Uchambuzi Wa Habari: Magufuli, Kitila Na Hema..

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Nilipata Kuandika kupitia ukurasa wangu wa facebook, kuwa inavyoonekana, Magufuli ana uwezo wa kumwona bata na sungura kwa wakati mmoja..! ( Novemba 30, 2015)

Si muda mrefu tumemsikia mwanazuoni Profesa Kitila Mkumbo akimnanga Magufuli. Tukamsikia na kumsoma Profesa akikosoa Rais kuteua wanazuoni ambao wangebaki kwenye taaluma zao.

Nilipomsikiliza ndugu yangu Kitila niliyaona ni maoni yake yenye kujenga lakini haikuondoa ukweli kuwa Rais kuteua wanazuoni kushika nyadhifa si jambo baya. Inafanyika duniani kote.

Teuzi ya Magufuli kwa Profesa ni ya kistratejia. Katika siasa ili kiongozi upate nafasi ya kufanya wananchi wanayokutaka kufanya wakati mwingine unawaingiza wakosoaji wako kwenye hema lako. Mkosoaji kwenye hema lenye tundu unapomwacha nje ya hema anaweza akijisikia haja ndogo na kwa hasira anaweza kukulowesha uliye ndani ya hema, kwa haja ndogo kupitia tundu la hema. Lakini, mkiwa kwenye hema moja, atalifanya hilo kutokea hemani kwa kuwalenga walio nje ya hema. Hiyo nayo ni siasa.

Profesa Kitila Mkumbo sasa ni ' Mserikali' haswa. Ndiye aliyekabidhiwa Wizara kama mtendaji mkuu. Ndiye atakayemsaidia waziri kwa kumshauri na kuyapanga ya kwenda kusema bungeni na hata kuzikabili hoja za wapinzani, ikiwamo wa Chama alichokuwa mwanachama na mshauri wake mkuu, ACT.

Kwa Magufuli, huo ni uwezo wa kiongozi kuyaona mambo katika sura nyingi. Si kila anayekupinga ni adui yako kiasi cha kushindwa kukaa naye kwenye hema moja.

Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana. Hivyo, inahusu uwezo kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti.

Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti.
Kuna wanaoema haijawahi kutokea. Ni kweli haijawahi kutokea na imechelewa kutokea. Maana, Magufuli yeye anamaanisha tunaposema tunajenga nyumba moja, haina maana ya kugombania fito. Ni lazima tubadilike.

Katika hili, mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.
Maggid Mjengwa
0754 678 252
 

Attachments

  • 2.jpg
    2.jpg
    7.7 KB · Views: 36
Umeandika ki-Profesa, na wasiwasi kama wengi wetu humu wa form 4 tutaelewa. Uko sahihi kabisa
 
LAKINI ana uelewa wa mambo ya kilimo na maji,,,;km ndio fani yake basi sio mbaya atamshauri vizuri waziri husika na kuleta tija
 
Mwache na yeye akatembelee kilimo kwanza na apewe nyumba Masaki...Mkuu..Tanzania ni yetu wote.

Kelele zote ni pale unapokuwa hujaambiwa nawa mikono ujongee mezani!
 
Back
Top Bottom