Uchambuzi: Rais Magufuli hakuwa sahihi kuvaa nguo za kijeshi, vinginevyo.....

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,766
36,626
Kwanza nianze na cheo cha Amir jeshi mkuu.

Kiuhalisia cheo hiki hakina hakina mahusiano yoyote na vyeo vinavyopatikana katika ngazi za kijeshi! Hiki hata mtu ambaye hajui nini maana ya jeshi akishakuwa rais wa nchi tu hupewa! Hakina mahusiano yoyote na vile vyeo vinavyopatikana ndani ya jeshi ambavyo mwisho wake ni Jenerali!

Mfano ingetokea kama rais Kikwete (enzi akiwa rais) leo angevaa vazi la jeshi basi angevaa katika ngazi ya ukanali ila kwa rais (e. g
angekuwa Kikwete) cheo chake cha Amir jeshi mkuu kingebaki palepale na angetambulika kwa cheo chake cha Amir jeshi mkuu!

Ni amri ya jeshi kuwa mtu anapokuwa katika vazi la jeshi basi awe kirasmi! Kuendana na cheo chake. Ila hii haiondoi maana kuwa mtu akivua lile vazi basi cheo chake hakitambuliki! La hasha! Ila msisitizo ni pale unapokuwa ndani ya lile vazi basi uwe rasmi ndani ya mfumo wa jeshi la wananchi!

Mathalan Mwamunyange akiwa kiraia bado ni mkuu wa majeshi na anapewa sifa zote za ukuu wa majeshi! Ila akiwa ndani ya vazi la jeshi ni lazima awe ndani ya vazi rasmi linalotambua cheo chake ndani ya mfumo wa jeshi (Jenerali)

Kwanini rais Magufuli hakuwa sahihi?
Mbali na kuwa bado ni Amir jeshi mkuu, rais Magufuli hana cheo chochote ndani ya mfumo wa jeshi! Hajawahi kuwa ndani ya jeshi la wananchi kama mwana jeshi! Lile vazi ni la mwanajeshi wa kawaida ndani ya jeshi la wananchi! Kwa maana nyingine rais Magufuli pale alikuwa ndani ya mfumo wa jeshi! Labda tuambiwe kuwa alipoenda Monduli naye alitunukiwa cheti cha kufuzu mafunzo ya kijeshi ndani ya JWTZ!

Vinginevyo rais atakuwa amevaa lile vazi kama wanavyofanya kina Diamond ambapo ni kinyume na taratibu za jeshi na ndo maana wanapigwa marufuku!

Nadhani mmekuwa mkimwona Kikwete enzi akiwa rais alikuwa akitoa saluti kwa viongozi wenzake! Pale alikuwa akitumia mfumo rasmi wa jeshi kwa wakubwa zake kijeshi (Ingawa cheo chake cha Amir jeshi mkuu kilikuwa palepale) hivyo alikuwa hakosei kufanya hivyo!

Narudia tena: cheo cha Amir jeshi mkuu hakipo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi. Hata mtoto mdogo akiwa rais wa nchi basi cheo hicho kinafuatia palepale!

Pia inashauriwa kuwa si vyema sana rais wa nchi ambaye amechaguliwa kwa kura kuwa ndani ya mavazi rasmi ya kijeshi kutokana na cheo chake! Hii inazua mkanganyiko wa heshima za kijeshi zinazotolewa! Mathalan Kikwete leo angeamua kuvaa vazi rasmi la kijeshi huku akiwa rais basi angeishia cheo cha kanali! Hapo yupo ndani ya vazi rasmi la jeshi kisha anapokea saluti kutoka kwa jenerali! Hii siyo sawa! Rais wa nchi anabaki kuwa Amir jeshi mkuu hii haijalishi kuwa amepita na/au hajapita jeshini! Kinacholeta mkanganyiko ni lile vazi rasmi la jeshi!

Huwa wanasema "ukiwa nje ya lile vazi utaheshimiwa kwa cheo chako kijeshi, ukiwa ndani ya vazi utaheshimiwa kutokana na vazi" na ndo maana mtu akiwa ndani ya lile vazi basi anawekewa vyeo vyake kijeshi lakini akiwa nje ya vazi hawekewi vyeo vyake ila bado anatambulika maisha yake yote!

Kwa hiyo kuna mawili! Eidha rais Magufuli ameanza rasmi mafunzo ya kijeshi na ana cheo cha chini kabisa kijeshi na/au alivaa lile vazi kama watu wengine! Ikiwa hilo la pili ni kweli basi hakuwa sahihi kutokana na kuvaa vazi rasmi la JWTZ bila kuwa ndani ya mfumo wa jeshi!
Ikiwa hilo la kwanza ni sahihi basi yuko sawa na cheo chake cha Amir jeshi mkuu bado kipo palepale ila kwa hapo yupo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi!

G Sam
 
Hoja yako umewaisilisha vizuri lakini bado inakosa uhalisia/uhalali kwa kukosa uthibitisho ama wa kanuni, taratibu, miongozo au sheria inayotawala eneo hilo.
 
Kabla haujaenda mbali na thread yako ndefu, je wewe ni mwanajeshi ama una taaluma ya kijeshi? Au ni raia tu?
 
Mkuu kwani unafikiri zile pushap wakati wa kampeni zilikuwa za nini? Yale yalikuwa mazoezi na ndo alishafuzu sasa.

BTW, haina athari yoyote kimaendeleo, kiuchumi wala kimaadili
 
Alitakiwa anyoe kabisa na "o" yake. kutofuga ndevu za kidevuni na kuwa na nywele fupi ni sehemu ya urasmi wa vazi la kijeshi. mustachi unaruhusiwa...
 
Mi hata sioni ishu iko wapi kwa yeye kuvaa miyo migwanda iliyokuwa mikubwa kumzidi.
 
Rais kuwa amiri jeshi mkuu ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa coup kwani yeye ndio anaongoza jeshi na mamlaka yote na maamuzi yote kijeshi.

Nakumbuka mwaka 2010 Obama alienda Afghanistan na kukutana na wanajeshi wake alivaa jacket la air force kama commander in Chief

Hakuna sheria inayomkataza Rais kuvaa gwanda duniani. Kwa hiyo Magufuli yupo sahihi kabisa na kuvaa hivyo kunawapa morali wanajeshi kumwona akitinga na combat na kumfurahia mtu wao
 
G Sam, mi nikusifu kwa kutetea hoja yako kwa ufanisi. Mambo mengine, ntarudi badae kidogo.
 
HII KITU IKO HIVI, KAMA WEWE NI PRO MAGUFULI, yuko sahihi, KAMA WEWE NI ANTI MAGUFULI, hayupo sahihi. Maana naona bavicha ndo wanaokataa kuwa hakuwa sahihi! Jezi kavaa, bavicha angalau mna topic ya wiki hii ila as usual, it leada to NOWHERE!!
Yaani imefika wakati ukawa mnaacha kuwa wapinzani kwa kukosa hoja sasa mnajadili matukio.
Uzuri strategists wa siaiemu wameshawajua mnapenda nini, wiki ijayo wanawanyuka na tukio lingine!
HAPA KAZI TU.
 
Kwanza nianze na cheo cha Amir jeshi mkuu.

Kiuhalisia cheo hiki hakina hakina mahusiano yoyote na vyeo vinavyopatikana katika ngazi za kijeshi! Hiki hata mtu ambaye hajui nini maana ya jeshi akishakuwa rais wa nchi tu hupewa! Hakina mahusiano yoyote na vile vyeo vinavyopatikana ndani ya jeshi ambavyo mwisho wake ni Jenerali!

Mfano ingetokea kama rais Kikwete (enzi akiwa rais) leo angevaa vazi la jeshi basi angevaa katika ngazi ya ukanali ila kwa rais (e. g
angekuwa Kikwete) cheo chake cha Amir jeshi mkuu kingebaki palepale na angetambulika kwa cheo chake cha Amir jeshi mkuu!

Ni amri ya jeshi kuwa mtu anapokuwa katika vazi la jeshi basi awe kirasmi! Kuendana na cheo chake. Ila hii haiondoi maana kuwa mtu akivua lile vazi basi cheo chake hakitambuliki! La hasha! Ila msisitizo ni pale unapokuwa ndani ya lile vazi basi uwe rasmi ndani ya mfumo wa jeshi la wananchi!

Mathalan Mwamunyange akiwa kiraia bado ni mkuu wa majeshi na anapewa sifa zote za ukuu wa majeshi! Ila akiwa ndani ya vazi la jeshi ni lazima awe ndani ya vazi rasmi linalotambua cheo chake ndani ya mfumo wa jeshi (Jenerali)

Kwanini rais Magufuli hakuwa sahihi?
Mbali na kuwa bado ni Amir jeshi mkuu, rais Magufuli hana cheo chochote ndani ya mfumo wa jeshi! Hajawahi kuwa ndani ya jeshi la wananchi kama mwana jeshi! Lile vazi ni la mwanajeshi wa kawaida ndani ya jeshi la wananchi! Kwa maana nyingine rais Magufuli pale alikuwa ndani ya mfumo wa jeshi! Labda tuambiwe kuwa alipoenda Monduli naye alitunukiwa cheti cha kufuzu mafunzo ya kijeshi ndani ya JWTZ!

Vinginevyo rais atakuwa amevaa lile vazi kama wanavyofanya kina Diamond ambapo ni kinyume na taratibu za jeshi na ndo maana wanapigwa marufuku!

Nadhani mmekuwa mkimwona Kikwete enzi akiwa rais alikuwa akitoa saluti kwa viongozi wenzake! Pale alikuwa akitumia mfumo rasmi wa jeshi kwa wakubwa zake kijeshi (Ingawa cheo chake cha Amir jeshi mkuu kilikuwa palepale) hivyo alikuwa hakosei kufanya hivyo!

Narudia tena: cheo cha Amir jeshi mkuu hakipo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi. Hata mtoto mdogo akiwa rais wa nchi basi cheo hicho kinafuatia palepale!

Pia inashauriwa kuwa si vyema sana rais wa nchi ambaye amechaguliwa kwa kura kuwa ndani ya mavazi rasmi ya kijeshi kutokana na cheo chake! Hii inazua mkanganyiko wa heshima za kijeshi zinazotolewa! Mathalan Kikwete leo angeamua kuvaa vazi rasmi la kijeshi huku akiwa rais basi angeishia cheo cha kanali! Hapo yupo ndani ya vazi rasmi la jeshi kisha anapokea saluti kutoka kwa jenerali! Hii siyo sawa! Rais wa nchi anabaki kuwa Amir jeshi mkuu hii haijalishi kuwa amepita na/au hajapita jeshini! Kinacholeta mkanganyiko ni lile vazi rasmi la jeshi!

Huwa wanasema "ukiwa nje ya lile vazi utaheshimiwa kwa cheo chako kijeshi, ukiwa ndani ya vazi utaheshimiwa kutokana na vazi" na ndo maana mtu akiwa ndani ya lile vazi basi anawekewa vyeo vyake kijeshi lakini akiwa nje ya vazi hawekewi vyeo vyake ila bado anatambulika maisha yake yote!

Kwa hiyo kuna mawili! Eidha rais Magufuli ameanza rasmi mafunzo ya kijeshi na ana cheo cha chini kabisa kijeshi na/au alivaa lile vazi kama watu wengine! Ikiwa hilo la pili ni kweli basi hakuwa sahihi kutokana na kuvaa vazi rasmi la JWTZ bila kuwa ndani ya mfumo wa jeshi!
Ikiwa hilo la kwanza ni sahihi basi yuko sawa na cheo chake cha Amir jeshi mkuu bado kipo palepale ila kwa hapo yupo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi!

G Sam

Umejaza maneno matupu na blah blah zisizo na ukweli.

Kwa mujibu wa Katiba yetu, mtu akiwa Rais anakuwa sehemu ya Jeshi ie Amiri Jeshi Mkuu.

Ndiye anatoa amri mbalimbali za utendaji, kivita, utawala na kutoa madaraka na vyeo jeshini.

Kimsingi inatakiwa kubuniwa shoulder titles za Rais km walivyofanya Kenya, USA nk
 
Mleta mada, G Sam hebu naomba ufafanue unaposema Mh. Rais hakuwa sahihi kwa sababu hayupo rasmi ndani ya mfumo wa jeshi unamaanisha nini? Je nani ana mamlaka ya kuunda vikosi na muundo wa jeshi? Je nani ana mamlaka ya kusimamisha madaraka ya mwanajeshi yoyote yule bila kujali cheo chake? Hebu jaribu kusoma vinzuri katiba ya nchi juu ya uwepo na madaraka ya amiri jeshi mkuu halafu ndipo uje na hiyo hoja yako.

Sehemu ya Katiba kuhusu Amiri jeshi mkuu
148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au nje ya Tanzania.
(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayo yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani-
(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi ya ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(b) madaraka ya kuwateua watu watakaojiunga na majeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshini wanajeshi;
(c) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongoza vikosi mbali mbali vya majeshi ya ulinzi; na
(d) madaraka ya kumwamuru mwanajeshi yeyote asitumie madaraka yoyote aliyokabidhiwa na ambayo yanaambatana na kuwa kwake mwanajeshi.
(3) Jambo lolote atakalotenda mwanajeshi yoyote kinyume cha amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2) ya ibara hii litakuwa batilifu.

TUKIJA KWENYE TANZANIA NATIONAL DEFFENCE ACT
15.-(1) The President may appoint an officer to be Chief of the Defence Forces.
(2) The Chief of the Defence Forces shall, subject to the powers of the President and the Minister and to the directions of the Defence Forces Committee as respects any matter for which it has responsibility, have the command, direction and general superintendence of the Defence Forces.
(3) Unless the President otherwise directs, all orders and instructions to the Defence Forces which are required to give effect to the decisions and to carry out the directions of the Government of Tanzania, the Minister, or the Defence Forces Committee shall be issued by or through the Chief of the Defence Forces.
 
Back
Top Bottom