Ndugu zangu,
Aprili 13 itabaki kuwa siku ya kukumbumbukwa na Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yetu. Huu ni wakati wa kuizunguka bendera yetu.
Haijawahi kutokea na hatutotaka kuona ikitokea tena kwenye Jamhuri yetu ya Muungano. Kundi la wahalifu halipaswi kuachwa likazaa wahalifu zaidi wa kufanya matendo haya maovu ya kishenzi na kijambazi; kuwaua viongozi wa wananchi na askari wetu.
Tuna imani na utendaji kazi wa Polisi wetu . Ni polisi wenye kujitoa kulinda maisha na mali za wananchi. You simply don't kill a police- Polisi humuui, basi.
Hivyo, kitendo cha kuwavamia na kuwaua polisi wetu kina maana ya kuwavamia Watanzania. Kwa maana hiyo, majambazi haya yenye malengo ya kuwaua polisi wetu na kuwanyang'anya silaha, kimsingi ni wachache na ni waoga. Hivyo, yanapaswa kuangamizwa kwa nguvu zote. Na kazi ya kuwaangamiza haiwezi kufanikiwa ikiachwa ifanywe na polisi wetu tu. Ni kazi yetu sote, popote tulipo. Ni muhimu sana kusaidia kazi ya kuwapata na kuwakamata viongozi wa mtandao huo wa ujambazi.
Yumkini moja ya malengo ya majambazi haya ni kusambaza hofu kwetu Watanzania. Hofu hii ihamie sasa kwao. Maana, kwa umoja wetu na mapenzi kwa nchi yetu taarifa zao zitapatikana kutoka kwa raia wema, hivyo, wenye kuratibu ujambazi huu lazima wapatikane kwa kuamini uwezo wa jeshi letu la polisi na vyombo vingine vya usalama.
Maggid Mjengwa,