Uchambuzi wa hotuba ya Rais Magufuli wakati akimwapisha Waziri wa Katiba na Sheria

Mkuu Chadema hawapendi uchambuzi wa kitaalamu
Wao wanampenda mtu anayemtukana Rais matusi
Wewe juha uko uchi ubongoni kauvalishe elimu! Hivi mtu kuandika kilichosemwa na mwingine kwa maana ya kunukuu ni kuchambua? Umesoma Nini na wapi ulikofundishwa kuwa quotation ni uchambuzi wa kitaalamu? Mbwiga unaboa Sana na unauharibu umaarufu wa ccm kwa hoja zako za kiutopolo!
 
UCHAMBUZI WA HOTUBA YA MAGUFULI.

Na, Robert Heriel

Kutokana maombi ya watu wengi wakiwamo viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa, na Watanzania kwa ujumla kuwasiliana nami kwa njia simu, wengine wakinitumia ujumbe kwenye WhatsApp, messenger, au SmS za kawaida, kunitaka nieleze maoni yangu kufuatia hotuba ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli, nami kwa heshima kubwa nichukue nafasi hii kupokea ombi lao. Nami leo hii nichukue nafasi hii kuchambua kile alichokieleza Mhe. Rais ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwenye sehemu kubwa ya hotuba hiyo, na kwa uchache kuikosoa hotuba hiyo.

Ifahamike Uchambuzi huu, ni kwa maslahi mapana ya taifa, huku nikizingatia zaidi uzalendo na kusema ukweli pasi na hofu wala kupendelea.

Uchambuzi wa Hotuba ya Mhe. Rais.

Hotuba ya Mhe Rais inaweza kujadiliwa na watu wengi. Wapo watakaombeza, wapo watakaompongeza, lakini pia wapo watakaozingatia ukweli pasipo kupendelea.

Hotuba ya Mhe Rais imejaribu kueleza mambo kadhaa ambayo mengine yapo dhahiri lakini mengine yakiwa ya siri.

Yafuatayo ni sehemu ya mambo ambayo Mhe. Rais ameweza kuyaeleza katika hotuba yake:

1. Historia ya Magonjwa

Mhe. Rais katika hotuba yake ameweza kueleza kwa kifupi kabisa historia ya magonjwa ikiwamo ugonjwa wa surua, Ukoma, TB, EBOLA, ZIKA miongoni mwa magonjwa mengine. Mhe Rais, ameweza kuelezea historia fupi ya magonjwa hayo na jinsi yalivyokuwa tishio kwa zama hizo lakini licha ya kuwa tishio magonjwa hayo yalipita na kuonekana yakawaida. Pia amewaasa watanzania kuchukua tahadhari. Lengo kuu la kutoa historia ya magonjwa ni kuwatoa hofu baadhi ya Watanzania ili kupunguza athari za kisaikolojia katika afya yao.

Hili naungana naye kwa asilimia mia moja.

2) Sababu za Kukataa Lockdown

Mhe Rais kupitia Hotuba yake ameelezea sababu ya kukataa lockdown nchi nzima au sehemu fulani ya nchi. Moja ya sababu kuu ni suala zima la uchumi. Mhe. Rais anaamini na anataka Watanzania waamini na kuungana naye kuwa kuifungia nchi au sehemu ya nchi kutaumiza uchumi wa taifa. Na hiyo italeta athari kwa nchi kujiendesha mathalani, kulipa wafanyakazi na watumishi wa serikali. Mhe. Rais kupitia hotuba yake amejitetea kwa kutoa mifano dhahiri ya kulipa Waalimu na Wafanyakazi wengine zaidi ya miezi miwili na kuwahakikishia kuendelea kuwalipa licha ya corona kuendelea kuitesa dunia.

Hili naungana naye kwa asilimia mia moja, na kila siku nalihamasisha kila nipatapo nafasi.

3) Hujuma kwenye Sekta ya Afya

Mhe. Rais kupitia hotuba yake ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na baadhi ya Wafanyakazi wa sekta ya Afya hasa katika Maabara kuu ya taifa kuwa huenda kuna hujuma inaendelea. Shutuma za Mhe. Rais katika ofisi hizo ni kutokana na uchunguzi wa kimkakati baada ya kuona matokeo ya shaka katika vipimo vya kupimia Corona.

Mhe. Rais kupitia hoja yake ya uhujumu kwa baadhi ya wataalamu amelenga kuwaambia Watanzania kuwa kuna Wasaliti wa nchi kwa namna ya moja kwa moja au ya kujificha. Hujuma kwa kukusudia au bila kukusudia.

Aidha, hujuma hizo zinalenga vipimo vyenyewe, Au Reagent, pamba, au kuna namna vifaa hivyo vimesetiwa kuwa vitoe majibu kwa mpango maalumu ulioratibiwa, yaani kila wapimwapo watu 20 basi yule wa 21 aonekane anamaambukizi.

Hii inanipa tafsiri kadhaa katika kumuelewa Mhe. Rais, mosi, Mhe Rais anajaribu kuniambia kuwa yeye hawaamini watenda kazi wake. Je ni kosa kwa Kiongozi kutowaamini Watendakazi wake, na hapa ni wahusika wa sekta za Afya? Jibu ni hapana, sio kosa kwake kutokuwaamini. Hasa ukizingatia kanuni ya "Trust no one", ya macheavili.

4) Umuhimu wa Intellejensia imara.

Hotuba ya Mhe Rais imefafanua kwa kina namna gani taifa letu lilivyokuwa na intellejensia imara, na jinsi linavyotakiwa kuwa imara. Kupitia mbinu ya kutuma sampo bandia na kuya-label kwa majina ya watu kisha kugundua kuwa kuna sintofahamu katika matokeo ya vipimo. Kumetoa maana kadhaa, moja wapo ni kuchunguza vipimo vilivyoletwa huenda vimeghushiwa na virusi vya corona, au Wahusika wamenunuliwa.

Intellejensia inasaidia kukusanya taarifa muhimu, kuzichunguza, kuzifanyia kazi, kuzizuia zisitoke ikiwa zitaleta madhara.

Katika Intellejensia Mhe. Rais amejaribu kueleza Watanzania kuwa makini na kila wasemalo mataifa ya nje. Yaani tuache ku-copy na ku- paste kila kitu.

Na hii tutaifanya ikiwa tutakuwa na Intellejensia imara ili kuepusha madhara.

Kupitia Intellejensia Mhe. Rais alilenga kuwaambia Watanzania kuwa kama hatutakuwa na Intelejensia nzuri ni rahisi kuvurugwa na Propaganda za maadui

5) Wazushi na Wapotoshaji

Mhe. Rais, kwenye hotuba yake ameelezea na kukemea wale wote wanaozusha na kupotosha katika janga hili la Corona. Sio kila anayeanguka na kufa kwa Corona, sio kila anayekufa amekufa kwa corona. Uwepo wa Corona hauondoi magonjwa mengine.

Lengo la hoja hii ni kuzuia watu wanaozusha kutengeneza hofu na wasiwasi ndani ya jamii.

6) Viongozi wa Dini Bandia.

Mhe. Rais katika hotuba yake amewaambia watanzania kuwa wakati huu ndio muda muafaka ya kuwatambua viongozi wa dini bandia ambao jambo hili wamekuwa na imani haba. Pia ameonyesha msimamo wake kuwa bado anaamini katika maombi, na anaomba kuungwa mkono katika hilo na Watanzania wengine.

7) Suala la Kupokea Ushauri

Mhe. Rais kupitia Hotuba yake amejibu ile kashfa aliyopewa na baadhi ya wakosoaji wake kuwa "hashauriki". Kupitia maneno yake kuwa ataongea na kushauriwa na Wataalamu wa masuala ya kiafya. Pia katikia kumsifia Katibu, ni dhahiri kuwa kile alichokuwa anakisema hasa kuhusu vipimo vya Sampo bandia inaonekana ni ushauri wa Katibu aliyekuwa akimtaja mara kwa mara huku akimpa sifa.

Hii inatoa maana moja kuwa, Mhe. Rais ni kiongozi anayeshaurika lakini sio kila mtu anaweza kupokea ushauri wake. Hii ni kwa mtu yoyote.

8) Afrika inaweza, ijiamini.

Mhe. Rais pia ameweza kueleza pia suala la Waafrika wakiwemo Watanzani kuwa tuamini kuwa "tunaweza" Mara kwa mara Mhe. Rais amelieleza jambo hili kila apatapo nafasi ya kuhutubia. Amewaomba Watanzania waamini katika tiba zao za asili ikiwamo kujifukiza(hotuba iliyopita aliyokaa na vyombo vya ulinzi na usalama). Pia katika kuthibitisha hilo, amewaambia wananchi kuwa ataagiza Dawa iliyokwisha kutangazwa huko Madagasca.

9) Kukumbusha Tahadhari.

Pia hotuba yake mara kwa mara amekuwa akikumbusha watu kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona.

Baada ya kuona sehemu ya mambo machache aliyoyaeleza Mhe. Rais katika Hotuba yake.

Mapungufu machache katika Hotuba ya Magufuli.

1. Sio kila Mpinzani anayekosoa anatumiwa na Mabeberu.

Mhe Rais, hotuba yake mwishoni mwishoni ameeleza kuhusu wapinzani waliotoa tamko la kutohudhuria vikao vya Bunge. na kutoa amri kuwa wasipewe posho, sijajua ipo kisheria au haipo kuwa mbunge asipohudhuria kikao kimoja asipewe posho au ni tamko la Mhe. Rais la kihisia. Lakini pia sio kila mpinzani anayekosoa serikali anatumiwa na Mabeberu.

b) Kuchanganya kisa cha Yona na Daniel

Mhe. Rais katika hotuba yake ameonyesha udhaifu katika kutoa mfano wa kisa cha biblia kwa kukichanganya. Hii inatoa tafsiri mbili, mosi huenda Mhe Rais amesahau Biblia, pili, hajui biblia.

Hii inaweza tumiwa na wapinzani wake kama kete ya kumsimanga mitandaoni au kwenye majukwaa mbalimbali.

Hata hivyo hakuna mwanadamua aliyekamilika kwa kila kitu.

ATHARI ZA HOTUBA YA MHE. RAIS
  • Kimataifa.
> Hotuba ya Mhe. Rais, imeitangazia dunia kuwa nchi ya Tanzania huenda haina Madaktari bora wa maabara. Itazua maswali mengi kwa watu wa kawaida na wanataaluma kuhusu elimu ya madaktari wa maabara. Inawezekana vipi Daktari wa maabara tena maabara kuu ya taifa ashindwe kujua sampo ya binadamu na sampo vya viumbe au vitu vingine?

> Hotuba itaongeza wasiwasi kwa mataifa mengine hasa ya Afrika kuhusu vipimo vya Corona kuwa huenda ni bandia au vimesetiwa kama sio kuwekwa maambukizi ya Corona.

> Hotuba ya Rais itaamsha hisia za uhasama baina ya taifa letu na baadhi ya mataifa yaliyoendelea ambayo Mhe. Rais ameyapa jina kama Mabeberu ambayo kimsingi anaamini hayapendi maendeleo ya taifa hili.

  • KITAIFA
> Hotuba ya Mhe. Rais itafanya baadhi ya Watanzania kutoamini matokeo ya vipimo vya afya hasa katika Ugonjwa wa Corona. Yaani mtu akipimwa hata akiwa na Corona anaweza kukataa kuwa ana huo ugonjwa.

> Hotuba ya Mhe. Rais itaibua dhana kwa baadhi ya Watanzania wenye ufinyu wa fikara kuwa hata Papai, fenesi na Mbuzi wana-Corona na hawafi, wengine kufikia hatua wasile kabisa jambo ambalo sio sahihi.

> Hotuba ya Mhe Rais itafanya watu wengi kuupuuzia ugonjwa wa Corona na kutochukua tahadhari licha ya Mhe. Rais kusisitiza kuwa watu waendelee kuchukua tahadhari. Hii ni kutokana na Mhe. Rais kuwaomba watanzania wasiwe na hofu kwani Corona ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine. Mhe. Rais hotuba yake haijaupa ugonjwa huu uzito sana katika hotuba yake, ila hotuba yake imejikita zaidi kuwapa moyo watanzania, na kuwaaminisha kuwa wapo watu wanaotishia watanzania kuhusu huu ugonjwa jambo ambalo ugonjwa sio mkubwa kama unavyotangazwa.

> Hotuba ya Mhe. Rais itawapa wapinzani mambo mengi zaidi ya kusema kwani katika kipengele cha matokeo ya sampo za mapapai, mafenesi, mbuzi n.k kina maswali mengi.

NINI HAKUPASWA KUKISEMA MHE. RAIS KWENYE HOTUBA YAKE
>
Mhe Rais hakupaswa kuzungumza habari za matokeo ya Sampo kwa namna alivyoelezea. Hakupaswa kusema mbele ya kamera kuwa zilipelekwa sampo za vitu a,b,c, d bila ya mpimaji wa sampo (mtaalamu wa maabara kujua) kisha matokeo yakatoka 1,2,3. Kutamka hivi ni kuambia Watanzania na dunia kwa ujumla kuwa Tanzania hakuna wataalamu za maabara na ndio maana walishindwa kung'amua kwa haraka kuwa hizo sampo hazijatoka kwenye mwili wa mwanadamu.

Mhe Rais alipaswa aseme kuwa; serikali ilipima pia baadhi ya viumbe hai na visivyohai kama vile mbuzi, fenesi, papai, n.k na kukutwa na virusi vya Corona, wakati kondoo, mafuta, nk havikukutwa na Corona. Hivyo WHO inapaswa ifuatilie jambo hilo.

Alafu Katika vikao vya ndani, akiwa pamoja na wataalamu wa Afya aeleze kile alichoeleza na kuwashughulikia wale wote waliopima sampo za viumbe wengine wakidhani ni sampo za binadamu. Hao watachukuliwa hatua za kisheria na kitaaluma kuwa elimu na fani yao inashaka.
Mwisho: Nimpongeze Mhe. Rais katika Hotuba yake ambayo kwa sehemu kubwa imetoa faraja, imeondoa hofu, imewatia moyo, imeonyesha uwajibikaji na namna serikali inavyojali wananchi wake licha ya changamoto za hapa na pale.

Watu tuendelee kuchukua tahadhari.

Binafsi tangu jana sipo poah kutokana na dalili kadhaa za homa, nimetumia tiba za jadi huku nikiendelea kujihadhari na wale wanaohusiana nami. Kikawaida sio muoga, ninakabiliana na jambo lolote bila kujali ukubwa wake kwa Maana Mungu Taikon ananguvu.

Robert Heriel

Taikon wa Fasihi

Kwa sasa Morogoro, Tanzania.

0693322300 Ipo pia whatsapp

0711345431
 
Na, Robert Heriel

Kutokana maombi ya watu wengi wakiwamo viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa, na Watanzania kwa ujumla kuwasiliana nami kwa njia simu, wengine wakinitumia ujumbe kwenye WhatsApp, messenger, au SmS za kawaida, kunitaka nieleze maoni yangu kufuatia hotuba ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli, nami kwa heshima kubwa nichukue nafasi hii kupokea ombi lao. Nami leo hii nichukue nafasi hii kuchambua kile alichokieleza Mhe. Rais ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwenye sehemu kubwa ya hotuba hiyo, na kwa uchache kuikosoa hotuba hiyo.

Ifahamike Uchambuzi huu, ni kwa maslahi mapana ya taifa, huku nikizingatia zaidi uzalendo na kusema ukweli pasi na hofu wala kupendelea.

Uchambuzi wa Hotuba ya Mhe. Rais.

Hotuba ya Mhe Rais inaweza kujadiliwa na watu wengi. Wapo watakaombeza, wapo watakaompongeza, lakini pia wapo watakaozingatia ukweli pasipo kupendelea.

Hotuba ya Mhe Rais imejaribu kueleza mambo kadhaa ambayo mengine yapo dhahiri lakini mengine yakiwa ya siri.

Yafuatayo ni sehemu ya mambo ambayo Mhe. Rais ameweza kuyaeleza katika hotuba yake:

1. Historia ya Magonjwa

Mhe. Rais katika hotuba yake ameweza kueleza kwa kifupi kabisa historia ya magonjwa ikiwamo ugonjwa wa surua, Ukoma, TB, EBOLA, ZIKA miongoni mwa magonjwa mengine. Mhe Rais, ameweza kuelezea historia fupi ya magonjwa hayo na jinsi yalivyokuwa tishio kwa zama hizo lakini licha ya kuwa tishio magonjwa hayo yalipita na kuonekana yakawaida. Pia amewaasa watanzania kuchukua tahadhari. Lengo kuu la kutoa historia ya magonjwa ni kuwatoa hofu baadhi ya Watanzania ili kupunguza athari za kisaikolojia katika afya yao.

Hili naungana naye kwa asilimia mia moja.

2) Sababu za Kukataa Lockdown

Mhe Rais kupitia Hotuba yake ameelezea sababu ya kukataa lockdown nchi nzima au sehemu fulani ya nchi. Moja ya sababu kuu ni suala zima la uchumi. Mhe. Rais anaamini na anataka Watanzania waamini na kuungana naye kuwa kuifungia nchi au sehemu ya nchi kutaumiza uchumi wa taifa. Na hiyo italeta athari kwa nchi kujiendesha mathalani, kulipa wafanyakazi na watumishi wa serikali. Mhe. Rais kupitia hotuba yake amejitetea kwa kutoa mifano dhahiri ya kulipa Waalimu na Wafanyakazi wengine zaidi ya miezi miwili na kuwahakikishia kuendelea kuwalipa licha ya corona kuendelea kuitesa dunia.

Hili naungana naye kwa asilimia mia moja, na kila siku nalihamasisha kila nipatapo nafasi.

3) Hujuma kwenye Sekta ya Afya

Mhe. Rais kupitia hotuba yake ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na baadhi ya Wafanyakazi wa sekta ya Afya hasa katika Maabara kuu ya taifa kuwa huenda kuna hujuma inaendelea. Shutuma za Mhe. Rais katika ofisi hizo ni kutokana na uchunguzi wa kimkakati baada ya kuona matokeo ya shaka katika vipimo vya kupimia Corona.

Mhe. Rais kupitia hoja yake ya uhujumu kwa baadhi ya wataalamu amelenga kuwaambia Watanzania kuwa kuna Wasaliti wa nchi kwa namna ya moja kwa moja au ya kujificha. Hujuma kwa kukusudia au bila kukusudia.

Aidha, hujuma hizo zinalenga vipimo vyenyewe, Au Reagent, pamba, au kuna namna vifaa hivyo vimesetiwa kuwa vitoe majibu kwa mpango maalumu ulioratibiwa, yaani kila wapimwapo watu 20 basi yule wa 21 aonekane anamaambukizi.

Hii inanipa tafsiri kadhaa katika kumuelewa Mhe. Rais, mosi, Mhe Rais anajaribu kuniambia kuwa yeye hawaamini watenda kazi wake. Je ni kosa kwa Kiongozi kutowaamini Watendakazi wake, na hapa ni wahusika wa sekta za Afya? Jibu ni hapana, sio kosa kwake kutokuwaamini. Hasa ukizingatia kanuni ya "Trust no one", ya macheavili.

4) Umuhimu wa Intellejensia imara.

Hotuba ya Mhe Rais imefafanua kwa kina namna gani taifa letu lilivyokuwa na intellejensia imara, na jinsi linavyotakiwa kuwa imara. Kupitia mbinu ya kutuma sampo bandia na kuya-label kwa majina ya watu kisha kugundua kuwa kuna sintofahamu katika matokeo ya vipimo. Kumetoa maana kadhaa, moja wapo ni kuchunguza vipimo vilivyoletwa huenda vimeghushiwa na virusi vya corona, au Wahusika wamenunuliwa.

Intellejensia inasaidia kukusanya taarifa muhimu, kuzichunguza, kuzifanyia kazi, kuzizuia zisitoke ikiwa zitaleta madhara.

Katika Intellejensia Mhe. Rais amejaribu kueleza Watanzania kuwa makini na kila wasemalo mataifa ya nje. Yaani tuache ku-copy na ku- paste kila kitu.

Na hii tutaifanya ikiwa tutakuwa na Intellejensia imara ili kuepusha madhara.

Kupitia Intellejensia Mhe. Rais alilenga kuwaambia Watanzania kuwa kama hatutakuwa na Intelejensia nzuri ni rahisi kuvurugwa na Propaganda za maadui

5) Wazushi na Wapotoshaji

Mhe. Rais, kwenye hotuba yake ameelezea na kukemea wale wote wanaozusha na kupotosha katika janga hili la Corona. Sio kila anayeanguka na kufa kwa Corona, sio kila anayekufa amekufa kwa corona. Uwepo wa Corona hauondoi magonjwa mengine.

Lengo la hoja hii ni kuzuia watu wanaozusha kutengeneza hofu na wasiwasi ndani ya jamii.

6) Viongozi wa Dini Bandia.

Mhe. Rais katika hotuba yake amewaambia watanzania kuwa wakati huu ndio muda muafaka ya kuwatambua viongozi wa dini bandia ambao jambo hili wamekuwa na imani haba. Pia ameonyesha msimamo wake kuwa bado anaamini katika maombi, na anaomba kuungwa mkono katika hilo na Watanzania wengine.

7) Suala la Kupokea Ushauri

Mhe. Rais kupitia Hotuba yake amejibu ile kashfa aliyopewa na baadhi ya wakosoaji wake kuwa "hashauriki". Kupitia maneno yake kuwa ataongea na kushauriwa na Wataalamu wa masuala ya kiafya. Pia katikia kumsifia Katibu, ni dhahiri kuwa kile alichokuwa anakisema hasa kuhusu vipimo vya Sampo bandia inaonekana ni ushauri wa Katibu aliyekuwa akimtaja mara kwa mara huku akimpa sifa.

Hii inatoa maana moja kuwa, Mhe. Rais ni kiongozi anayeshaurika lakini sio kila mtu anaweza kupokea ushauri wake. Hii ni kwa mtu yoyote.

8) Afrika inaweza, ijiamini.

Mhe. Rais pia ameweza kueleza pia suala la Waafrika wakiwemo Watanzani kuwa tuamini kuwa "tunaweza" Mara kwa mara Mhe. Rais amelieleza jambo hili kila apatapo nafasi ya kuhutubia. Amewaomba Watanzania waamini katika tiba zao za asili ikiwamo kujifukiza(hotuba iliyopita aliyokaa na vyombo vya ulinzi na usalama). Pia katika kuthibitisha hilo, amewaambia wananchi kuwa ataagiza Dawa iliyokwisha kutangazwa huko Madagasca.

9) Kukumbusha Tahadhari.

Pia hotuba yake mara kwa mara amekuwa akikumbusha watu kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona.

Baada ya kuona sehemu ya mambo machache aliyoyaeleza Mhe. Rais katika Hotuba yake.

Mapungufu machache katika Hotuba ya Magufuli.

1. Sio kila Mpinzani anayekosoa anatumiwa na Mabeberu.

Mhe Rais, hotuba yake mwishoni mwishoni ameeleza kuhusu wapinzani waliotoa tamko la kutohudhuria vikao vya Bunge. na kutoa amri kuwa wasipewe posho, sijajua ipo kisheria au haipo kuwa mbunge asipohudhuria kikao kimoja asipewe posho au ni tamko la Mhe. Rais la kihisia. Lakini pia sio kila mpinzani anayekosoa serikali anatumiwa na Mabeberu.

b) Kuchanganya kisa cha Yona na Daniel

Mhe. Rais katika hotuba yake ameonyesha udhaifu katika kutoa mfano wa kisa cha biblia kwa kukichanganya. Hii inatoa tafsiri mbili, mosi huenda Mhe Rais amesahau Biblia, pili, hajui biblia.

Hii inaweza tumiwa na wapinzani wake kama kete ya kumsimanga mitandaoni au kwenye majukwaa mbalimbali.

Hata hivyo hakuna mwanadamua aliyekamilika kwa kila kitu.

Mwisho: Nimpongeze Mhe. Rais katika Hotuba yake ambayo kwa sehemu kubwa imetoa faraja, imeondoa hofu, imewatia moyo, imeonyesha uwajibikaji na namna serikali inavyojali wananchi wake licha ya changamoto za hapa na pale.

Watu tuendelee kuchukua tahadhari.

Binafsi tangu jana sipo poah kutokana na dalili kadhaa za homa, nimetumia tiba za jadi huku nikiendelea kujihadhari na wale wanaohusiana nami. Kikawaida sio muoga, ninakabiliana na jambo lolote bila kujali ukubwa wake kwa Maana Mungu Taikon ananguvu.

Robert Heriel

Taikon wa Fasihi

Kwa sasa Morogoro, Tanzania.

0693322300 Ipo pia whatsapp

0711345431

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona umesahau anayeapishwa ni waziri wa sheria huu mjadala hauoni kwamba Mwigulu ameanza hii ngwe kwa mguu wa kushoto huku ukijua aliyemteua ni mtu wa kukurupuka. Waziri wa sheria na vipimo vya Mahabara tena kutafuta jinai hivi angekuwa Marehemu mzee Mahiga kweli angempa ujumbe wa namna hii.

Yaani mzee baba walipa kodi maskini wa nchi hii wamemlipia ada kuwa mwanasayansi tena wa kiwango cha Phd sasa haya anayosema kweli kulikuwa kuna haja ya yeye kupoteza huo muda woote shuleni na gharama kubwa zoote kuanza kutukumbusha elmu akhera na ndumba kweli kutibu milipuko ya magonjwa??????!!!!! Manake katika walioamini mambo ya semunge na yeye yumo na matokeo yake hamtaki hata kukumbushwa.

Sibora angekuwa mganga toka awali
 
Back
Top Bottom