajiri katika kaburi ni kuonyesha wazi namna gani nafasi ya uhai ambavyo hatuitumii katika utoshelevu wake. Steve Jobs alisema kuwa kulala katika utoshelevu na kufanikiwa kwa kufanya kitu bora katika siku kwake kulifaa zaidi kuliko kulala kaburini akiwa tajiri. Hapa ni pakutafakari sana nafasi hii ya kuwa hai


8. Kuwa wa pekee , jitofautishe siku zote. Upekee wako ndio alama yako na hatatokea mtu kama wewe ukishaondoka katika maisha haya. Hivyo ishi utofauti wako na kwa nafasi yako toa mchango kwa huo huo upekee wako.


9. Fanya kazi na watu walio tayari kufanya kazi na wewe. Utayari ni hali ambayo kadri siku zinapoenda watu walio tayari wanazidi kupungua, hivyo ukipata wachache walio tayari ni heri uende nao hao kuliko wengi wasio na tayari ya kutenda


10. Kuwa na fokasi ni kusema HAPANA hata katika mambo mazuri 1000 ambayo yatabisha hodi kwako.


11. Biashara yenye mafanikio makubwa duniani kote ni ile yenye kuweka shabaha yake katika bidhaa hiyo, huduma hiyo na ujuzi huo kumwangalia mteja wake siku zote.


12. Jana imeshapita, leo unayo na kesho i katika nafasi ya wewe kufanya vizuri sasa kutabiri kesho nzuri. Jifunze katika kutazama mbele na yaliyopita yasiwe kikwazo kwa safari yako ya kusonga mbele siku zote.


13. Lengo au malengo ndio njia ya mawazo kujiweka katika umbo na kushikika, mbali na hapo mawazo kila mtu anaweza kuwaza mafanikio lakini ni mpaka pale ambapo ukiweka lengo ndipo wazo linashika umbo lake. Kukosa malengo ni kuishi katika ndoto ungali unatembea


14. Kufanya kazi na kujituma ni nidhamu ya watu waliofanikiwa duniani kote na hakuna mbadala wao kuwaondoa katika kazi siku zote. Kundi hili ndio utakuta wakifanya kazi masaa mengi zaidi kuliko makundi mengine yote. Steve Jobs anaeleza alipokuwa akiamka asubuhi sana na kwenda kazini kufanya kazi sana na hii ndio siri pia ya mafanikio ambayo aliiletea kampuni ya Apple.


15. Ishi kama msanii, ona vitu katika namna tafauti tafauti siku zote na hii ndio njia ya kutoishiwa mawazo na ubunifu.


16. Unganisha mawazo na nguvu ( Kazi ) katika kuhakikisha mambo yanatokea


17. Hamasisha wafanyakazi wako, na hata wale wakaribu yako katika kuwafanya nao wapige hatua kubwa siku zote. Kampuni zinazofanya vizuri duniani zina siri hii ya kuhamasisha wafanyakazi wao kufanya kazi katika ubora


18. Usifikiri eneo moja “Parochial Thinking”. Dunia inaenda kwa kasi sana kufikiri eneo moja hakutoshi kwa sasa, ufikiri zaidi ya eneo dogo unaloishia kufikiri.


19. Kuwa na shauku hakutoshi unahitaji kuichochea shauku yako siku zote ili ufanye mambo makubwa katika maisha.


20. Fanya sasa ( Do it now ). Huwezi jua kuwa nafasi hiyo yaweza kujirudia tena, hasa nafasi kama uhai ni zawadi ya pekee iliyo na toleo mara moja.


21. Usiweke wazi kila kitu juu ya biashara yako au maisha yako, kufichwa kwa baadhi ya vitu katika maisha ni kuvipa thamani yake.


22. Urahisi ni kazi kuliko ugumu


23. Fikiri kupitia changamoto siku zote ili uzalishe mawazo na njia ya kutoka.


24. Tafuta hekima siku zote. Steve Jobs kila ilipokuwa ikifika mchana alimpenda sana kumsoma Socrates ili ajifunze hekima katika maisha yake na biashara. Na wewe pia weka nafasi ya kujifunza kupitia Vitabu Takatifu na kwa watu wengine kupata hekima


25. Ajiri watu wenye shauku ya kutaka kuleta mabadiliko katika dunia na wana kiu hiyo kuleta utofauti duniani.


Kuna mengi zaidi ya kuendelea kujifunza katika kitabu hiki cha nukuu zake na maneno yake katika kutuachia alama kubwa sana ya maneno yenye nguvu katika kutupa hamasa ya kwenda kutenda zaidi na kuwa watu wenye matokeo chanya kwa jamii yetu na dunia kwa ujumla
 
Back
Top Bottom